KANGI LUGOLA kutolewa kafara!

KANGI LUGOLA kutolewa kafara!

Kangi Lugola ni Mwana CCM ambaye anatimiza vema wajibu wake wa kuisimamia serikali iwajibike kwa wananchi. Hongera sana Lugola. Hizi propaganda za Jambo Leo zisikukatishe tamaa

Security ya ID humu JF haipo kabisa siku hizi,
ona sasa ID ya mtu imeingiliwa hapa mwenye nayo sijui yuko wapi?
 
Criminals na Schizophrenic ndiyo siku zote hujipitisha, lazimisha na kung'ang'ania siasa ili kuongoza serikali.
Watu wenye akili timamu ni mpaka wasukumwe sana ndipo hujitumbukiza kuwa viongozi serikalini.

All politicians are criminals and schizophrenic until proved otherwise
 
Lakini kiukweli Lugola alifaa kuwa chadema.Hicho chama cha magamba wana kolimba sijui kama unalijua hilo!
 
Jambo leo! Anyway hakuna atakayeishi milele, wala kukatisha maisha ya mtu siyo suluhu ya tatizo lililopo.
 
Askali Polisi aliye disco education? Nchni ya ajabu sana hii.
 
Angekuwa chadema akasema uozo wa chama chake angeitwa msaliti, mhaini, mamluki na mengine kibao kwa sbb cdm huruhusiwi kukosoa. Safi CCM kwa kuweka demokrasia ili watu wakosoe utendaji wa chama chenu

Mi nafikiri kumkosoa kiongozi wa serikali, haimaanishi wakati wote kukikosoa chama. Angewaponda Team Kinana; ndio ungejua maana ya demokrasia ndani ya chama.
 
Ulikuwa wapi mhe waziri mkuu? Utaponea wapi Kagasheki? Ulisema umenyang'anywa majukumu..we ni waziri wa namna gani..? Utaponea wapi? Utaponea wapi waziri wa mambo ya ndani! I like this guy

I agree with you. The guy is more than good but unfortunately is on the wrong side. Si ajabu zikasukwa njama za kumnyamazisha. Wapiga kura wake wanapashwa kuwa na fahari kwa kuchagua mbunge kifaa kama huyu.

Tiba
 
jembe lugola karibu chadema ,magamba wamchukue zitto wao.
Kama ni usajili, kama vifanyavyo vilabu vikubwa vya mpira wa mguu, kubadilishana huko CDM wakubali kumtoa ZZK bure na wao wawe tayari kumlipia dau lolote Kangi Lugora, ili atue kwenye timu ya ushindi ya CDM, ili aongeze nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, akisaidiana na akina Tundu Lissu, Godbless Lema,Mchungaji Msigwa, John Mnyika, Ezekiel Wenje na Sugu.

Kwa kikosi hicho kikali, magamba wanaweza kulala kwa magoli mengi, kama vile kwenye mtani jembe, jinsi Yanga alivyobugizwa na Simba, goli 3 kwa kagoli kao kamoja ka kufutia machozi!!
 
Mh Mbunge Kangi Lugola,ambae amekuwa mwiba mkali kwa Mawaziri huenda akatolewa kafara baada ya kutumiwa massege za kutishiwa kuuawa huku yeye akisema kuwa hataenda kutoa ripoti Polisi.Hii ni baada ya mh Kangi Lugola kuwa miongoni mwa Wabunge waliotamka wazi bila kificho ndani ya Bunge kuwa mh Waziri Mkuu ni mzigo na anaetakiwa kujiuzulu.Wiki mbili zilizopita wakati Wabunge wakijadili ripoti ya tume ya bunge iliyowasilishwa na mwenyekiti wake Mh James Lembeli, mh Kangi Lugola alimshambulia Waziri mkuu akimtuhumu kuwa Wamempa,Ndege,Helkopita na Magari ya Vingora lakini wakati Watanzania wanauawa yeye alikua amejikalia tu Ofisini. "ulikuwa wapi Mh Waziri mkuu" tumekupa magari na vingora,tumekupa Ndege,tumekupa na hata Helkopta?Kwa habari zaidi soma gazeti la Jambo leo!
ime kafara iwe ni nini Lugola ni jembe pamoja na kuwa yuko ccm
 
Yeye mwenyewe ni polisi akaripoti polisi kufanya nini??? sema ukweli na hutishwi
 
Kangi Lugola ni Mwana CCM ambaye anatimiza vema wajibu wake wa kuisimamia serikali iwajibike kwa wananchi. Hongera sana Lugola. Hizi propaganda za Jambo Leo zisikukatishe tamaa

Mh! Siamini macho yangu,nilijua lazima utamponda ,kangi lugola anasema ukweli hakika.
 
Kumpa mtu crediti kwa sababu tu ana ujasiri wa kumsema raisi, waziri mkuu au mawaziri....sidhani kama ni kumtendea haki yeye na wanainchi.

Hichohicho ndicho wanachofanya hata wapinzani kila siku.

Nadhani tupime zaidi utendaji wa muhusika...na kama unavutiwa na utendaji wa mbunge, waziri au kiongozi fulani mtendee haki yeye na sisi wanainchi kwa kutupa wasifu wake kiutendaji na sio CV...

Kwa mfano mngetuambia jamaa alipokuwa security airport alidhibiti magendo kwa kiwango kadhaa tofauti na waliomtangulia au waliopo sasa, au jimbo lake limepiga hatua moja mbili tatu kutokana na utendaji wake, na hamasa kwa wanainchi wake.

No wonder " wahubiri" wamekuwa wafanyabiashara wakubwa wa imani na wamekuwa mabilionea kutokana na waTZ kuwa waumini wazuri wa kuamishwa kwa ufundi tu wa kuongea.
 
Back
Top Bottom