Kanisa Katoliki kuadhimisha miaka 150 ya kuingia Tz Bara ni dhahiri ukatoliki bado ni mchanga Tz

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Kanisa Katoliki Tanzania Bara litaadhimisha Miaka 150 tangu Ukristo Ukatoliki uingie Tanzania bara kupitia Mji mkongwe wa Bagamoyo,na pia wataashimisha miaka 100 toka Kanisa Katoliki la Tanzania Bara kupata Padre wa Kwanza Mzalendo(Mtanzania)

Mapadre hawa walitoka katika Maeneo ya kanda ya Ziwa ambapo ni Geita,Bunda na Bukoba na wote walisoma na kulelewa ktk Seminary Ndogo ya Rubya iliyoko Jimbo La Bukoba.Hii ni kusema kuwa Bukoba ndio inajenga Historia ya Uinjilishaji wa kiroho ktk kanisa katoliki,kwanza kwa kuwa na Mapadre wa kwanza wazalendo na pia kwa kuwa na Cardinal wa Kwanza Mwafrika na kutoka Africa Muadhama Rugambwa.

Adhimisho hili linapa picha kuwa,kumbe Ukristo Ukatoliki Tanzania Bara hauna zaidi ya miaka 150...Ukilinganisha na Uislamu.Na maswali ya kujiuliza ni kuwa kwanini Ukristo ulichelewa sana kufika Afrika na Tanzania kaa ujumla na kuacha Uislam uliofika karibu miaka 500 na zaidi nyuma?

Mwaka 2012 Shirika la Roho Mtalatifu(Holy Ghost Fathers) barani Afrika,walikutana Bagamoyo Tanzania...mahali ambapo ulikuwa "mlango" wao wa kuingilia Afrika...Na hiki ndicho walichoandika

.
Maadhimisho ya Mkutano mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu katika Mji Mkongwe wa Bagamoyo ni tukio la kihistoria, linalotupania nafasi ya kukumbuka kwa mara nyingine tena, historia ya mchakato wa Uinjilishaji Afrika Mashariki. Katika makala zilizotangulia, Mheshimiwa Padre Philipo Massawe amebainisha vigezo na masharti yaliyopelekea hata Shirika la Roho Mtakatifu likaamua kuadhimisha Mkutano wake mkuu Bagamoyo kwa mwaka 2012.
Ametumegea kwa kina changamoto na vuguvugu la Uinjilishaji Zanzibar na Tanganyika kwa wakati ule. Leo anatuvusha mabonde na milima hadi nchini Kenya. Itakumbukwa kwamba, Bagamoyo ni chimbuko la Ukristo Afrika Mashariki.

Wamisionari hawa hawakubaki tu Tanganyika, bali pia waliingia Kenya. Kati ya mwaka 1889-1899 walianza Mombasa na sehemua za Pwani Malindi, na baadaye walikwenda Bura, Taita, Mto Tana, Machakos na mwishowe wakafika Nairobi. Hoja tunayojenga hapa siyo kuandika historia, ila ni kuonyesha sifa mojawapo inayofanya Mkutano Mkuu wa Shirika pawe ni sehemu ambayo kuna alama muhimu au makini. Kwa hii historia fupi, Bagamoyo imekuja kuwa ni Mama wa Makanisa Katoliki siyo tu kwa Tanzania bali kwa Afrika ya Mashariki.

Uamuzi wa kufanya Mkutano Mkuu wa Shirika Bagamoyo kunatupa nafasi ya kipekee kabisa kuwaenzi kwa heshima kubwa wale wamisionari wa kwanza wa Shirika. Katika utamaduni wetu wa Kiafrika hii ina maana kubwa sana kwetu. Tunasema tunaleta Shirika lote pale mahali ambapo Kanisa la Afrika ya Mashariki na ya Kati lilipozaliwa. Kitendo hiki kina maana kwamba kwamwe hatutawasahau hawa waanzilishi kwani kufanya hivyo ni kinyume na utamaduni wetu, na ukristu wetu. Tunaungama kwenye Kanuni ya Imani kwamba tunaamini katika ushirika wa watakatifu.

