Kanisa lingine lachomwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa lingine lachomwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by OSOKONI, Oct 17, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Saa chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwasihi viongozi na waumini wa dini za Kikiristo na Kiislamu nchini kuwa wavulilivu na kujiepusha na vitendo vya kulipiza visasi, Kanisa la la Pentekoste (MMPT) lililopo Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji limechomwa moto na kutetekezwa kabisa na watu wasiojulikana.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku majira ya saa 4:00 usiku katika eneo la Buronge mjini Kigoma.

  Kashai alisema kanisa hilo lilichomwa na watu wasiojulikana na kwamba mali mbalimbali zenye thamani ya Sh. 1,337,000 ziliteketea.

  Alisema sababu za kuchomwa kwa kanisa hilo hazijafahamika na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa huku upelelezi wa tukio hili ukiendelea ili kuwabaini wahalifu hao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

  MCHUNGAJI ANENA


  Mchungaji wa Kanisa hilo, Emmanuel Simon, alisema:

  “Nilipata taarifa kuwa kanisa langu limeteketea kwa moto, nilikwenda Polisi Central kutoa taarifa ndipo tulikwenda eneo la tukio tukakuta kanisa lote limeteketea kwa moto.”

  Alisema katika kanisa kulikuwa na mabechi 14, mlango mmoja, virago vitatu, masanduku ya sadaka na ubao wa kufundishia, vyote vikiwa na thamani ya Sh. 1,337,000.

  Mchungaji Simon alisema hajui watu waliochoma kanisa hilo na kuiomba serikali iangalie matukio ya uchomaji wa makanisa yanayoendelea nchi nzima.

  Pia, alilitaka Jeshi la Polisi kufanya doria kwenye makanisa wakati wa usiku ili kukomesha vitendo vya uchomaji wa makanisa.

  Alisema kanisa ni taasisi ya jamii, hivyo anaomba serikali ichangie gharama ya ujenzi wa jengo hilo ili wananchi wanaoabudu katika kanisa hilo wapate sehemu ya kuabudia.

  KANISA LA WAADVENTISTA LALAANI


  Kanisa la Waadventista Wasabato limetoa tamko rasmi dhidi ya tukio la kuharibiwa kwa jengo la ibada la kanisa hilo lililoko Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuchomwa moto kwa makanisa mengine ya Kikristo na watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa Kiislamu.

  Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mjini Morogoro jana, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Mashariki mwa Tanzania, Mark Malekana, alitaka serikali kulichukulia suala hilo kwa uzito wa kipekee.

  Alisema licha ya kanisa hilo licha ya kupongeza kauli za viongozi wa madhehebu mengine ya dini na serikali za kukemea na kulaani viendo hivyo, lakini viongozi wa dini ya Kiislam nao wanapaswa kuwachukulia hatua za kinidhamu waumini wao wanaohatarisha amani .

  “ Lazima hawa viongozi wa dini ya Kiislam wawachukulie hatua hao waumini ambao wameanza kuharibu amani ama sivyo jamii itakuwa na picha isiyo sahihi,” alisema.

  Askofu huyo alisema matukio ya kushambulia na kuharibu majengo matakatifu ya ibada ya Kikristo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara na hata kusababisha wasiwasi kwa waumini wa dini hiyo, jambo ambalo likiachwa liendelee linaweza kuharibu amani nchini.

  “Kanisa halikufurahishwa kabisa na kitendo cha mtoto kudhalilisha kitabu kitukufu cha Kuran na nailipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua zilizochukuliwa za kumuweka kituoni mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi na kwa usalama,” alisema.

  Aliongeza: “Kitendo cha kukamatwa na polisi kinaonyesha jinsi dola isivyochukulia kirahisi mambo yayoweza kuvuruga amani miongoni mwa jamii. Kwa kweli kitendo cha mtoto huyo ni cha aibu.”

  Alisema kuwa bado kanisa lake linalaani vitendo vya watu wazima wenye kujua sheria za nchi, tena watu wa kiroho kuamua kuchukua hatua mkononi kwa kuvamia kituo cha polisi na kufanya uharibifu wa makanisa ambayo hata hayakuhusika na kitendo kilichofanywa na mtoto huyo.

  “Kwa kweli vitendo hivyo havikupaswa kabisa kutendwa na watu wanaomcha Mungu, kwani mcha Mungu ni mtu anayetegemewa kuwa muhimili wa amani katika jamii na kutokana na hali hiyo, ninawaomba pia viongozi wa dini ya Kiislam wawachukulie hatua za kinidhamu hawa waumini wao wanaohatarisha amani yetu ama sivyo jamii itakuwa na picha mbaya isiyo sahihi,” alifafanua Askofu Malekana.

