Kanuni 28 za kuishi na Watu / Binadam Vizuri

Kanuni 28 za kuishi na Watu / Binadam Vizuri

Nani kakudanganya?

kuna watu wana nyota tu ya kupendwa

nawajua watu unakuta tapeli..,malaya...muongo muongo..
but ana marafiki kila kona...
anapendwa na kila mtu....
akipatwa na shida unaona watu tele wanakuja kumsaidia..

watu wa hivyo hata akikutapeli ukienda kumshtaki watu wanakuona wewe
ndo 'mnoko' huna roho ya kusamehe mambo madogo...

tembea uone...
toa mfano mmoja
 
Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani.

Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani.

Zifuatazo ni KANUNI na MBINU muhimu za kuishi na watu vizuri.
1: Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda.
2: Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana.
3: Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha juu na kadhalika.
4: Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu.
5: Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe.
6: Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjenga.
7: Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya.
8: Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu.
9: Shukru kwa kila jambo jema linapotendeka kwa kusema ahsante au shukru kwa kila jambo._
10: Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa.
11: Usipende mabishano na kama yakitokea,usitake kila mara kushinda.
12: Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu.
13: Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu.
14: Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu.
15: Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki.
16: Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea.
17: Usiwe unachonganisha watu,ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema.
18: Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo.
19: Tunza siri zako na za wengine.
20: Usiwe mwepesi wa hasira
21: Kumbuka majina ya watu unaokutana nao.
22: Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri.
23: Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli.
24: Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda.
25: Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika.
26: Jifunze kusamehe makosa ya watu.
27: Unapofanya makosa,kubali na kuungama na kuomba msamaha.
28: Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako.
Shukran kwa Uzi huu
 
Wakati MGUMU SANA katika Maisha ni ile point kila mtu unamuona Mbaya

No matter how much you are trying to be GOOD GUY to people (them)

Depression is Realy
 
kila mtu hapa anamlaumu kila mtu,
kila mtu anasema binadamu wabaya.

anyway mimi ndo huyo binadamu sasa,.
 
Back
Top Bottom