Kanisa katoliki wamwibia mjane

Kesho nitakuja na ushahidi mzima, nimelihusisha kanisa lote maana haya malalamiko kanisa katoliki Tanzania bara wanayo,hii kesi aridhi kilimanjaro na polisi wanaizungushwa sana danadana nyingi hiyo ni dalili tosha ya mazingira ya rushwa

Sasa kwa nini usingengoja hiyo kesho ukaja na kila kitu? Unatuhumu na ushahidi unauacha nyuma ili iweje? Hivi kweli kanisa katoliki ni taasisi dhaifu kiasi hicho? Watake kumdhulumu au kumnyanganya mjane tena eti kwa kuhonga polisi! Basi hiyo itakuwa sio kwa ajili ya kanisa/shule, labda hapo useme ni mtu binafsi anatumia kivuli cha kanisa. Na bado hii stori ikipatikana kutoka upande mwingine naamini haitakuwa na hii picha uliyoileta. Wewe pia wapaswa kuwa na hofu ya Mungu na uwe mkweli.
 

huyo mzungu alilipataje hilo eneo? embu tuanzie hapa....na kama hujui, je unajua sheria zikoje kuhusu wageni (foreigners) kumiliki ardhi?, naamini kama unayafahamu hayo yote, basi naamini usingeandika hayo maelezo hapo juu.

na kama huna majibu ya maswali hapo juu, huo uhakika wa huyo mzungu kumiliki ardhi umeutoa wapi?, je kwa sababu wewe ni mkazi wa hayo maeneo?, au kwa sababu ulikuwepo wakati huyo mzungu ananunua hilo eneo?,

na zaidi ya yote, je kuna vielelezo vyovyote vya kuthibitisha uhalali wa huyo mzungu kumiliki ardhi?. kama upo basi wekeni vivuli vyake hapa
 

Wew kinachokukereketa hapa ni ujane tu Wa Huyo mama na ndo umepigwa upofu hapo wala hutaki kypapasa kwingine ukajua kunanini!!we adi unahoji kama kanisa katoriki kuna aliesoma!!ivi mzima wewe???Huyo mleta umbea mwenyew alisema ataleta ushahidi kesho ila adi Leo kapotea.jaribu kuchangamsha akili yako sawasaw na uspende kuhukumu mambo kwa kuegemea upande mmoja
 
