Kanisa Tanzania ni CCM?

Kanisa Tanzania ni CCM?

Kanisa katoliki limezidi, yaani wataki wa utawala wa kikwete walikuwa wanatoa nyaraka Mbali mbali kwa kuwa hakuwa mhumini wao, lakini kwa sasa wako kimya mbali na maovu yanayo fanywa na serikali hii kwa sababu mtu flani ni mshirika wao kweli huu ni ukafili na siyo dini
Ukweli Mchungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani tupoteze muda wetu kuwaombea akina tundulisu na mbowe? Si bora muda huo ningeenda kuangalia mapilau
 
Maaskofu na Wachungaji wa Tanzania ni wanagiki, waoga na wenye tabia ya kujipendekeza kwa serikali. Wanaogopa kuikosoa, wanasifu viongozi daima. Mimi ni mkristo pia. Tabia hii inanikera kwa kuwa inaambukiza watu wengi hasa wa vijijini na wanawake wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maaskofu wetu bure kabisa!!

Askofu.jpg
 
Askofu Msaidizi wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Katanga katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Elisha Tendwa amesema baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa wakitoa malalamiko juu ya utawala wa Rais John Magufuli siku moja wangefika Congo wasingethubutu kutoa lawama hizo.

Amesema kuwa ni vema kabla ya watu kutoa lawama kwa Serikali juu ya mambo mbalimbali ni vema wakalinganisha na kufanya tathmini juu ya hali ilivyo kwa nchi nyingine ikiwemo nchi ya DRC.

Kwa Hisani ya Majs aliyelileta hili bandiko JF
 
Piga picha Lissu angekuwa ni Mbunge toka CCM! Leo Maaskofu wangetoa matamko huku kofia zao zikiwa mikononi!
 
Kwanza nitangaze kabisa Maslahi binafsi kwenye hoja yangu hii. Mimi ni Mkristo na hapa ninaposema "Kanisa" namaanisha mjumuiko wa wakristo na wala sizungumzii "madhehebu". Kwa ivo ninaposema Kanisa namaanisha mjumuiko wa wakristo wote waliomo kwenye madhehebu mbali mbali hapa Tanzania.

Kwa muda mrefu sana madhehebu mbali mbali yamekuwa yakiandaa mikesha ama matamasha ya "amani" kuombea nchi yetu. Jambo la kushangaza haijawahi hata kwa bahati mbaya kutokea kwenye matamasha hayo waandaaji wakawaalika wanasiasa toka vyama vya upinzani kuwa wageni Rasmi. Hao waandaaji wanaposema wanaombea amani wanamaanisha ni dhidi ya wapinzani? Au mungu wao anawaonesha kwamba amani inaletwa na CCM?

Mwezi uliopita ulikuwa ni kama mwezi wa mashindano ya mikutano ya kumuombea Rais John Magufuli. Lakini huwezi kuona wanaokimbizana leo kumuombea Magufuli wakifanya hivyo kwa viongozi wa vyama vya upinzani. Jee vyama vya upinzani viongozi wake hawatakiwi kuombewa ili wapate "ulinzi" wa Mungu. Ama mungu wa Maaskofu si Mungu wa viongozi wa vyama vya upinzani?

Wakati wa Uchaguzi utawasikia Maaskofu wakitoa salamu za "uchaguzi" kwa kutumia kauli mbiu zinazotumiwa na CCM. Wao "amani na utulivu" ni pale tu CCM inapobakia madarakani. Na baada ya uchaguzi hata kama kuna watu wanadai kudhulumiwa haki yao ya ushindi utawasikia Maaskofu wanasema "tunashukuru mungu" uchaguzi umepita kwa amani.

Hivi msimamo wa hawa viongozi wa Kanisa kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar ulikuwaje? Au waliamini alichokisema Lukuvi?

Pole.90%Ya viongozi wa Dino zote ni wanachama hai wa CCM.

Naona hata Mungu wanaomuabudu hawa watu anakadi ya CCM, siku watakapokuja viongozi wa Dino wenye Mungu asiye na Chama tuyaona tofauti yake.

Hawa hukimbilia kusema Chaguo la Mungu anapoharibu hukaa kimya kama wamemwagiwa Maji baridi.
 
Siasa zipi maombi sio siasa.

Ni kweli Maombi siyo SIASA pale yanapokuwa hapo upande wa CCM. Yanapokuwa upande wa pili ni SIASA.

Hongera Mwanachama wa Chama Cha Mauaji
 
Siasa na dini ni njia za kummiliki, kumtawala na kumtumikisha mlalahoi. Jasho la mlalahoi huliwa kwa njia nyingi zilizohalalishwa kwa namna moja au nyingine.
Hata hivyo, hali huwa mbaya zaidi vitu hivyo vinapoungana moja kwa moja.
 
ulichoandika hakina tofauti na yule mtu anaekwenda kuomba kanisani kusamehewa dhambi na wakati huohuo anasema kwmaba,eti yesu alichukua dhambi zake pale msalabani
 
Back
Top Bottom