Kansa ya kibofu cha mkojo (prostate cancer) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kansa ya kibofu cha mkojo (prostate cancer)

Discussion in 'JF Doctor' started by kanyagio, Oct 23, 2011.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  wanandugu, nimefurahi sana na JF doctor forum jinsi watu wanavyotoa maelezo mbalimbali ya afya.

  ninaomba mwenye maelezo yakinifu kama ya MziziMkavukuhusu kuzuia ugonjwa wa kansa ya kibofu cha mkojo (prostate cancer) hasa kwa kutumia njia na vitu vya asili tulivyo navyo katika mazingira yetu (including lifestyle) naomba atujuze.

  natanguliza shukrani
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Saratani ya tezi kibofu cha mkojo (Prostate)

  Saratani ya mamalia dume (tezi kibofu) huwa kati ya wanaume. Huweza kutibiwa inapogunduliwa mapema. Ugonjwa huu huwaambukiza wanaume walio na umri wa miaka 55 na zaidi. Mamalia dume hutengeza manii ambayo mbegu za kiume hupatikana. Huambukiza chini ya kibofu cha mikojo.
  Wanaume wengine wamo hatarini kupata saratani ya mamalia dume:
  • Walio na umri wa miaka 55 na zaidi
  • Wanaume ambao wamekuwa na jamaa kama baba au kaka ambao washauguwa ugonjwa huu.
  • Wanaume weusi.
  • Kula vyakula vingi vya mafuta, nyama nyekundu, siagi na maziwa.
  Dalili ya saratani ya mamalia dume:
  • Kukojoakojoa kila mara hasa wakati wa siku.
  • Kuwa na shida za kuanza kukojoa au kusitiri mikojo.
  • Kukojoa kwa matone matone.
  • Kuhisi uchungu au moto unapokojoa
  • Kuwa na shida kusimika.
  • Kuhisi uchungu unapomwaga manii.
  • Kukojoa mikojo iliyochanganyika na damu.
  • Maumivu ya kila mara hasa sehemu za mgongo,nyonga au mapajani sehemu za juu.
  Daktari wako anaweza kukufanyia uchunguzi kutambua kama una saratani ya mamalia dume.Kwa kutumia kemikali ya “Prostate specific antigen” au PSA katika damu yako, ikiwa una idadi ya juu ya PSA , waweza kuwa na ugonjwa huu.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Saratani ya Makodo (Testicular)

  Saratani ya makodo au mapumbu ndio inayojulikana sana hasa kwa vijana barubaru wa kati ya miaka 15 hadi 35. Habari njema ni kuwa saratani ya makodo ni haba sana na inatibika.

  Licha ya kutoa mbegu za uzazi, makodo pia hutengeza homoni za kiume. Makodo ni laini, mviringo na ngumu. Wanaume wanahitaji kujikagua wenyewe mara kwa mara kila mwezi kutambua mabadiliko.

  Wanaume wengine wamo hatarini zaidi mwa kupata saratani ya makodo:

  • Watoto wa kiume waliozaliwa na makodo isiyo ning’inia chini.
  • Wanaume ambao makodo yao hayakumea kawaida.
  • Wanaume waliozaliwa na Klinefelter’s Syndrome (Hali ya mvulana kuzaliwa na chromosome zaidi ya 46 iliyo kawaida. Akikua mwili wake una dalili za uke kama vile matiti na kutokuwa na nywele usoni)
  Dalili za Saratani ya Makodo
  • Uvimbe usiyo na uchungu kwa kodo
  • Uchungu ndani ya kodo
  • Kodo kuwa ngumu na kubadilika kwa saizi. (Kuvimba au kurudi). Kuhisi uzito kwa mapumbu (mfuko wa makodo)
  • Uchungu usio mkali kwa manena na sehemu ya chini ya tumbo.
  • Matiti kuwa makubwa au kuuma.
  Hizi pia zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengine ambayo si saratani. Ukihisi dalili yoyote ya hizi, muone daktari.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  KAHAWA YAPUNGUZA UWEZEKANO WA KANSA YA KIBOFU.

  coffee7.jpg  Picha; VOA. Kahawa ni kinywaji kikubwa katika nchi za Afrika Mashariki na Ethiopia.
  "wanaume wanaokunywa vikombe sita au zaidi vya kahawa kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata kensa hiyo kwa asilimia 60 ukilinganisha na wanaume wasiokunywa kabisa kahawa."

  Utafiti mpya uliofanywa kwa kushirikisha wanaume elfu 50 unasema kuwa watu wanaokunywa kahawa kwa wingi wana nafasi nzuri ya kuepukana na saratani au kensa ya tezi la kibofu cha mkojo.
  Kwa muda wa zaidi ya miaka 20 kumekuwa na imani kuwa unywaji kahawa unasaidia katika kuepusha kensa hiyo, lakini katika tafiti huu mpya wanasayansi wanasema wamegundua tofauti kubwa katika kuepusha saratani kali.
  Mwanasayansi Kathryn Wilson wa Idara ya afya ya umma ya chuo kikuu cha Havard nchini Marekani anasema "wanaume wanaokunywa vikombe sita au zaidi vya kahawa kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata kensa hiyo kwa asilimia 60 ukilinganisha na wanaume wasiokunywa kabisa kahawa."
  Kahawa ina kemikali mbali mbali, ikiwa na viambatisho vinavyopambana na magonjwa na hiyo huenda ni pamoja na kemikali zinazozuia kensa ya tezi la kibofu cha mkojo.
  Kensa hiyo ni ya pili kwa kuuwa wanaume duniani, ikiwa inasababisha vifo vya watu wapatao robo millioni kwa mwaka.
  Dr. Wilson na wenzake walichapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la kisayansi la "Journal of the National Cancer Institute."
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Matatizo ya kibofu yanaweza kutibika kwa chakula!