Kwetu sisi wanashirika na kwa wakristu wa sehemu hii ya Afrika, hawa ni mababu zetu ambao walitoa maisha yao kwa ajili ya bara letu na hasa sehemu hii ya Afrika, walijitosa kwa moyo mmoja na kwa nguvu zao zote. Kikubwa kwao kilikuwa ni HUDUMA, KUJITOLEA kabisa bila ya kujibakiza hata chembe (total dedication), kwa kuwa walisukumwa na upendo wa Kristo, aliyekufa kwa ajili yetu wote pale Msalabani.

Wao walitoa maisha yao wakifuata mfano wa Yesu mwenyewe. Maisha yao ni mfano wa imani isiyotikisika kama Yesu anavyotueleza kwenye Injili kwamba imani inaweza kusukuma milima. Imani na matumaini yao kwa Mungu haina mpaka. Walitii ile amri ya Yesu: “Enendeni duniani kote mkawafanye mataifa yote kuwa wafuasi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi (Mt 28:
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
19).

Katika utume wao wakimisionari walikuwa na ari kama ile ya Mtakatifu Paulo ambaye tumaini lake lilikuwa “ili watu wa Mataifa wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, iliyotakaswa na Roho Mtakatifu (Warumi 15:16). Tunaenda Bagamoyo kukumbuka utume wao, mateso yao, kujitoleo kwao, walikufa wakiwa vijana wadogo kabisa katika ubichi wao, na jinsi walivyotoa maisha yao kwa ajili ya kutangaza Habari Njema ya Kristo Afrika ya Mashariki.

Kama Biblia inavyotuasa, “Wakumbukeni viongozi wenu wale waliowaambia Neno la Mungu. Angalieni mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.” (Waebrania 13:7). Hakuna njia iliyobora zaidi kwetu sisi isipokuwa kufuata mfano wa maisha yao ya kujitoa na kujitolea kwa watu katika utume hasa wale walio maskini na katika utumwa wa aina mbali mbali, kuiga mfano wa imani yao na kuwa na moyo wa kimisionari na wa kijasiri.

Kanda ya Tanzania inasema karibuni sana Bagamoyo mwaka wa 2012 kusheherekea kwa pamoja Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Shirika la Roho Mtakatifu utakaofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, bara ambalo ni kipenzi cha mwanzilishi wa Shirika letu Padre Fransisko Maria Pauli Libernmann. Huyu ambaye tunamwita mwanzilishi wetu wa pili wa Shirika alisema, “Moyo wangu upo Afrika, Moyo wangu upo na waafrika"


Ndi kusema,ni kweli kuwa Ukristo ilikuwa ni njia ya kueneza ukoloni na ndio maana ulikuja Tanzania Bara mara tu baada ya Makoloni kugawanywa?
 
Ukristu upo Africa kwa zaidi ya miaka elfu 2. Labda useme Misri sio Africa au Ethiopia sio Africa. Nchi ya Ethiopia na Eritrea ambako kote bado Wakristu ni wengi kuliko wafuasi wa dini zingine ni nchi zilizopokea Ukristu na kuifanya dini hiyo kuwa dini ya taifa mapema kuliko nchi kama Uingereza.

Ni kweli Ukristu ulichelewa kuja Tanzania lakini sio Africa.
 
Mbona hao ma padri woote ni mapadri wa kwanza tanzania wakati wapo wengi?
 
Ukristu upo Africa kwa zaidi ya miaka elfu 2. Labda useme Misri sio Africa au Ethiopia sio Africa. Nchi ya Ethiopia na Eritrea ambako kote bado Wakristu ni wengi kuliko wafuasi wa dini zingine ni nchi zilizopokea Ukristu na kuifanya dini hiyo kuwa dini ya taifa mapema kuliko nchi kama Uingereza.

