KANGI LUGOLA kutolewa kafara!

KANGI LUGOLA kutolewa kafara!

Imekuwa bahati mbaya kwangu kwani naamini CCM kuna mizigo mingi, tofauti yao ni sura,vitengo na mavazi kama si majimbo wanayotoka
 
Hakuna pinda lazima ang'oke nyie maccm mtaua wangapi???
 
Mh Mbunge Kangi Lugola,ambae amekuwa mwiba mkali kwa Mawaziri huenda akatolewa kafara baada ya kutumiwa massege za kutishiwa kuuawa huku yeye akisema kuwa hataenda kutoa ripoti Polisi.
Hii ni baada ya mh Kangi Lugola kuwa miongoni mwa Wabunge waliotamka wazi bila kificho ndani ya Bunge kuwa mh Waziri Mkuu ni mzigo na anaetakiwa kujiuzulu.

Wiki mbili zilizopita wakati Wabunge wakijadili ripoti ya tume ya bunge iliyowasilishwa na mwenyekiti wake Mh James Lembeli, mh Kangi Lugola alimshambulia Waziri mkuu akimtuhumu kuwa Wamempa,Ndege,Helkopita na Magari ya Vingora lakini wakati Watanzania wanauawa yeye alikua amejikalia tu Ofisini. "ulikuwa wapi Mh Waziri mkuu" tumekupa magari na vingora,tumekupa Ndege,tumekupa na hata Helkopta?

Kwa habari zaidi soma gazeti la Jambo leo!

Kangi Lugola ni Mbunge wa Mwibara ambaye ni tishio kwa uhai wa CCM. Huyu jamaa yuko makini na haogopi kitu.
Nampa Big up sana huyu jamaa pamoja na kwamba yuko Chama Cha Mafisadi CCM. Nasikia huyu jamaa ni jangu mstahafu kwa maana ingine anajua sana habari za Intelijensia. Ili Polisi waweze kumzushia Kesi za kubambika wanatakiwa wafanye kazi ya ziada!

Hata hivo ningependa kumpa ushauri wa Bure kabisa kwake kwamba,Mhe. Kangi Lugola unatakiwa kuhamia Upinzani mara moja kabla hawajakutoa kafara.

Karibu sana CHADEMA ili uendeleze mapambano.
 
Ulikuwa wapi mhe waziri mkuu? Utaponea wapi Kagasheki? Ulisema umenyang'anywa majukumu..we ni waziri wa namna gani..? Utaponea wapi? Utaponea wapi waziri wa mambo ya ndani! I like this guy
Mhe.Kangi Lugola ni katika wabunde wachache wa ccm wenye mtizamo wa kimasilahi ya taifa kuliko chama chao.Mimi binafsi sishangai na naamini kuwa hata yeye kwa kupanga kuyasema hayo aliyoyasema hatashangaa kupokea vitisho kama ilivyo kawaida ya siasa zetu za Kiswahili ambapo mtu badala ya kuangalia hoja zinazoongelewa kama zina ukweli huwa wanamtizama mtu na maisha yake.Je kama hawataisemea CCM akina lugola nani aisemee?.Kimsingi kwa hoja anazozitoa Bungeni hata kama siipendi ccm lakini kwa Lugola huwa naanza kufikiri kumbe hata CCM bado kuna wafia nchi.Polisi wenyewe ukienda kutoa taarifa kama hiyo ya kutishiwa kwa sababu ni wavivu wa kufikiri wanataka wewe ndiye umtaje aliye kuandikia halafu wanaenda kumwambia kuwa tumeambiwa na mlalamikaji kuwa wewe ndiye uliyeandika badala ya kufanya kazi yao ya uchunguzi kitaalamu. Hivyo hata mimi kama ningekuwa nafasi yake ningenyamaza tu nione kitakacho tokea kwani mimi naamini mwenye kukutendea baya akidhamiria hahitaji kukutisha kwanza.Lakini naamini Mhe.Lugola alishamfahamu kwani hata yeye alishawahi kuifanya kazi ya upolisi kama R C O.ambayo ni nafasi kubwa kipolosi.
 
Mh Kangi Lugola ni Nyoka wa Shaba wanao mtafuta kwa mabaya wakimkaribia hakika hawatapona.
 
Lugola anasema kweli. Sema tu huwa anashinikizwa na kundi lake la Team Lowasa kuongea kwa jazba

Kumbe CCM napo kuna makundi??? 2015 is near the corner let's wait and see manake Lowassa want to lead the country, membe the same, Kanda ya ziwa tumewasikia wameanza mchakato!! This country is heading highway to the grave!!
 
Mh Mbunge Kangi Lugola,ambae amekuwa mwiba mkali kwa Mawaziri huenda akatolewa kafara baada ya kutumiwa massege za kutishiwa kuuawa huku yeye akisema kuwa hataenda kutoa ripoti Polisi.
Hii ni baada ya mh Kangi Lugola kuwa miongoni mwa Wabunge waliotamka wazi bila kificho ndani ya Bunge kuwa mh Waziri Mkuu ni mzigo na anaetakiwa kujiuzulu.

