Kanisa Katoliki mnataka kutuharibia nchi?

b191

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
742
1,031
Habari wanabodi..

Awali ya yote ninaomba niwapongeze wale wote ambao wamefanikiwa kuuona mwaka mpya wa 2017.

Pili nawapa pole wale wote ambao wameanza mwaka kwa matatizo mbalimbali. Ninaamini MUNGU atawapa Faraja.

NAOMBA NIJIKITE KWENYE MADA.

Labda nianze kueleza taratibu za Kanisa Katoliki katika ibada zake.

Kanisa Katoliki lina sehemu kuu mbili za katika Ibada;
1. Liturjia ya Neno
2. Liturjia ya Ekaristi

Sehemu hizo zote mbili hazimruhusu mtu kusema neno lolote lililo nje ya utaratibu wa Kikanisa. Hata wakati wa matangazo hutakiwi kutangaza jambo ambalo Kiongozi Mkuu (Paroko au Askofu) halifahamu.

Pia Kanisa halina utaratibu wa kuruhusu mambo ya SIASA ndani ya Kanisa bali hutoa msimamo usiofungamana na upande wowote ili kutoadhiri msimamo wa Waumini. Japo linaruhusu KUKOSOA na KUPONGEZA PIA.

WAPI KANISA LINATAKA KUTUHARIBIA NCHI?

1. Kuruhusu hotuba za Kisiasa ndani ya Kanisa. Hili nionavyo mimi litaharibu Nchi. Wanasiasa wanayo majukwaa yao ya kuzungumzia mambo yao ya siasa na siyo Kanisani. Siku za hivi karibuni Kanisa Katoliki limekuwa likiwaruhusu wanasiasa kusimama Madhabauni na kutoa hutoba zao za Kiserikali na Kisiasa ama kwa kujibu hoja fulani au kutoa matamko ama kusambaza Kauli Mbiu fulani, (tafsiri yangu ya haraka hapa ni kwamba wanasiasa wanahitaji "mass support" hata kama wanafanya jambo baya). Kwa hili Kanisa halitendi haki maana viongozi wa Nchi hii ni wetu sote. Kama viongozi wetu wanahitaji kujibu hoja, kutoa matamko au kusambaza kauli mbio wasitumie NYUMBA ZA IBADA.

KANISA KATOLIKI WAPENI WATU NAFASI KANISANI YA KUSALIMIA TU NA KUSISITIJA JUU YA AMANI, UPENDO, MSHIKAMANO NA UWAJIBIKAJI NA SIYO VINGINEVYO.

2. Matamko ya viongozi wa Kanisa Katoliki. Hawa viongozi ni lazima wajikite kwenye ukweli na siyo kujipendekeza. Nyakati hizi viongozi wa Kanisa Katoliki wamekuwa ni watu wa kupongeza tu bila kukosoa ukilinganisha na nyakati za nyuma.

a. Mmepongeza yale mazuri = VEMA.

b. Kwa nini hamkosoi na kusema ukweli juu ya mambo ambayo Serikali inakosea au hata kuhoji tu?. Mfano sijasikia mkikosoa au kuhoji juu ya,
i. Ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchi.

ii. Matumizi ya fedha za wahanga wa Kagera.

iii. Nyongeza ya mishahara ambayo ni haki ya mfanyakazi.

iv. nk

KANISA KATOLIKI MKIENDELEA HIVI MTATUHARIBIA NCHI YETU.

Nawasilisha.
 
Tukiweka pembeni udini kuna ka ukweli ndani yake. Katoliki ya halisi mkiingia kanisani wote ni sawa mambo ya salamu zilizo nje ya Ibada Takatifu mnapeana nje ya kanisa. Na ndani ya kanisa utaratibu uliendelea bila kuingiliwa na mtu, bosi ni mwendesha Ibada tu. Naunga mkono hoja, Katoliki turudishieni utaratibu wetu, mambo ambayo yako nje ya Ibada yafanyike nje ya Kanisa.
 
Unataka nchi iharibike mara ngapi! Viongozi wa dini ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Ni wasabato pekee ndio hawaruhusu ujinga huo makanisani kwao kwa sababu hawategemei misaada ya serikali na wanasiasa kuendesha mambo yao


Mkuu;
Weye kweli wa maana sana. Kumbe hawategemei misaada ya serekali na wanasiasa kendeshea mambo yao?? Sawa mzee, ila, sio kwamba hawana tumbo bali ni kwa vile kijiko chao kipo kwenye sahani yenye chakula. Sio hivyo, nadhani usingelikuwa hapo kwenye key board ukitwanga hizo herufi. Hakuna anayeichukia fweza. Wakipewa huwa hawapigi kelele ka wanasiasa.
 
Back
Top Bottom