Kanisa limuondoe Baba Paroko wa Kitunda

Kanisa limuondoe Baba Paroko wa Kitunda

Mleta mada, hivi mbona kwenu mna asili ya majungu sana?
Kwanini umeleta huu umbea wako humu?
Si kuna baraza la walei hapo kwenu peleka maneno humo ebo!
 
Baba Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu Kitunda kwa nini anakuwa na kigugumizi cha kutangaza Jumuiya zilizohamishwa kutoka Parokia yake kwenda Parokia ya Kipunguni - Akwino.

Kwanini bado hatangazi ili hali taarifa anazo haoni kama waamini anawagawa!

Kanisa Katoliki linamsimamo lazima aheshimu maamuzi ya Askofu kugawa mipaka haiwezekani watu watembee km 4 kwenda kusali ili hali kuna Parokia ipo karibu hata km 1 haifiki.

Baba Askofu amuangalie sana huyu paroko amekaa hapo muda mrefu ametengeneza himaya yake. Kitu ambacho sio kizuri kwa Kanisa.

Haiwezekani tumehamishwa kwenda Parokia nyingine lakini viongozi wanadai michango ya Parokia nyingine ambayo tumeshahama hili ni tatizo na linaleta mgawanyo ndani ya Jumuiya.

Nawasilisha.
Tutamis Father Sabuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa sisi tufanyaje?

Ama unataka na hii Mama aingilie kati?
 
Mkuu; hebu tulia kidogo halafu utuambie vizuri. Je, Nani alizigawa hizo Jumuiya kutoka Parokia ya Roho Mtakatifu kwenda Parokia ya Kipunguni-Akwino?
Je, Baba Paroko wa Kipunguni amesemaje kuhusu hilo? i.e. Paroko wa Kipunguni ana taarifa rasmi juu ya jambo hilo? Mwisho labda nukuulize Je, Huduma za kiroho kwa sasa unazipata kutoka Parokia gani?
Kwa kifupi ni kwamba utaratibu unaelekeza kwamba kule unakopata Huduma ndiko Utoe Uwezeshaji wa hizo huduma i.e. Ndiko upeleke michango yako.
Kanisa halimlazimishi muumini kusali parokia fulani. Kinachotokea ni umbali wa parokia/kigango unafanya watu wasali parokia/kigango cha karibu. Lakini kama wewe unaweza kusali parokia au kigango kilicho maili 70 unakaribishwa kupata huduma za kiroho huko.
 
Back
Top Bottom