kwanini wanampa nafasi?,au wanaogopa atawatumbua nini?tatizo siyo kanisa..tatizo ni yule anaepewa nafasi kusalimia waamini ndo hajielewi nahisi mnamjua mdomo wake usivokuwa na mipaka
kwanini wanampa nafasi?,au wanaogopa atawatumbua nini?
We umualikamgeni kwako utamzuiakuonga?naunga mkono hoja
kualikukana kilasiku jamani?We umualikamgeni kwako utamzuiakuonga?
yangefanyikaa msikitinii washauriwaa watu zamani mabomu yangesharushwaa kumbuka mwembechai magomeni libumbaa kilichomkutaa akawakimbiaa wakaendaa kumvunja mikono mbagalaManeno yako sawia maana haya yangefanyika misikitini ingekuwa kelele sana ni vyema nyumba za ibada zikawekwa mbali na siasa
Acha uongo nanii..!!Unataka nchi iharibike mara ngapi! Viongozi wa dini ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Ni wasabato pekee ndio hawaruhusu ujinga huo makanisani kwao kwa sababu hawategemei misaada ya serikali na wanasiasa kuendesha mambo yao
Mkuu umenena vyema, kwanza mi nilijuavyo hili kanisa hata hiyo nafasi ya mtu kusalimia kanisani pia ni geni. Ndani ya kanisa ni ibada tu, nimekulia ukatoliki naujua vyema.Habari wanabodi..
Awali ya yote ninaomba niwapongeze wale wote ambao wamefanikiwa kuuona mwaka mpya wa 2017.
Pili nawapa pole wale wote ambao wameanza mwaka kwa matatizo mbalimbali. Ninaamini MUNGU atawapa Faraja.
NAOMBA NIJIKITE KWENYE MADA.
Labda nianze kueleza taratibu za Kanisa Katoliki katika ibada zake.
Kanisa Katoliki lina sehemu kuu mbili za katika Ibada;
1. Liturjia ya Neno
2. Liturjia ya Ekaristi
Sehemu hizo zote mbili hazimruhusu mtu kusema neno lolote lililo nje ya utaratibu wa Kikanisa. Hata wakati wa matangazo hutakiwi kutangaza jambo ambalo Kiongozi Mkuu (Paroko au Askofu) halifahamu.
Pia Kanisa halina utaratibu wa kuruhusu mambo ya SIASA ndani ya Kanisa bali hutoa msimamo usiofungamana na upande wowote ili kutoadhiri msimamo wa Waumini. Japo linaruhusu KUKOSOA na KUPONGEZA PIA.
WAPI KANISA LINATAKA KUTUHARIBIA NCHI?
1. Kuruhusu hotuba za Kisiasa ndani ya Kanisa. Hili nionavyo mimi litaharibu Nchi. Wanasiasa wanayo majukwaa yao ya kuzungumzia mambo yao ya siasa na siyo Kanisani. Siku za hivi karibuni Kanisa Katoliki limekuwa likiwaruhusu wanasiasa kusimama Madhabauni na kutoa hutoba zao za Kiserikali na Kisiasa ama kwa kujibu hoja fulani au kutoa matamko ama kusambaza Kauli Mbiu fulani, (tafsiri yangu ya haraka hapa ni kwamba wanasiasa wanahitaji "mass support" hata kama wanafanya jambo baya). Kwa hili Kanisa halitendi haki maana viongozi wa Nchi hii ni wetu sote. Kama viongozi wetu wanahitaji kujibu hoja, kutoa matamko au kusambaza kauli mbio wasitumie NYUMBA ZA IBADA.
KANISA KATOLIKI WAPENI WATU NAFASI KANISANI YA KUSALIMIA TU NA KUSISITIJA JUU YA AMANI, UPENDO, MSHIKAMANO NA UWAJIBIKAJI NA SIYO VINGINEVYO.
2. Matamko ya viongozi wa Kanisa Katoliki. Hawa viongozi ni lazima wajikite kwenye ukweli na siyo kujipendekeza. Nyakati hizi viongozi wa Kanisa Katoliki wamekuwa ni watu wa kupongeza tu bila kukosoa ukilinganisha na nyakati za nyuma.
a. Mmepongeza yale mazuri = VEMA.
b. Kwa nini hamkosoi na kusema ukweli juu ya mambo ambayo Serikali inakosea au hata kuhoji tu?. Mfano sijasikia mkikosoa au kuhoji juu ya,
i. Ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchi.
ii. Matumizi ya fedha za wahanga wa Kagera.
iii. Nyongeza ya mishahara ambayo ni haki ya mfanyakazi.
iv. nk
KANISA KATOLIKI MKIENDELEA HIVI MTATUHARIBIA NCHI YETU.
Nawasilisha.
Hapana, hujamuelewa mtoa mada. Kanisani kwa wakatoliki ni mahali patakatifu hakuna mazungumzo mengine nje ya ibada. Mazungumzo pekee yaliyo nje ya mfumo wa kiibada ni tafsiri ya masomo, anaitoa padri, na matangazo tu. Nje ya hayo, mengine yote hunenwa sawa dunia nzima.Sioni kama kanisa linashida, utaratibu wake ni ule ule!
Shida ipo kwa hawa wanasiasa, mfano huyu Bwana yule amekuwa mtu wa kutopangiwa kitu cha kuongea, hata akiambiwa hapa hupaswi kusema hivi yeye ng'o atalipuka tu na yale anayoyataka yeye ili apate sifa...
Wanasiasa ndio wenye matatizo!!
Acha uongo nanii..!!
Promo onlyUnataka nchi iharibike mara ngapi! Viongozi wa dini ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Ni wasabato pekee ndio hawaruhusu ujinga huo makanisani kwao kwa sababu hawategemei misaada ya serikali na wanasiasa kuendesha mambo yao
Mtoa mada nimemuelewa vyema, pengine wewe ndiye hukunielewa tafsiri yako imekwenda op kwa jinsi nilivyoquote huyo mdau...Hapana, hujamuelewa mtoa mada. Kanisani kwa wakatoliki ni mahali patakatifu hakuna mazungumzo mengine nje ya ibada. Mazungumzo pekee yaliyo nje ya mfumo wa kiibada ni tafsiri ya masomo, anaitoa padri, na matangazo tu. Nje ya hayo, mengine yote hunenwa sawa dunia nzima.
Nje ya wasomaji wa masomo, padri na mtangaza matangazo. Mimbari ya kanisa hakuna apaswaye kunena jambo hapo.
ni wale-wale tu coz huyo Pengo hakukemea alibariki ziitwe sadaka.Ni kilaini au pengo?