Niliambiwa kwamba Kanda ya ziwa wanafanya sherehe na mikesha wakishangiliwa bahati nasibu aliyoipata Magufuli wakati wakubwa wanagombania maslahi.
Inanipa shida kuelewa hawa ndugu zangu kama pamoja na ongezeko la upashanaji habari ambao ulikuwa unatosha kuwapa taarifa nyingi na sahihi juu ya matukio ya watendaji na mifumo ya uongozi nchini.
Watanzania wakiwemo kanda ya ziwa, wamkuwa katika dimbwi la kilio kikuu kwa miaka mingi wakilia mateso, manyanyasho. rushwa, maisha magumu, kukosa huduma, vifo vya kulazimishiwa, uonevu, kuminywa kwa haki, kudharirishwa wanapohhitaji huduma kama vile tanesco, n.k, halafu wanaambiwa hayo mateso ni uongozi mbovu na mfumo wa utawala usiofaa, wanaelekezwa na njia sahihi.
Wanaposhindwa kuamka na kupita katika njia sahihi, wanadanganyika na shilling 5,000/= ili auze kadi yake ya kupigia kura, anaalikwa kula pilau kwenye sherehe za mafisadi, anapewa khanga na mara nyingine kupiga picha ame pause na mafisadi, tayari anasahau kwamba hao mafirauni wamempa dhiki maisha yake yote, anaendelea kukenua meno na kuyashangilia, anadiriki hata kushinda mtandaoni akiyapepelea, ni zaidi ya wendawazimu. Watafiti fanyeni kufuatilia ili mje muone Tanzania ina vichaa wangapi kwa kutumia kura zitakazopigwa kuiunga mkono ccm!.
Ukiona mtu anaunga mkono mgombea kwa sababu ni kabila lake au wanatoka kanda moja, huyo mtu ni zaidi ya marehmu asiye na fahamu. Kabila linakusaidiaje wewe kutatua matatizo ambayo umekuwa ukilia lia nayo?
Kabila la mgombea litafufua viwanda, kutengeneza ajira na kupandisha kiwango chako cha elimu ili usome, upate sifa za kufanya kazi bora na uajiriwe?
Kuwa kabila moja au kutoka kanda moja na mgombea, kunapunguzaje mfumuko wa bei na kuongeza nguvu ya shilingi ili uweze kumudu maisha kwa kipato chako?
Kuwa kabila moja au kutoka eneo moja na mgombea, kunaongezaje upatikanaji na ubora wa kiwango cha huduma katika ofisi za umma ili ukihitaji huduma za umeme, afya, elimu, masoko, ushauri wa kitaalamu, maji, polisi na usalama, mahakama, upate huduma za kiwango sahihi kwa muda sahihi na gharama halisi???
Kuwa kabila moja na kutoka kanda moja na mgombea, kunaondoaje rushwa na unyanyasaji wa raia?
Huyo mgombea atatembeza migao ya madakitari, polisi, mahakimu, walimu, shule namitaala yake, masoko ya bidhaa, ajira na kila hitaji bora kwa watu wa kabila lake au wa kandaanayotoka ambao hawatakuwa wakifanya kwa viwango tofauti na wale wa kwingine??
Unapoangalia kabila ama ukanda, ukitegemea favoritism, na nepotism, ni kweli huyo mgombea wenu atawaweza kuwabeba kabila lake na kanda yake yote bado Tanzania ibaki kuwa taifa moja? Kama mgombea wenu anasifa hizo, na ninyi mnashabikia kwa sabbu mnategemea upendeleo, je bado anasifa za kuliongoza taifa??
Na kwa kuwa mnamfahamu vizuri basi bila shaka taifa lione kwamba mgombea huyo ni bingwa wa ubaguzi na upendeleo kwamba nje ya watu wa kwao, wengine wategemee makombo yatakayosalia, kitu ambacho sikubaliani nacho.
Ninaomba Watanzania tusiendelee kuumizwa na mitazamo ya udini, ukabila, ukanda. Tuchague kiongozi mwenye sifa sahihi, uwezo wa kiwango na awe katika mfumo utakaomsaidia ama kumsukuma kutenda mema na haki kwa Watanzania. Kinyume cha paleni patapotea na tutatakiwa tuhesabiwe ni wafu zaidi ya marehemu. Kama tunajihesabu tuko hai, tuangalie madonda yetu anayovuja damu bado ambayo JK ametusababishia kwa favoritism na nepotism ambazo amekuwa akizifanya wazi wazi, maksudi bila haya wala hisia.
Kumchagua Magufuli kwa sababu ya kutoka naye kanda moja ama kabila moja, haikuondoeli dhiki zako kwa sababu hata kama angetamani lakini uwezo huo hana. Magufuli ni mwana cccm kama walivyo wana ccm wengine.
Hata kama Magufuli mnamwona ni mwema kama malaika wa nuru, lakini kumbukeni hataweza kuwatatutuli shida zenu nyumba kwa nyumba na hivyo mtasherehekea na kuendelea na mateso yenu na watoto wenu.
Magufuli hata atakapokuwa raisi, hatakuwa na uhuru wala uwezo wa kufanya lolote alitakalo kama CCM haijaridhia. Kumbuka amesema yeye atafuata Ccm kwanza, mengine baadaye. Ccm ndiyo iliyowaumiza na imewekeza kwenye mateso yenu milele. Fungukeni macho.
