Kanisa Tanzania ni CCM?

Viongozi wengi wa dini wanafki waoga na wana njaa mno

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 


Kati ya thread zenye nguvu, zilizojaa ukweli na umuhimu hii ni moja wapo. kwa kutangaza maslahi binafsi mimi ni mkristo, na ninaujua ukristo halisi. kanisa limekuwa na tabia mbaya sana ya kufikiri ccm ndio wenye hati miliki na ndio raia halali wa tanzania maana hata wapinzani wanapoonewa na kunyanyaswa hakuna kiongozi yeyote wa kanisa ambaye amewahi kujitokeza hadharani kukemea. kazi kubwa ya viongozi wa kanisani tangu zamani haikuwa kuisifia serikali.. ukisoma Biblia nzima viongozi wa kiroho hawakuwasifia watawala, pale walipofanya vizuri walinyamaza kimya ila pale walipokosea waliwakemea tena hadharani. Bwana Yesu alikwenda mbali kumwita mfalme Herode mbwea. Yohana alimkemea Herode hadi akakasirika hadi kumfunga gerezeni.

Kanisa la Tanzania limeshindwa kufahamu kuwa viongozi wa upinzani nao ni viongozi wa kisiasa kama walivyo ccm
 
Waovu huweza kutumia siasa au dini kuendeleza nia zao na kutekekeleza uhalifu na unyonyaji dhidi ya uma.
Hali huwa mbaya zaidi pale wanaotumia vivuli au maficho haya mawili (dini na siasa) wanapoungana.
Hata hivyo, wapo viongozi wa dini na siasa walio wema, lakini kimsingi taasisi zao zina asili ya kumtumikisha na kumnyonya mlalahoi.
 
[emoji21][emoji21][emoji21]

Sent from my HUAWEI Y330-U01 using JamiiForums mobile app
 
Wanavutiwa mshiko mkubwa sana na viongozi wa serekali inamaana hujui kama msaidizi wa kardinali pengo na askofu kilain wana kashifa ya wizi wa pesa za umma?

Sent from my Fero L100 using JamiiForums mobile app
 
Mbona unauliza majibu ?
Kwenye ile Ibada ya mazishi Askofu kasema "kuna watu hawana shukrani kwa maendeleo yanayoletwa na serikali ya awamu ya Tano". Hotuba yenye madubwana kama haya kwenye msiba yanamfariji mfiwa kweli? Au "baba'" Askofu naye aliamua kuleta siasa msibani kwa kuwa eti inasemwa kuwa hata Marehemu mwenyewe kabla hajafa alitelekezwa kwa mambo ya siasa vile vile?
 
Nimemdharau sana askofu yule , mlokole gani mwongo kiasi kile ?
 
Hakuna watu wanafki kwa nchi hii kama sisi wakiristo hasa RC......yaani kimya kama hakuna yanayoendelea nnchini....
wakati wa JK ilikuwa kila siku matamko kwel dini yake ilimponza mzee JK we mic u babu
 

Umeongea kitu ambacho hata Mimi huwa ninakishangaa.Iliposhinda CUF Kabisa halikusema Bali lizidi kutaadjarisha tuombee uchaguzi wa pili upite,je CUF nsiyo watanzania??

Nadhani labda CCM ni mbingu,itafika wakati titaacha kwenda makanisani
 

Ni aibu kuandika utumbo uliouandika.Akili yako hakuna ina Makinikia
 
Mtoa mada hayo mambo umeyafahamu leo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ndiyo nimeamua kuyaandika!

Tetty halafu ukiwa kanisani sasa wanavyohimiza tutoe sadaka hadi unashangaa. Watu wanawashutumu Wakatoliki lakini hata huku kwa wengine kuanzia Lutheran hadi wale walokole wa Petekoste nao ni kama vile wanaamini mungu wao kaiteremsha CCM itawale Tanzania.

Umewahi kusikia Kanisa wanashutumu CCM wakisema kwamba watatawala Tanzania miaka mia ijayo?
 
Sasa hivi viongozi wa dini unafiki tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wengi wa viongozi wa dini walikuwa wanachama wa CCM na wengine bado ni wanachama hivyo hawawezi kuona Chama chao Kinachofanya ,mawazo yao na akili yao kimefungwa katika AMANI bila HAKI,wakidhani kila inaachofanya CCM ni sahihi.Ati Polisi akipiga raia ni sahihi ila Raia akipiga polisi kosa la JINAI.

Polisi akiua RAIA ni sahihi ameua mtuhumiwa ,ila RAIA akijitetea akaua Polisi tunaita GAIDI
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…