Mkuu Nyasiro hii iko poa zaidi. Nimependa sana ulivyobadilisha user interface. Nashauri uweke language selection wakati wa kuinstall mf. unaweza kuweka English na Swahili ili mtumiaji aweze kuchagua lugha atakayopenda wakati wa installation.
Inspired...as always 🙂
:A S wink: Bahati mbaya sikuweka clipboard monitoring.....
BTW
Nlitaka ku-implement KiSwahili Text to Speech katika kamusi hii lakini nimekwama kutoka na kutokuwepo kwa TTS engine. Kuna SwahiliTTS inaonekana imefanywa kwa Java na Wakenya katika Chuo Kikuu cha Nairobi lakini pia sijafanikiwa kuona inavyofanya kazi zaidi ya kuishia kusoma documents tu: http://www.ajol.info/index.php/ajst/article/viewFile/55170/43645
Nilipata matumaini kidogo nilipoona Speech Synthesizer inayo support kiswahili na nimejaribu kuipitia na kuona inavyofanya kazi, kwa ukweli imejitahidi lakini ina matatizo ya stress kwenye kutamka ny na ng' Tatizo sauti zinazokuwa generated sio za kiswahili ingawa zinafuata utamkaji wa kiswahili iangalie hapa + source codes eSpeak: Speech Synthesizer
Nyasiro,ningependa kuona SwahiliTTS engine inayofanya kazi ki-swahili na sio kizungu... ichek may be tunaweza kutengeneza engine yetu one day.
sad indeed!
Nyasiro,
Watanzania kwa situation ya sasa ni big failure, kuanzia viongozi mpaka waongozwa. Ni vibaya ila acha niseme tu kuwa Watanzania, hasa walio fani za ufundi kwa namna yeyote tumeiangusha sana nchi hii. Nimeshafanya initiative nyingi sana kujaribu kuleta unity ya hawa wataalam ili kufanya kitu ila mara zote nimekuta ni wabinafsi pasipo maelezo. Kila mtu anataka lake na hana mpango wa maslahi ya nchi.
Kwa hiyo nasikitika kusema kuwa hilo kwa sasa halitatokea na kama likitokea, basi itakuwa moja ya maajabu!
Mimi ninafikiria kuwekeza kwenye next generation zaidi kuliko hii ya sasa, so I don't think I will take on this initiative. Nataka kwenda vyuoni ambako vijana hawajawa tainted na ubinafsi uliopo kwa "weledi" wa mtaani.
Tanzania ina safari ndefu, na mpaka tutakapofika ... tuendelee tu na vya kizungu-kizungu
View attachment 166259
Na ikiwa maximized inaonekana hivi
View attachment 166260
So far naona sasa hivi imesimama vema software
Naona kama umekata tamaa. Mimi naamini hakuna kinachoshindikana hasa ukizingatia mfumo wa fonolojia ya kiswahili ni rahisi sana. Kiswahili kina irabu tano (a,e,i,o,u) ambazo utamkaji wake hauna mbwembwe. Pia tuna konsonanti na nazali (nasal) sounds ambazo hazina shida kabisa. Hii kitu naona ni rahisi kama kuhesabu 1-2-3. Tukipata engine ya namna hii tutarahisihsa sana utendaji kazi katika sehemu mbalimbali, kwa mfano usomaji wa hotuba na vitabu virefu ambavyo binadamu anachoka kusoma unaweza kurahisishwa sana.
Wazo la kwenda vyuoni ni zuri lakini kwa mfumo wa elimu wa Tanzania ni vigumu kupata mchango unaohitajika kwani unakuta mtu anasoma DIT kwa mfano ana course 10 sasa ukishamwambia kufanya kazi nyingine ya namna hii itakuwa ngumu kwake.
Wakenya wanazidi kutupiga bao kila sekta tupo nyuma sana. Watanzaia tunaumwa huu ugonjwa Tanzanian Surfers Loves News, Entertainment and Pornography na unahitaji tiba.
Tuanze kupunguza uzungu uzungu taratibu tutafika tu.
Shukrani sana kwa feedback naona karibia kila kitu kimekuwa aligned kama kilivyopangiliwa.
Sijakata tamaa ila naona kuna vitu kuvifanya Tanzania kama team ni kama haiwezekani.
Watu hawako serious, na walio serious wengi wabinafsi. Badala ya kuhangaika nao tumeamu tutafanya kama solo.
Kwa hiyo project ambazo tuliplan ziwe community driven zitabaki internal. Pamoja na mfumo wa elimu kuwa maiti, tutaendelea kumwaga sumu mashuleni/mavyuoni ili kizazi kijacho ndio kifanye yale tuliyo envision yafanywe na kizazi cha kwetu.
Lets die with our selfishness and let the youngsters shine!
Good work, kutakuwa na version nyingine? Nyasiro
Mkuu hiyo imekaa poa zaidi.vp kuna uwezekano wa kuifanya app kwenye simu? au haujafikiria hilo. itasaidia sana kwa sisi ambao hatujui lugha alafu pia hatuna pc
select * from dict where swahilisortby = 'ng'ombe'
select * from dict where swahilisortby = "ng'ombe"
Kuna bug nimeigundua.
Unapo search neno la kiswahili ambalo lina alama " ' " kama kwenye neno ng'ombe kamusi haileti majibu. Bila shaka kutakuwa na shida kwenye SQL SELECT STATEMENT. Ntalifuatilia suala hili.
UPDATE
Nilikuwa nafanya testing:
Na matokeo yanaonesha code hii haitafanya kazi
Code:select * from dict where swahilisortby = 'ng'ombe'
code hapo juu zina quote 1. katika sql single quote inatumika kuonesha mipaka ya string. kwa hiyo uki search neno kama ng'ombe SQL query ita search mpaka kwenye ng na hii italeta syntax error kwa sababu kunakuwa kuna string 2 ndani ya quote 1
lakini
code hii itafanya kazi vizuri kwa sababu kuna double quotes na string ni moja tu.Code:select * from dict where swahilisortby = "ng'ombe"
Sasa nimechanganyikiwa kidogo kuhusu matumizi ya double quotes na single quotes kwenye sql statements
CC Stefano Mtangoo zech snipa Sabrina and all devs