Kamwe usitamani kuja jiji la Dar es Salaam.!

Kamwe usitamani kuja jiji la Dar es Salaam.!

Papaa Gx

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
11,508
Reaction score
18,668
Habari zenu wadau.

Moja kwa moja twende kwenye mada husika. Nakusihii na kukushauri ewe uliepo huko mikoani usitamani wala kufikiria kuja Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam kwa sasa limekuwa na kero nyingi sana zinazo fanya kuonekana kuwa chungu kwa wananchi.

Kero ziko nyingi ila binafsi ningependa kuzungumzia kero ya usafiri. Usafiri umekuwa ni shida sana katika jiji hili iwe asubuhi, mchana na jioni ndio tabu kweli kweli. Usafiri umekuwa shida sana kiasi kwamba ukienda katika vituo vya daladala kama vile Mbagala, Kariakoo, Banana, mawasiliano nakadhalika wananchi wamekuwa wakigombea usafiri.

Hii ni kero kubwa sana hasa kwa ndugu zetu walemavu, wazee wasiojiweza, wajawazito pamoja na mama wenye watoto wachanga. Kero hii pia imewaathiri kwa kiwango kikubwa wanafunzi, kundi hili limekuwa likichelewa kufika kwa wakati katika maeneo yao kero kubwa ikiwa ni usafiri.

Kwa hiyo kama unakuja Dar es Salaam ujue kuna kadhia ya usafiri.
 
Dar ni basi tu,hua nashangaa kumuona mkuu wao wa mkoa anagombana na watu kwa issue zisizo za msingi wkt dar yake ina matatizo mengi,mengi,mengi,mengi,mengi,mengi,mengi sana ikiwepo Usafiri na usafi wa jiji.

Anyway ngoja wanyonge tukae pembeni.
 
Kuna jamaa Yuko mkoani kila mambo yakichacha, anakuja daa kujitoa kafara katika kitafuta hadi anafanikiwa.
akifanikiwa anarudi kwao. Ila hii mara ya Tatu ameamua kubanana humuhumu.

kila kitu ni mtazamo tu, maana hata NewYork kunafoleni
 
Habari zenu wadau.

Moja kwa moja twende kwenye mada husika. Nakusihii na kukushauri ewe uliepo huko mikoani usitamani wala kufikiria kuja Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam kwa sasa limekuwa na kero nyingi sana zinazo fanya kuonekana kuwa chungu kwa wananchi.

Kero ziko nyingi ila binafsi ningependa kuzungumzia kero ya usafiri. Usafiri umekuwa ni shida sana katika jiji hili iwe asubuhi, mchana na jioni ndio tabu kweli kweli. Usafiri umekuwa shida sana kiasi kwamba ukienda katika vituo vya daladala kama vile Mbagala, Kariakoo, Banana, mawasiliano nakadhalika wananchi wamekuwa wakigombea usafiri.

Hii ni kero kubwa sana hasa kwa ndugu zetu walemavu, wazee wasiojiweza, wajawazito pamoja na mama wenye watoto wachanga. Kero hii pia imewaathiri kwa kiwango kikubwa wanafunzi, kundi hili limekuwa likichelewa kufika kwa wakati katika maeneo yao kero kubwa ikiwa ni usafiri.

Kwa hiyo kama unakuja Dar es Salaam ujue kuna kadhia ya usafiri.
Hivi haya mambo ya 'Usije dar 'bado yapo zama hizi, mi nijuavyo kwa ulimwengu huu wa utandawazi hakuna asiyejua mambo mbalimbali ya dar so hakukuwa na haja ya kuwaeleza watu wasiende dar by the way wewe ungeonesha mfano wa kuhama dar wengine wafuate
 
Foleni zamani bwana kipindi stendi ya daladala ubungo ipo Tanesco pale siku hizi foleni imetekwa,

By the way usiwatishe acha raia waje tupambane huku huku
 
Hiyo sio sababu ya kufanya watu wasije mjini ukitoa watu wanaokuja dar bila sababu kuna watu wanakuja kwa mishe maalamu inakuwa vipi unawaambie wasije dar kama mji umekushinda rudi mkoani kwenu waachie watu wanaoweza kukabiliana na hizo changamoto at least ungesema watu wasije sababu kuna vita ungekuwa sahihi ila kwa hiyo sababu haina mantiki.
 
Utakuta unatushahuri hivi wakati wewe upo hapo Dar es salaam, na sisi wavijijini tunataka tujekuchachua kidogo hapo mjini.

Tunasikia kuna mandege makubwa makubwa magari ya haraka na hata viwanda.

Namalizia kujichanga mwaka hauishi lazima na Mimi nije Dar
 
sisi wana kijiji hatuna shida,,
tunatembea Km 40 Kwenda na kurudi kuchota maji,,sembuse dar,,
au hamtaki tuje tuone SGR,mwendokasi,na fulayiova,,vipi tunaruhusiwa kupiga picha na dimulaina,,,
tukirudi kijijini tuzoe watoto wakali,,,,,
 
Ni kweli usemacho ,lakini hizo changamoto kuna mishe unaweza fanya bila kuadhiliwa na changamoto hizo xilizopo jijini
 
Back
Top Bottom