Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Mtani usiteseke sana.... Kwa huko nje ya nchi wanajua tu Tanzania kuna Wachaga na Wamasai.... Tunawabeba hata nchi kama nchi.

Ukifika Finland au Ufaransa ukisema umetoka Tanzania utaulizwa Mchaga? Hamna mtu anamjua Mfipa au Myao au sijui Mnyantunzu au Mbarbeig huko Ulaya.

Sijataja Waha maana wataanza ubishi hapa
Hahaha absolutely true
 
'Chasaka' sijaelewa maana yake boss.
Chasaka maana yake ni mtu wa Porini yaani mtu wa kuja hata kama umetokea Dar umeenda Uru huko.

Kwahiyo wanaweza kukuita Chasaka au Mpori.

Bukoba wanaitwa Wanyamahanga yaani mtu wa kuja.
 
Huwezi kuwa proud kwa kuwa huna sifa za kuwa mchaga. Kuzaliwa Moshi au kama mama yako aliolewa Moshi akiwa ameshakuzaa na mwanaume mwingine hakuna namna unaweza kuwa Mchaga... Wewe ni Chasaka..
SEMA umeongea kibaguzi sana wew mnyama-anga wa kichaga.[emoji23]
Sisi wahaya watu wa makabila mengine tunawaita WANYAMA-ANGA..
So utajisiaje nikikuita hivyo
 
Ni wabaguzi hawakuwafanyi kuwa special mfano wewe unatabia za kibaguzi hakukufanyi kuwa special, ubaguzi ni ujinga ndo maana kila Mahalia unapigwa vita mfano uko kwenye mikoa mingine mngekua mnatreatiwa vibaya kama mnavyotreat watu ambao sio wachaga Ila wamezaliwa na kukulia Moshi unafikiri ingekuaje na hii ndo sababu Nyerere aliwadis ni wabinafsi sana yule Babu aliona mbali sana kuhusu wachaga na hakukosea
Kusema kweli mimi ni mbaguzi sana hasa linapokuja suala la mtu mvivu na mpumbavu asiyejituma na mtu mwenye wivu kama wewe.
Hebu sema hapa hadharani wachaga huwa wanabagua watu kwenye masuala gani? Hawa dada zako walioolewa Moshi wanabaguliwa? Au ulitaka na wewe uolewe ili uone umetendewa sawa?
 
SEMA umeongea kibaguzi sana wew mnyama-anga wa kichaga.[emoji23]
Sisi wahaya watu wa makabila mengine tunawaita WANYAMA-ANGA..
So utajisiaje nikikuita hivyo
Kwa hiyo nyie kuita wengine hivyo sio ubaguzi bali wachaga ndio wabaguzi?
Sisi wachaga mnatuita majina mengi ya kibaguzi kama ulilotaja, mara mnatuita wezi, dada zetu mnasema wanaua waume zao ila huwezi sikia tunalialia kuwa mnatubagua. Tunaelewa ni namna gani mko na insecurity hivyo tunaendelea na maisha hadi mnaanza kutuiga.
 
Ishu ni kwamba hata hao kina Mvungi, Msuya, Sabuni, Minja, Mjema, Mnzava na wengine huona fahari sana kutambuliwa kama Wachaga. Wachaga ndio wamefanya kukaonekana kuko "blessed"
Mwambie awaulize hao kina Minja au msuya wanapokwenda kwao wanasema kwanini wanakwenda moshi badala ya kusema mwanga au same anakwenda
 
Boss unachosema ni kwamba kanda ya kaskazini ni maarufu sababu ya wachaga?