  Askofu huyo alisema kuwa kanisa lake limefarijika kwa kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali akiwAmo Rais Kikwete; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki; Kamanda wa Polisi Kanda na Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam kwamba zinazooneshwa kukerwa na matendo hayo na kuwataka waamini wa dhehebu hilo na Watanzania kwa ujumla kuwa wavumilivu wakati serikali ikishughulikia suala hilo.

  Alisema Kanisa la Waadiventista Wasabato haliwezi kutafuta haki kwa kuvunja sheria, bali linapoona kuwa halitendewi inavyostahili, huitafuta haki kwa mujibu wa sheria.

  Katika vurugu zilizotokea Oktoba 12, Mbagala jijini Dar es Salaam, jumla ya makanisa saba yalichomwa moto na mengine kuharibiwa na kikundi cha watu wanaotumia kivuli cha dini ya Kiislam kufanya vurugu hizo.

  MBATIA: TUJADILI MUSTAKABALI

  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amemuomba Rais Jakaya Kikwete kuwakutanisha viongozi wa dini za Kikristo na Kiislam pamoja na wanasiasa ili kujadili namna ya kumaliza chuki inayozuka kati ya dini hizo mbili.

  Mbatia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mstakabali wa vurugu zilizojitokeza wiki iliyopita huko Mbagala, baada ya kwa waumini wa Kiislam kuchoma makanisa kufuatia kijana mmoja wa anayedaiwa kuwa Mkristo kukojolea Kuran.

  Mbatia alisema tukio hilo siyo jambo la kuchukulia kibusara eti kwamba lilisababishwa na watoto, bali kutafuta ufumbuzi wa chanzo cha matatizo hayo.

  “Vitendo hivi havijaibuka jana wala juzi, tumeshuhudia mara kadhaa makanisa yakichomwa hata Zanzibar tumeshuhudia, hivyo watoto nao wanajifunza kutoka kwa wakubwa kwamba chuki ipo kati ya pande hizo, tusisubiri itokee kama nchi za wenzetu kwa sababu nao walianza hivi hivi,” alisema.

  Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, aliongeza: “Tunaiomba serikali isifumbie macho jambo hili, bali ichukue jukumu la kuwakutanisha viongozi wa dini hizo pamoja na wanasiasa kuzungunguza kwa pamoja na kuangalia namna ya kumaliza chuki iliyopo hivi sasa.”

  Alisema ni jambo la kushangaza kuona viongozi wa dini na wanasiasa wamenyamaza na pasipo kusema jambo lolote kuhusiana na vurugu zinazojitokeza.

  “Ni jambo la kushangaza kuona kwamba hali inazidi kuwa tete, lakini wenye kuchukua maamuzi na kukemea wamekaa kimya, ni shetani gani ameingilia nchi hii au wana lao jambo?” alihoji.

  Aidha, alisema baadhi ya wanasiasa nao wamekuwa ni kichocheo cha kujenga matabaka ya udini na kwamba kitendo hicho kinatakiwa kukemewa mara moja.

  126 KORTINI LEO


  Watu 126 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Dar es Salaam kufuatia vurugu zilizotokea katika eneo la Mbagala Kizuiani wiki iliyopita ambazo zilisababisha kuchoma moto makanisa na kuharibu mali.

  Vurugu hizo zilisababishwa na kitendo mtoto wa miaka 14 kukojolea kurani.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema jana kuwa askari polisi waliendelea na msako ili kubaini wahalifu katika tukio hilo, hata hivyo, alisema kuwa walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine sita juzi.

  “Unajua jana asubuhi nilikuwa kwenye kikao kujadili suala hilo na kuamua kuwa muda wowote kuanzia leo (jana) watuhumiwa wote watakufikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria zitakamilika,” alisema Misime.

  Watu hao wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani imedaiwa kuwa ni waumini wa dini ya Kiislam, waliovamia makanisa manne na kuyakuchoma moto, kwa madai kuwa mtoto mwenye umri wa miaka 14 alikojolea kitabu cha Kurani tukufu.

  Kufuatia vurugu hizo, mali mbalimbali ziliharibiwa ikiwa ni pamoja vifaa vya kuendeshea ibada, vioo vya magari vilivunjwa, hasara kamili ya uharibifu huo haijafahamika.

  Rais Kikwete katika hotuba yake juzi ya kuzima mbio za Mwenge wa uhuru na Kumbukumbu ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliwataka viongozi wa dini hizo na waumini wao kuwa watulivu na wavumilivu wakati Jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi. Pia alisema wahusika wa vurugu hizo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  WAislam wa Mbagala type wanaenea nchi nzima
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Baba yake Ponda anaishi Kigoma

  MZEE Issa Ponda baba wa Katibu wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu Bwana Ponda Issa Ponda amewataka Waislamu kuungana katika yale yanayowaunganisha ili waweze kukabiliana na nguvu ya adui iliyowaelemea.


