Kanisa limuondoe Baba Paroko wa Kitunda

Kanisa limuondoe Baba Paroko wa Kitunda

Baba paroko wa parokia ya roho mtakatifu Kitunda kwa nini anakuwa na kigugumizi cha kutangaza Jumuiya zilizohamishwa kutoka parokia Yake kwenda Parokia ya Kipunguni - Akwino.

Kwanini bado hatangazi ili hali taarifa anazo haoni kama waamini anawagawa.

Kanisa katoliki linamsimamo lazima aheshimu maamuzi ya Askofu kugawa mipaka haiwezekani watu watembee km 4 kwenda kusali ili hali kuna Parokia ipo karibu km haifiki.

Baba Askofu amuangalie sana Huyu paroko amekaa hapo muda mrefu ametengeneza himaya yake. Kitu ambacho sio kizuri kwa kanisa.

Haiwezekani tumehamishwa kwenda parokia nyingine lakini viongozi wanadai michango ya parokia nyingine ambayo tumeshahama hili ni tatizo na linaleta mgawanyo ndani ya Jumuiya.

Nawasilisha.
Ninavyo fahamu na ndivyo ilivyo, kila Parokia ina mipaka yake au tuseme Eneo lake kiutawala/kiutendaji. Paroko na wasaidizi wake wanatakiwa watoe huduma za kiroho ndani ya Eneo lao na si vinginevyo. Utoaji wa huduma una gharama zake ambazo Waumini wa Eneo hilo ndio wanatakiwa kuzichangia. Kusali ni mahali popote kwa raha zako; lakini ujue kwamba inapokuja ni suala la Huduma za Kiroho utakazohitaji zitatolewa na Parokia yako husika. Vinginevyo Huduma za kiroho unaweza kuzipata kutoka Parokia nyingine kwa kibali cha Maandishi kutoka Parokiani kwako. Hili lipo hivyo ili kuepusha migongano, migogoro, vurugu na hata uvunjifu wa Taratibu za Kikanisa hususan kwa wale Waumini au hata Maparoko wakorofi wasiozingatia Taratibu zilizowekwa na Kanisa Mahalia.
 
Mleta uzi,ungetumia platform nyingine kufikisha malalamiko yako lkn sio hapa.
Baba paroko tueleze platform nyingine ni ipi hiyo? Redio Maria?

Yani ukiona mtu anaandika kero za kanisa katoliki basi unatamani ummeze, mmezoea kuwageuza watu kondoo wala wasihoji lolote.
 
Baba paroko tueleze platform nyingine ni ipi hiyo? Redio Maria?

Yani ukiona mtu anaandika kero za kanisa katoliki basi unatamani ummeze, mmezoea kuwageuza watu kondoo wala wasihoji lolote.
Mimi sio Baba Paroko ila nachangia kwamba umefanya vyema kutoa dukuduku lako hapa ili kama anahudhuriaga humu aweze kujua kuna hoja au Baba Askofu yumo humu aweze kulifahamu hilo i.e. message sent and delivered kwa sababu mfumo wa Kanisa Katoliki uliopo hauruhusu Direct Communication kati ya Waumini na Askofu. Yaani kama unalalamikia kitu/jambo fulani Parokiani sharti jambo hilo lipitie kwa Paroko au Paroko awe na Taarifa nalo ndipo Askofu atalisikiliza au kuli-entertain. Ndo maana utakuta Maparoko wengine wanafanya watakavyo kwa sababu huendi/hufiki popote na hoja zako bila yeye kutamka.
 
Shida waumini wa siku izi mnanyima uhuru wa mababa sana shida mababa zetu wapole,wanahekima za kidini tunawakosea na si vizuri kuongea mambo ya dini uku
Aisee unawaamini hao jamaa. Hao ni watu na wanatenda dhambi kama sisi tuu. Wakikosea waambiwe ukweli
 
Baba Askofu amuangalie sana Huyu paroko amekaa hapo muda mrefu ametengeneza himaya yake. Kitu ambacho sio kizuri kwa kanisa.

Haiwezekani tumehamishwa kwenda parokia nyingine lakini viongozi wanadai michango ya parokia nyingine ambayo tumeshahama hili ni tatizo na linaleta mgawanyo ndani ya Jumuiya
Kumuanika hapa kiongozi huyu hujafanya uungwana hata kidogo,sijafurahishwa na uamuzi uliochukua inawezekana kwa namna moja au nyingine hamko sawa kuna pahala mlitofautiana ili kwakuwa hubanwi kusema chochote ,hii sio poa heshimu kanisa na waumini kwa ujumla bila shaka hayo ndio majibu sahihi kwako chekecha,tathmini,chukua hatua
 
Baba paroko tueleze platform nyingine ni ipi hiyo? Redio Maria?

Yani ukiona mtu anaandika kero za kanisa katoliki basi unatamani ummeze, mmezoea kuwageuza watu kondoo wala wasihoji lolote.
Wee Mzee Matola umenifuata na huku?, Mkristo mwenye BUSARA hawezi kuleta malalamiko yake kwenye mitandao ya kijamii Bali huko huko Kanisani kwake kuna ngazi nyingi anaweza akazitumia kufikisha malalamiko yake na kisha yakafanyiwa kazi kuliko kuleta hapa JF,ambapo hataweza kupata Suluhu zaidi ya kejeli,majungu na maneno yasiyofaa kutoka kwa watu ambao wapo Imani zingine au wenye uelewa duni.Ni sawasawa na mambo ya Kiofisi kuyaexpose kwa watu wasiohusika au Ishu za Kifamilia kuwaambia watu ambao hawahusiki unadhani utapata suluhisho la tatizo lako?.Kwa hakika huwezi.
 
Niambie ni mkatoliki yupi anaweza kuthubutu kumwambia Baba paroko hili siyo sawa? Aisee wewe umeandika kitu huku ukijuwa kabisa uhalisia wake ni jambo ambalo haliwezekani.

Wacha malalamiko yao mengi mitaani ndio njia sahihi yatawafikia tu, na uzuri Watawa Wakatoliki ni wasomi hivyo wanatembelea hizi platforms, kelele zikizidi watabadirika na kuondoa baadhi ya mambo ya kujinga ya kanisa la kisasa.
 
13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg

Waafriika tuna shida mahali
 
Back
Top Bottom