Magufuli kama Magufuli hana uwezo wa kuumba watu wa kufanya nao kazi. Ni lazima aunde srikali kwa kuwa na mawaziri hao hao mafisadi wwenye kiapo cha kulinda ufirauni kwa gharama yoyote kwa kuwa ni wanufaika. Hayo madabiliko anayfanya kwa kutumia watu gani? Kiapo chake ni KULINDA MASLAHI YA CCM KWANZA.
Ccm hao hao ambao mmewaona wakifisadi fedha zenu kwa mikataba fake, wizi mbali mbali na kisha kuteteana na kulindana ndiyo watakaokuwa wakimpa mwongozo wa namna gani afanye.
Hao hao waliokataa maoni ya Watanzania kwenye katiba na kuichakachua hadharani, ndio hayo hayo atatakiwa afanye kazi nao kwa maslahi ya ccm taifa baadaye.
Magufuli huyo ni mtii na mfuatiliaji wa kuhakikisha maagizo anayoagizwa anayatimiza kwa gharama yoyote. Itakuwaje pale atakaposimama na fimbo ya chuma, hataki mijadala wala kuhojiwa juu ya kuhakikisha anatekeleza sera za "Udini wa Cccm?, Migawanyo na matabaka kwa Watanzania,? Ulinzi wa mafisadi? Kuchakachua ellimu ili na kundi fulani ambalo halikuwa na elimu waonekane wengi wamesoma? Kulindana na kuhakikisha mikataba fake iliyokwisha kusainiwa na HIZI SHERIA MUMIANI ZA JUZI ZINATEKELEZWA BILA N AFASI YA KUFANYIWA REVIEW WALA KUHOJIWA?
Magufuli hawezi kusaliti itikadi za chama chake, na hilo ndilo kalisema. Labda niwaulize maswali:-
Nil siku gani Magufuli alisimama bungeni kama mbunge akajitenga na maamuzi ya hovyo yaonevu wa raia na kukumbutia maslahi ya mafisadi?
Magufurli akiwa Mbunge, alikuwa upande gani wkati wa kuchakachua rasimu ya katiba ya Warioba?
Juzi wakati miswada ya wizi inapitishwa, magufuli alisimama upande gani kuonyesha anajali taifa zaidi ya ccm?
Mnaoshangilishwa, naomba kila mmoja afumbe macho, awakumbuke ndugu zake waliopoteza maisha kwa sababu ya umasikini na kukosa huduma bora za afya kwa sababu ya ccm, wakumbuke wagonjwa wanaoishi kwa mitishamba na wale wanaosubiri kufa kwa sababu hawawezi kwenda india kutibiwa? Wakumbuke Wazazi wako wanaoishi katika umaskini kwa sababu wamejitoka kukusomesha kwa gharama kubwa halafu umemaliza shule huna ajira na huzuni mnayoipata wewe na wazazi wako.
wafikirie yatima wanaoishi mitaani, wanavyoongezeka kila siku kwa kuachwa na wazazi wao bila mpango wowote wa kuwapatia elimu ili waishi kama watoto wengine. Watoto wako wewe utakapokufa ghafula , serikali ya cc itawasaidia licha ya kodi kubwa unayolipa leo?
Fikiria wakulima wanavyohangaika na kilimo duni, wanashinda juani, nguo zimechanika, wamekuwa weusi ajili ya jua, macho yamekuwa mekundu, hawana hata ufahamu wala hawajui kuna kupumzika, wanalima kwa nnguvu na gharama kubwa, halafu wanapovuna hakuna soko la uhakika la bidhaa zao. Wanaletewa watu wa kuwakopa kwa bei iliyochini zaidi ya gharama walizotumia. Michango inaongezeka mara mlinzi wa shule, mara ujenzi wa nini mara nini, wakishindwa wanakamatwa, wanapigwa, wanafungiwa ofisini, wengine wanahamia porini ili wajiepushe na mateso kwa sababu hakuna anayeweza kujali na kuelewa shida zao. Wengine wameliwa na wanyama na kpoteza maisha katika kukimbia huko.
Wakumbuke Watanzania wanaopoteza haki zao kwa uonevu na kushamiri kwa rushwa. Wakienda polisi hawana rushwa wanaishia kubambikizwa kesi na wengine wameawa mikononi mwa polisi na serikali ya cccm imenyamaza kimya kuonyesha hizo ndizo sera zake.
Mfikirie alilyekwenda mahakamani huku haki zake zikiwa peupe lakini akaishia kutiwa hatiani kwa mfumo mbovu na upindishaji wa sheria. kumbuka familia za watu wamskini wasiokuwa na matumaini waliofukuzwa maeneo ya migodo wakamilikishwa wageni. Wanauawa kila siku na serikali ya ccm inasimama upande wa wageni na kuwaacha waTanzania maskini wakiishi kama wanyama katika ardhi ya nchi yao.
Yako mengi ya kusema., lakini kwa haya machache, naomba mtafakari na kisha muamuae kuendelea kusherehekea kuchaguliwa kwa Magufuli ili mradi ni mtu wa kwenu, huku mkijua mnashangilia mateso ya ndugu zenu na vizazi vyenu? Au mtaamua maamuzi sahihi ya kujiokoa ninyi, ndugu zenu na taifa zima kutoka katika mitego ya ibilisi ccm ambaye huja kama kondoo lakini ni mbwa mwitu mkali.
Mkifika hapa, najua hamtahadaika na kabila wala ukanda. Ccm na watu wake ni wale wale, na kuwashangilia nikushangilia mateso ya mauti zetu, ndugu zetu na watoto wetu.
Mwenye sikio na alisikie neno hili ambalo Tabby awaambia Kanda ya ziwa na Watanzania wote!.