Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,215
- 10,283
Mwezi Novemba mwaka jana Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa kikatoliki Marekani ulitoa tamko kulani sera za serikali ya Trump za kuwatimua na kuwapakazia wahamiaji waliokuwepo Marekani. Hii ilikuwa muendelezo wa hotuba ya Pope Leo XIV ya mwezi Januari mwaka jana kwa mabalozi waliokuwa wakiwakilisha nchi zao katika Holy See ambapo aliyalaani mataifa yanayotumia ubabe kukandamiza mataifa mengine.
Jana makadinali watatu wa Marekani ( wa Chicago Washington na Newark) wameisema serikali ya Marekani kuhusu matumizi ya nguvu za kijeshi Venezuela tishio la kuipora Greenland na makato ya misaada nchi za nje ambayo yana hatari ya kuongeza mateso badala ya amani.
Kwa hali hii kumshitaki Father Kitima Vatican ni kupoteza muda maana anaendeleza msimamo wa Papa wa kupinga ukandamizaji na uonevu pale anapoona au kuhisi unafanyika. Kama hawajafurahia mwenendo wa Father Kitima basi wamtake pia Pope Leo asijiingize kwenye siasa na ajikite kwenye kuhubiri Neno Takatifu.
Amandla...