Serengeti, manyara, tarangire, milima ya upareni, mbulumbulu, masai mara, ngorongoro, mapango ya tanga n.k ni maarufu sababu ya uwepo wa wachaga? Kama ndicho ulichomaanisha ww ni mpotoshaji.
Wengi wanapakataa kwao
 
Kusema kweli mimi ni mbaguzi sana hasa linapokuja suala la mtu mvivu na mpumbavu asiyejituma na mtu mwenye wivu kama wewe.
Hebu sema hapa hadharani wachaga huwa wanabagua watu kwenye masuala gani? Hawa dada zako walioolewa Moshi wanabaguliwa? Au ulitaka na wewe uolewe ili uone umetendewa sawa?
Hivi unanijua mpaka unaniita mvivu, nilishakuomba msaada ili kuprove mim ni mvivu jibu ni hapana unijui

unajua umeonyesha ujinga wa kiwango Cha juu sana ndo maana nakuambia Tena wewe ni mjinga
 
Tatizo lao wachaga wana kiherehere sana kwa kila kitu na kupenda sifa za kuchonga kibwege kuumbe hamna kitu! jambo hili limewapa umaarufu sana... ..fikiria mchaga anaiba Mbuzi anamweka kwa gunia ili akauze supu mnadani....yule Mbuzi akilia Meeeheee!!

Mchaga anaanza!! '''Yelewi Meku!! acha iso bana aa! ...umelewa mbege!! sasa umeamua ku naria km mbusi eee??.... ntakuacha, babaanguuu! usiniretee maringo!! eee!! oraka msuru na Mao!! endee nyamazo mbh!raaa!aaaaa!!

Sarakasi zimewafanya wawe maarufu!!! sasa fikiria kitendo cha demu wa kichaga kukuwekea hapo ushughulikie!! Nyapu yake then yeye ana soma gazeti kabisaa!! anakwambia ''ukimarisa msee wangu niwekee pesa angu apo eee!!..kabla hujaondoka!!eee!!

km mie muongo tongoza mchaga wa kishmundu uone hawajui kukata viuno......utacheka hadi uyambe kifukuto!
 
Mwambie awaulize hao kina Minja au msuya wanapokwenda kwao wanasema kwanini wanakwenda moshi badala ya kusema mwanga au same anakwenda
Moshi Kuna makabila mengi ambao wamezaliwa na wazazi wao Wana mashamba, Kuna wapare, wasambaa wanyaturu, wamasai wengi tu wamezaliwa na kukulia Moshi na wazazi wao wanaishi Moshi mtu kama huyo akenda Moshi unataka aseme anaenda wapi

Ukienda Moshi rural kule tambarare tpc, kahe, mabogini, rundugai, chekereni ni nadra sana kukuta wachaga sababu wachaga wengi wako miliman kama kibosho, marangu, machame,n.k mtu akisema anaenda Moshi unataka aseme anaenda wapi ujinga ni kufiri Moshi wanakaa tu wachaga
 
Kwanza ujue kuna 1. Kabila kubwa 2. Kabila Maarufu na 3. Kabila linaloheshimika.

Ukienda kanda ya ziwa utakuta Wasukuma ndio kabila maarufu na pia kabila kubwa. Ila kwa kanda hiyo kabila linaloheshimika ninaweza kusema ni Wahaya.

Kwa kanda ya Kaskazini Kabila maarufu ni Wamasai, Kabila kubwa (kwa idadi ya watu) ni Wairaq na Kabila linaloheshimika ni Wachaga.

(JAPO WACHAGA SIO KABILA)
Wachaga wanaheshimika kwa kuwa ndio Jamii ambayo iko "organized" kuliko jamii ingine yeyote Tanzania.

Umeuliza kwa nini inaonekana "WACHAGA" wanaibeba kaskazini?

Jibu rahisi tu ni kuwa kwa upende wa Kaskazini ni maeneo wanayoishi "WACHAGA" peke yake ambayo yalikuwa na maendeleo ya hali ya juu hususani sehemu za vijijini. Kwa leo hii ukiambiwa kuwa Hospitali ya KCMC iko ndani ya Wilaya ya Moshi Vijijini tena Tarafa ya URU utakataa kwa nguvu zako zote.

Karibia kama siyo theluthi ya shule zote za sekondari za Tanzania zinapatikana Kilimanjaro maeneo wanayoishi Wachaga. Ni nadra sana kutembea zaidi ya Km 5 bila kukuta Shule ya sekondari kwa maeneo haya.