Wiki mbili zilizopita wakati Wabunge wakijadili ripoti ya tume ya bunge iliyowasilishwa na mwenyekiti wake Mh James Lembeli, mh Kangi Lugola alimshambulia Waziri mkuu akimtuhumu kuwa Wamempa,Ndege,Helkopita na Magari ya Vingora lakini wakati Watanzania wanauawa yeye alikua amejikalia tu Ofisini. "ulikuwa wapi Mh Waziri mkuu" tumekupa magari na vingora,tumekupa Ndege,tumekupa na hata Helkopta?

Kwa habari zaidi soma gazeti la Jambo leo!

Kangi Lugola na Deo Filikunjombe ni backbenchers wa CCM period
 
Kumbe CCM napo kuna makundi??? 2015 is near the corner let's wait and see manake Lowassa want to lead the country, membe the same, Kanda ya ziwa tumewasikia wameanza mchakato!! This country is heading highway to the grave!!

measkron,

Hapo kwenye nyekundu hapo. You're very right. The country is leading straight away to its own grave!!!
Ni dhahiri nchi hii hapa tulipofikia imeshapoteza mwelekeo kwa kukosa UONGOZI BORA na SIASA SAFI kama alivowahi kusema Baba wa Taifa hili Mwl.J.K. Nyerere(RIP).

Unashangaa kuona kwamba kwa sasa kuna mnyukano wa chichini wa watu kutaka kwenda Ikulu na ilhali hawana SIFA hata kidogo za kukaa Jumba hilo takatifu!! Mtu kama Edward Lowasa,Bernad Membe, Emmanuel Nchimbi(aliyetimuliwa Uwaziri juzi),Januari Makamba, Rose Migiro na wengineo hawana sifa kabisa za kukalia kiti cha Ikulu!!!

Lakini kwa vile nchi hii inaendeshwa na Mafisadi ndiyo maana watu wanakimbilia Ikulu ili wakaendelee kufanya Ufisadi wao kwa uhakika zaidi, bila woga wala hofu! Hivi kweli itakuwaje Rais akiwa mtu kama Lowassa( Mzee wa Richmond)?Mtu aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu kwa tuhuma za Ufisadi leo anaomba arudi Ikulu, akafanye nini? Kama u-PM ulimshinda ataweza kuvaa viatu vya Urais kweli??? No way!

Mtu kama Nchimbi hana sifa hata moja. Hapo tu kwenye Uwaziri amechemka halafu ati mtu ana ndoto za kuingia Ikulu?? Labda Ikulu ya Mafisadi na Walevi wa Madaraka! Njoo kwa Bwana mdogo Januari Makamba, sijui anapata wapi ushawoshi huu wa kutka kuingia Ikulu, bila shaka ni kwa baba yake Mzee Yusufu Makamba, kwa mtindo uleule wa wa Usultani. Kwamba kwa vile baba alikuwa Kiongozi mkuu wa CCM basi hiyo ni tiketi ya kwenda Ikulu!!! Nonsense!

Hivi Makamba Januari anafikiri kuwa Rais ni sawa na kuwa Mbunge? Kwamba unapigiwa kura unapata ushindi wa kishindo halafu unaenda kwenye mjengo wa Bunge halafu unaishia KULALA usingizi na KUUNGA HOJA KWA 100% hata kama hoja yenyewe ni uharo???Nafikiri Makamba hajui maana ya kuwa Rais wa nchi! Tunajua alikuwa mwandishi wa Hotuba za Rais Kiwete sasa anafikiri kwa mtaji huo anaweza kuwa Rais.....hakika ni kichekesho!!

Acha tusuburi hiyo 2015 nani ataingia Ikulu kama CCM watafanikiwa kuihujumu CHADEMA kwa mara nyingine. Time gonna tell.
 
Kangi Lugola ni Mwana CCM ambaye anatimiza vema wajibu wake wa kuisimamia serikali iwajibike kwa wananchi. Hongera sana Lugola. Hizi propaganda za Jambo Leo zisikukatishe tamaa

leo umeona kama gazeti la jambo leo linaandika propaganda???? Lkn gazeti hilo hilo lingeandika propaganda juu ya CDM ungesema ni kweli. Msiwe wanafiki kama rangi za kinyonga.
 
Kangi Lugola ni Mwana CCM ambaye anatimiza vema wajibu wake wa kuisimamia serikali iwajibike kwa wananchi. Hongera sana Lugola. Hizi propaganda za Jambo Leo zisikukatishe tamaa

Apewe kifimbo cha uwaziri na hasa wa maliasili uone kama atapona na huo ujuaji wake.
 
Kumbe hili jamaa limesoma!!!!!! Nilifikiri elimu yake sawa na ya mbunge wangu Profesa Maji Marefu....JK mpe Wizara ya mambo ya ndani huyu mtu.
 
Mh Lugola anaipenda Tsnzania na siyo chama. Viongozi na hasa wanasiasa inatakiwa muipende nchi na siyo vyama vyenu.mpenda chama kamwe hawezi kuleta maendeleo ya nchi.
 
Mh Lugola anaipenda Tsnzania na siyo chama. Viongozi na hasa wanasiasa inatakiwa muipende nchi na siyo vyama vyenu.mpenda chama kamwe hawezi kuleta maendeleo ya nchi.
 
Inspector hatishiwi nyau, atadeal nao mwenyewe kama kweli katumiwa hizo msg
tunapenda wabunge wakweli kama Kangi,
wengineo ni wale wa NDIOOOOOOOOO......huyu nampa bigup
 
Back
Top Bottom