Kwanza nitangaze kabisa Maslahi binafsi kwenye hoja yangu hii. Mimi ni Mkristo na hapa ninaposema "Kanisa" namaanisha mjumuiko wa wakristo na wala sizungumzii "madhehebu". Kwa ivo ninaposema Kanisa namaanisha mjumuiko wa wakristo wote waliomo kwenye madhehebu mbali mbali hapa Tanzania.
Kwa muda mrefu sana madhehebu mbali mbali yamekuwa yakiandaa mikesha ama matamasha ya "amani" kuombea nchi yetu. Jambo la kushangaza haijawahi hata kwa bahati mbaya kutokea kwenye matamasha hayo waandaaji wakawaalika wanasiasa toka vyama vya upinzani kuwa wageni Rasmi. Hao waandaaji wanaposema wanaombea amani wanamaanisha ni dhidi ya wapinzani? Au mungu wao anawaonesha kwamba amani inaletwa na CCM?
Mwezi uliopita ulikuwa ni kama mwezi wa mashindano ya mikutano ya kumuombea Rais John Magufuli. Lakini huwezi kuona wanaokimbizana leo kumuombea Magufuli wakifanya hivyo kwa viongozi wa vyama vya upinzani. Jee vyama vya upinzani viongozi wake hawatakiwi kuombewa ili wapate "ulinzi" wa Mungu. Ama mungu wa Maaskofu si Mungu wa viongozi wa vyama vya upinzani?
Wakati wa Uchaguzi utawasikia Maaskofu wakitoa salamu za "uchaguzi" kwa kutumia kauli mbiu zinazotumiwa na CCM. Wao "amani na utulivu" ni pale tu CCM inapobakia madarakani. Na baada ya uchaguzi hata kama kuna watu wanadai kudhulumiwa haki yao ya ushindi utawasikia Maaskofu wanasema "tunashukuru mungu" uchaguzi umepita kwa amani.
Hivi msimamo wa hawa viongozi wa Kanisa kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar ulikuwaje? Au waliamini alichokisema Lukuvi?