  Mzee Issa alitoa wito huo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake siku chache baada ya maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu yaliyofanyika kitaifa mkoani Kigoma.


  Mzee huyo maarufu Kigoma aliwakumbusha Waislamu kuwa silaha yao ni ucha Mungu kwa mujibu wa kitabu cha Allah na mafunzo sahihi ya Mtume (s.a.w.).


  Akizungumzia madai ya kusakwa kwa mwanawe na polisi mkoa wa Dar es Salaam, Mzee huyo wa Kibwari tapo maarufu la Kimanyema alisema watendaji wengi wa vyombo vya dola hawafahamu historia ya nchi hii matokeo yake wamekuwa wakifanya mambo kiupofu.


  Alisema wangelifahamu vyema Tanzania ya kabla ya uhuru (Tanganyika) wasingeshiriki kufanya haya wanayoyafanya.


  Aidha alisema anamuunga mkono mwanawe Ponda Issa Ponda kwa kuwa anatekeleza kile alichomfundisha.


  "Kama ningesikia amefanya ujambazi mahali ningekuwa wa kwanza kuisaidia polisi, lakini anasakwa kwa kuwa anahimiza haki na uadilifu, mimi niko pamoja naye 'Hattaa ataanal yaqiin' (mpaka idhihirike yakini)", aliongea kwa msisitizo Mzee Issa.


  Aliwaomba Waislamu wote nchini wapokee kama zawadi aya ya Qur'an isemayo:


  "Je, watu wanadhani wataachwa kwa kuwa wanasema "Tumeamini?" Basi ndio wasijaribiwe. Hapana, bila shaka tuliwatia katika taabu wale waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale walio wakweli na atawatambulisha (wale walio) waongo. Je, wanadhani wale wafanyao maovu kwamba watatushinda (tusiwapate kuwapatia adhabu?) Hukumu mbaya hiyo wanayohukumu". (29:2-4)

   
 4. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  .Ningeshangaa sana kama habari isingekuwa imeandikwa na Nipashe
   
 5. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Ivi nyie waislamu kwa nini hampendi amani??kwa nini mnataka kutuletea vita??...hii ni too much!!
  Yani nyie watu mnalazimisha tuwachukie bure.
   
 6. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  ulitaka nao waifiche??acha hadi watoto wenu wajue uovu wenu.
   
 7. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ni vigumu kufanya mambo ya ki taliban/boko haram/al shabab nchi ikiwa na amani tele...ndiyo maana wanaitafuta vita kwa nguvu zao zote...kwa sasa amani ya nchi hii inawategemea wakristo tu...!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee ndiye anayehusika na uchomaji wa Kanisa huko Kigoma
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  Offcourse ingeandikwa na annuur si mngeandamana kwenda bakwata
   
 10. spartacus

  spartacus JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mi nikishaona kiarabu nachukia kupita maelezo kozi nina hasira sana na waislamu.......hivo nikishakujumuisha nao, kinachofata hapo huwa out of my control.....yan bora uabudu mavi kuliko kuwa muislam
   
 11. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya makanisa mengine mnayachoma wenyewe baada ya kudhulumiana sadaka mnachoma ili kuficha kumbukumbu. lol
   
 12. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Tangu serikali ya Mwinyi mpaka sasa mmefumbia tatizo la kukashifu dini, mnadhani leo serikali itaweza? kila wakati Redio Imani inatoa matamko ya aibu, as if no body is responsible wakati vyombo vya dola vinatumia kodi tunazokamliwa kujilipa lakini wanashindwa kutimiza wajibu! Mie nayaona kama mazingaombwe ya Rais wetu.

  Tamko alilolitoa kwenye matukio ya makanisa nilidhani kuwa ni issue ndogo, nilivo ona zile picha, nikamshangaa Rais hajaona kuwa hii issue ni kubwa. Hivi wanajamvi hii ndo serikali inayoweza solve matatizo haya? ndo maana naona kama huu ni usanii wa serikali ku- solve tatizo.
   
 13. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Na kweli bila wakristo kuwepo wangesha uana wote kama somalia
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280

  Ndugu yangu kiarabu sio uislamu hata kidogo.........ni lugha tu na hata biblia ipo kwa kiarabu pia
   
 15. PROPHET POLY

  PROPHET POLY JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 469
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  This makes me believe that 'all' muslims except few have got big problems in their so called holy book or minds.either wrong teaching or wrong interpritation among the shekhs!!!all over world-muslims are problemes.i think the knowledge emberded is wrong.look at this example-china did not fight religious to wine its economy among big/small countries.be wise muslims to avoid wars unnecessarily.
   
Loading...