Ndg wanajamvi nasikitika sikuweza kuwa hapa kwa muda kdg haswa ukizingatia kama mtoa mada nilitakiwa niyajibu maswali yenj na pia kufafanua baadhi ya mambo. Nilikua namuuguza mama yangu mpendwa. Baada ya kusoma jinsi wengi wenu mliochangia ni kwamba kuna mnaodai lile eneo ni la kanisa, la hasha si la kanisa, lile eneo alimilikishwa Dr Balletto tena kisheria na hata ukienda pale ardhi wilayani ukaomba ramani utaona tu, na jirani yake ndo lilikua eneo la shule ya marangu. Ieleweke kwamba shule ile haikua mali ya kanisa katoliki hadi miaka ya 80 ilipokabidhiwa kwa jimbo katoliki la moshi, kwahiyo kanisa lilikua halina ardhi yyte pale, na baada ya kukabidhiwa shule kanisa ndo lilianza kufatilia ardhi ya jirani yani kwa mjane kama nilivyoeleza kwenye mada. Nimesoma alivyoandika mdau ngaiwoye anaesema kua ni jirani yake anavyoeleza ni sawa, nimesoma alivyoandika mdau chaga king ni kweli huyo dr Baleto kuna wkt alikua kule maua, na huskii familia yake ikiongelea maswala ya maua sababu ilibaki chini ya maua sem, mmeongelea juu ya lease na tittledeed nazan kuna waliofafanua hapo, ila napenda ieleweke document alizo nazo yule mama zinatambulika ofisi ya ardhi wilaya na ktk ramani hilo ya wilaya ilioyopo ofisi za ardhi shamba hilo lipo na linaonekana kwa jina la marehem na si kanisa wala shule. Kuna wengine wamedai kufahamu hiyo shamba na historia yake kua lilikua ni la kanisa, nawasihi waache uzushi na kubuni, ni lini kanisa lilimiliki pale wakati shule yenyewe ilikua si yao?? Kuna wengine wamemkashif mama mjane wakati hawamjui wala hawajui historia ila wameamua tu kutetea kanisa, mi mwenyewe ni mkatoliki toka kuzaliwa hadi uzee huu, sina sababu ya kulisingizia kanisa ila kwa hili kanisa ama watendaji wake hawako sawa. Kuna waliohoji uraiya wa mama mjane nazani ni ndg msingida, mama huyu ni raiya wa tanzania mzaliwa wa marangu na mwanae pia ni mtanzania maana alizaliwa hapa. Kuna mwingine alihoji kwanini raiya wa nje anamiliki shamba hapa, kuna watanzania kibao wana nyumba ughaibuni pia wana mashamba nchi za watu sioni tatizo kwa marehem kwani mkewe alikua mtanzania kabisa. Nawalongeza wale wote walioonyesha moyo wa huruma kwa mjane, MUNGU awabariki sana. Hivi sasa taarifa ambazo nimezipata ni kua mama mjane na mwanae wamefata mkondo wa sheria na hivi sasa wameshafungua shauri katika mahakama ya ardhi moshi na tayari kanisa na shule wameshapewa zuio la kuendeleza ujenzi pale huku kesi ikiendelea katika mahakama hiyo ingawa matisho ya mwalimu mkuu kwa mjane yanaendelea. Kwa maana hiyo basi nitashindwa kuweka ushahidi hapa kama nilivyoahidi kwa kua nitakua naingilia kazi za mahakama na uhuru wake. Wale wanaosema wanakaa pale ama wanapajua pale mfano benteke, ngaiwoye na wengine watakua sasa wameona barua za zuio zilivyobandikwa pale. Wasalaam mimi Bigjahman mpenda haki na muumini halali wa kanisa katoliki la roma
 
...sasa mbona ulilileta huku kabla ya baraza la ardhi kufanya haki yake, ila ujue ukiona shule imerudishwa mikononi mwa kanisa ama taass nyingine, ujue mwanzo ilikuwa chini ya taasisi hiyo then ikataifishwa. Anyways, nitatafuta namna ya kulipata hilo shauri.
 

Ivi unajua maana ya kumilikishwa adhi??na he kwa sheria ya MWAKA gani inayoruhusu RAIA Wa kigeni kumilikishwa ardhi!???ebu tupunguzie umbea wako na ichonganishi,,kaendelee kumuuguza mama sio utuletee stress zako hapa.kumbe kazi unayo ya kumuuguza mama bado unataka kazi ingine ya umbea na ichpnganishi!!
 
Mleta thread kakurupuka sana, heading yako ni ya kuchonganisha kanisa na waumini na kulifanya kanisa kuwa kichaka cha uwizi.Nadhani una chuki binafsi na kanisa.Akili yako haina akili.Ebu tuondolee upuuzi wako hapa
 
WagoWago mbona huyu kajieleza vizuri tu.kinahokuuma kwene maelezo yake ni nini?Ebu ni saidie na mimi hapa sheria ya mwaka gani ilianza kuzuia raia wa nje kumiliki ardhi mpaka kufikia mwaka 1993?na je?kama raia mgeni alishakuwa na ardhi kabla ya hiyo sheria, huwa inakuwaje kisheria?Chaga King umeoyesha busara sana.nadhani huyu mtu asitupiwe maneno yasiyofaa tena.kuna walioshauri kuwa huyo Mjane aende baraza la ardhi,kafanya ivo.wanaotaka kumsaidia wafanye ivo.
 
Hahaha
 
Mama asikubali aende mahakamani
 
Umenikumbusha wizi wa ardhi kanisa katoliki walichofanya pale ubungo emaus. Wakafanya mpango wa kuback date tarehe ili wahalalishe kumbomolea mtu nyumba yake kisa tu alikataa kuwauzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…