  MATATIZO YA KIBOFU YANAWEZA KUTIBIKA KWA CHAKULA! [​IMG]
  Matatizo ya kiafya katika kibofu cha mkojo yamekuwa mengi hivi sasa, hasa kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 50. Kazi kubwa ya kibofu ni kusaidia ukuaji wa mbegu za kiume, kama kibofu kikiwa na matatizo, uzalishaji wa mbegu za kiume nao hupungua sana na tatizo lisipotibiwa haraka, husababisha ugumba. Aina nyingine ya matatizo ya kibofu husababisha uvimbe sehemu za siri.Inaelezwa kuwa matatizo ya kibofu mara nyingi huwa ni ya kurithi, ingawa kuna sababu nyingine pia.

  Ugonjwa unaweza kusambaa ukoo mzima, kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Sababu nyingine zinazosababisha ugonjwa huu zinaelezwa kuwa ni kukaa kwa muda mrefu, kuvaa nguo zinazobana, ukosefu wa choo na maambukizi. Kupenda kujamiina sana nako kunaelezwa kuwa ni sababu moja wapo. Pamoja na ukubwa wa tatizo hili ambalo husababisha kansa pia, kuna habari njema kuwa matatizo madogo ya kibofu yanaweza kutibiwa nyumbani kwa kula vyakula na kufuata kanuna kadhaa na mtu akapona kabisa au akazuia isimpate, lakini iwapo tatizo limeshakomaa na kuwa sugu, unashauriwa kwenda hospitali na kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.

  UTAJUAJE UNA TATIZO?
  Dalili moja wapo ya mtu mwenye tatizo la kibofu ni kusikia maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo. Dalili nyingine ni kushindwa kukojoa kabisa licha ya kuhisi kubanwa na mkojo. Dalili nyingine ni kusikia maumivu chini ya mgongo na kwenye ‘hips’. Kwa kuwa mtu huwezi kujipima kama una tatizo hilo, ina shauriwa kwenda hispitali kupima. Saratani ya kibofu ni miongoni mwa matatizo yanayoweza kujitokeza na inaweza kuuawa!

  DONDOO ZA TIBA MBADALA..
  Tiba mbadala ya matatizo ya kibofu hufanyakazi vizuri na imeonesha mafanikio makubwa kwa watu waliowahi kujaribu. Mbegu za maboga ni miongoni mwa tiba mbadala za kutibu matatizo ya kibofu. Pondaponda kiasi cha mbegu 15 hadi 20 za maboga na changanya kwenye mlo wako wa kila siku.Utaona mabadiliko ya haraka ya unafuu ndani ya wiki mbili hadi tatu. Vitamini E ni kirutubisho muhimu sana katika kutibu matatizo ya kibofu. Aidha, mboga za majani rangi ya kijani, mayai na bidhaa zitokanazo na maziwa nazo zina kiwango kikubwa cha vitamin E, hivyo viliwe kila siku.Dawa nyingine mbadala ya matatizo ya kibofu ni enema ya maji ya uvugu.

  Enema ya aina hii ifanywe mara mbili au tatu kwa wiki ili kurejesha utendaji wake wa kawaida. Uvutaji sigara na unywaji pombe hauruhusiwi kabisa wakati wa kufanya tiba hizi, hali kadhalika vyakula vilivyoungwa sana. Mwisho, inashauriwa sana kuacha kunywa vinywaji vyote vyenye ‘caffeine’, hii ni pamoja na chai na kahawa, kwa sababu huzalisha matizo zaidi. Mazoezi ya nusu saa ya kukimbia au kuendesha baiskeli yatasaidia zaidi. Kwa kuwa baridi ni miongoni mwa sababu zinazochangia maradhi ya kibofu, mgonjwa anayeishi sehemu yenye baridi anashauriwa kuhamia sehemu yenye joto.

  Chanzo: https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/45782-matatizo-ya-kibofu-yanaweza-kutibika-kwa-chakula.html
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kuweka tu rekodi sawa....kansa ya kibofu cha mkojo (carcinoma of the urinary bladder) ni tofauti kansa ya tezi ya mamalia dume (prostate cancer). Kama mchoro unavyoonyesha hapo juu, kibofu cha mkojo ni sehemu tofauti na ina kazi tofauti na prostate. Na hivyo hata risk za kansa ya kibofu na kansa ya prostate no tofauti pia.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Ngoja niwachomekee hapa hapa. Napata mixed info kuhusu pioglitazone, that uk na russia it is banned kwa sababu inasababisha kansa ya kibofu cha mkojo. Bt in south africa and of coz tz bado inatumika. Riwa na mzizi plz help.mtandaoni sijaona hii info
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Nasikia kujichua kunapunguza risk ya prostrate cancer...mnasemaje madaktari
   
Loading...