Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,815
- 168,011
Jana nilienda kusali kwenye kanisa moja mitaa ya kati.
Huko mhubiri alikuwa bize kuuponda mchezo wa soka kuwa ni wa kishetani uliotawaliwa na uongo na hila.
Akasema mchezaji anapompiga chenga mwenzake anakuwa amedanganya, maana anakuwa anamdanganya kuwa anaenda kulia wakati anaenda kushoto.
Akaendelea kusema wanapoangushana na kuchezeana faulo wanakuwa wanavunja amani na wanafanya uadui.
Pia akasema wachezaji wanapojiangusha kutafuta penalt wanasema uongo.
Akatoa kali zaidi kwa kusema fifa na kombe vya dunia viliundwa na shetani mwenyewe na akavileta duniani ili kuwapofusha watu.
Watu wawe busy na mpira na kumsahau mungu.
Akawashauri waumini wake waache kabisa kufuatilia michuano ya kombe la dunia inayoendelea afrika ya kusini.
He he he..askofu kumbe kuna makanisa hayana exit door? makubwa haya!Buji unafanya survey kwenye makanisa?? utaingia mahala ambapo NO EXIT... shauri yako, we test zali tu
buji unafanya survey kwenye makanisa?? Utaingia mahala ambapo no exit... Shauri yako, we test zali tu
Mshikaji hilo ni kanisa la nabii tito
Kama hujui kitu ukikaa kimya watu watahisi kuwa hujui, lakini ukifungua mdomo na kuongea, na ukaongea uongo mtupu basi watu watathibitisha hisia zao kuwa wewe hujui!
He he he..askofu kumbe kuna makanisa hayana exit door? makubwa haya!
Bwana ehh, nilikuwa na kiu ya neno la mungu, si ndio nikajikuta najichomeka kusiko faa?
Duh, kama ni hivyo basi Messi ataenda Motoni