Hali ni tofauti kwa maeneo ya upareni.... Utakuta shule kwa wastani wa kila baada ya km 15 hadi 20 kwa maeneo ya kijijini na kwa mjini walau km 7 mpaka 10. Kama mtu anajua umbali wa Shule ya sekondari Vunta mpaka ya Kirangare atasema nasema ukweli.

Maeneo wanayoishi wachaga yana taasisi kubwa hata vijijini na sehemu kubwa imefanywa kwa juhudi za wananchi wenyewe. Kuna mahospitali makubwa yaliyoanzishwa zamani sana kama vile Kibosho Hospital, Kibong'oto (maarufu kwa kifua kikuu), Machame Hospital.... Adhani ina miaka kama 110 au zaidi.... Hospitali ya Kilema... Ilianzishwa miaka ya mwishoni mwa karne ya 19 (1890s)..,Hospitali ya Marangu.... Hospitali ya Huruma iliyopo Rombo.

Sitaongelea barabara za lami zinazoelekea Sanya Juu, Masama, Machame, Kibosho Umbwe, Mbokomu, Kibosho Mweka, Kibosho Kirima, marangu hadi Kilema (kwa sasa inazunguka mpaka kwa Lazari)... Kwenda Kirua Vunjo kupitia Kongo, barabara ya kupandisha Uchira, Old Moshi hadi ilipokuwa shule ya Kolila zamani, marangu mtoni hadi marangu gate, rombo kupitia Mwika.... Naona nikiendelea nitawaabisha tu watani.

Unaachaje kubebwa na mtu mwenye Chuo kikuu cha KCMC, MWENGE, SIMUKO, Chuo cha Wanyamapori Mweka (Tanzania vipo 2 tu na hiki ndio kilikuwa pekee kwa Afrika mpaka miaka ya 2000) Marangu TTC, Mandaka TTC, Singachini TTC, vyuo vya uuguzi KCMC, Machame, Kibosho nk.

Naona niache kutaja shule kama Umbwe, Lyamungo, Kibosho Girls, Machame Girls, Weruweru, St. JAMES' seminary (1925), Uru seminary.... Maua Seminary au basi Ashira Girls... Wengine wakati wanakazana kupokea mahari WACHAGA walikuwa wakijenga shule kwa ajili ya watoto wao wa kike... Unaachaje kusema wanabeba Kaskazini?

Turudi kwenye maendeleo binafsi... Wewe binafsi kama kweli hauna chuki na wachaga utakubali kuwa ndio Jamii pekee kwa TANZANIA NZIMA na sio Kaskazini tu ambapo hauwezi kukuta nyumba ambayo haijaezekwa kwa bati yata kama ni kule kibosho "Ntudu" au Mahoma - Old Moshi.

Pia ndio sehemu ambayo watu hawajisaidii machakani au kwenye choo cha shule kama wapare.... Utakuwa shahidi yangu kama unamjua mchaga kuwa hata kama anaishi sehemu ya mbali na Kilimanjaro utamjua kwa haraka bila kuambiwa kwa kuona nyumba yake tu kwani itakuwa tofauti na ya wenyeji... (standing out). Na "mchaga" asipokuwepo sehemu basi jua wazi hiyo sehemu hakuna maendeleo. Wengi ni "ULTIMATE OPPORTUNISTS".

Kwa mumalizia jibu hili fupi hebu niambie kama huko Kaskazini ni Wapare (Wasu), Wairaq au Wamasai wapi huwa wana"flock" kurudi nybani kwa likizo (VACATION) kama wazungu wengine wafanyavyo kipindi cha majira ya joto?

Sio wapare huwa wanajifanya kuwa na wao ni kina Mangi wanafuata Wachaga kurudi Moshi na wanaishia Hedaru kisha wanarejea maana hawajajenga kwao?

Tuanze na majibu haya kwanza.
Umemaliza kaka👏
 
Back
Top Bottom