Kanali Lubangu: Usiposhangilia Liverpool FC kuchukua ubingwa wa EPL 2019-2020 unaweza kushitakiwa kwa utovu wa nidhamu

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,334
17,835
Kanali mstaafu wa jeshi la mashabiki wa soka duniani anasema mashabiki wote wa mpira wa miguu duniani wasiposhangilia pamoja na shabiki wa Liverpool FC kwa kushinda taji la ubingwa wa Ligi kuu nchini Uingereza la msimu wa 2019/2020 unaweza kushitakiwa na kuhukumiwa adhabu ya kutoshangilia timu yeyote kwa miaka 6.

Kanali huyo ambae aliwahi kuwa mnadhimu wa jeshi la mashabiki wa soka, anasema kuchukua ubingwa wa EPL wakati bado zimebakia mechi 7 kumalizia ligi siyo kawaida, ukizingatia ni ubingwa wa mara ya 19 kwa klabu ya Liverpool FC.

Huyu Kanali siyo bure atakuwa Scouser au ana undugu na Steven Gerrard.

Ha haaaaa ..
Ni utani jamani hakuna kanali kama huyo duniani. Soma vizuri hayo majina na vyeo kabla haujakimbilia polisi kunishitaki.
 
Back
Top Bottom