Ni kweli Ukristu ulichelewa kuja Tanzania lakini sio Africa.
Kuna tafauti baina ya ukristo ulioingia Absynia(ethiopia) miaka hyo alfu kadhaa iliyopita na ukatoliki,mleta uzi amezungumzia ukatoliki kichelewa kuingia tanzania na sio ukristo in general.Yakupasa ufahamu kuwa kulikuwapo ukristo kabla ya kuja dhehebu la katoliki.
 
barafu huu uzi utafufuka mwezi ujao (Agosti 2017) kwenye kilele cha maadhimisho

Pia nawatakia wakatoli wote maadhimisho mema ya miaka 100 toka apatikane Padri wa kwanza Mzalendo
 
Hivi hizi dini zilikua na misimamo gani juu ya utumwa uliokuwa unaendelea kipindi hicho?

Sent from my HUAWEI LUA-L21 using JamiiForums mobile app
 
barafu huu uzi utafufuka mwezi ujao (Agosti 2017) kwenye kilele cha maadhimisho

Pia nawatakia wakatoli wote maadhimisho mema ya miaka 100 toka apatikane Padri wa kwanza Mzalendo

Ndio mwezi wa nane huo sasa, kilele ni lini?
 
Kuna tafauti baina ya ukristo ulioingia Absynia(ethiopia) miaka hyo alfu kadhaa iliyopita na ukatoliki,mleta uzi amezungumzia ukatoliki kichelewa kuingia tanzania na sio ukristo in general.Yakupasa ufahamu kuwa kulikuwapo ukristo kabla ya kuja dhehebu la katoliki.
Ilikuwa mwaka gani mkuu!
 
Wareno walimaliza kuijenga Fort Jesus ya Mombasa mwaka 1596. Wareno walikuwa ni wakatoliki. Sijui kama walijenga kanisa miaka hiyo.

In 1885, British Church Missionary Society (wa anglikana na waprotestanti wengine), walifungua kituo cha kidini Kilimanjaro.
The Holy Ghost Fathers from Alsace (wakatoliki) and Lutheran evangelists from Leipzig walisha fungua vituo vyao vya kidini huko Kilimanjaro in the 1890s.

Nahisi wakatoliki walifungua kituo cha kidini huko Peramiho in the late 1890s.

Ukatoliki ulikuwepo kule North Africa wakati watu weusi wana ishi huko (kabla ya waarabu kuja North Africa).

St Augustine alikuwa ni mwafrika mweusi mkatoliki (asili yake ni Algeria ya leo).

Wakristo wasiokubaliana na Ukatoliki walikuwepo pia huko North Africa miaka hiyo.

St Luke, ambae pia ni Lucius of Cyrene (alie ambatana mara kwa mara na Mtume Paulo, kwenye safari mbali mbali za ki injili), ambae pia ni mwandishi wa kitabu cha injili ya Luka na kitabu cha Matendo ya Mitume, naye alikua mwafrika mweusi kutoka huko Cyrene (leo hii ni Libya).

Wenyeji wa kale wa Cyrene ni uzao wa Phut mwana wa Ham mwana wa Noah.

Around 1/3 – 1/2 ya wabantu wa leo (including asilimia kubwa ya Wachagga) ni uzao wa huyu Phut.
 
barafu huu uzi utafufuka mwezi ujao (Agosti 2017) kwenye kilele cha maadhimisho

Pia nawatakia wakatoli wote maadhimisho mema ya miaka 100 toka apatikane Padri wa kwanza Mzalendo
Kweli kabisa, na vitenge tumenunua
 
Adhimisho hili linapa picha kuwa,kumbe Ukristo Ukatoliki Tanzania Bara hauna zaidi ya miaka 150...Ukilinganisha na Uislamu.
Naona dalili za ligi ya kijinga. Hao waliotangulia, walileta kitu gani tunachoweza kujivunia zaidi ya upuuzi? Heri hawa walileta shule, hospitali na ustaarabu
 
Back
Top Bottom