A
Anonymous
Guest
Sisi Mawakala wa kutuma na kuweka fedha kwa njia ya simu hasahasa hizi kampuni mbili pendwa hapa nchini najua mtakuwa mmeshazifahamu, tuna kilio chetu kuhusu kampuni za simu, hizo mbili zinatukata kuanzia Asilimia 10 hadi 20 ya commission tunayostahili kupata kwa kufanya miamala nje ya mkoa.
Yaani wanachokifanya ni kwamba Mawakala wanatakiwa kuhudumia miamala ndani ya mkoa husika ambao wakala yumo, na sio kutuma pesa kwenda nje ya mkoa mwingine.
Hivi tunajiuliza nini maana ya biashara huru? Mtu wa Congo hatakiwi kununua mzigo Kariakoo?
Huu ni wizi ambao umekuja kwa gia ya maelekezo kwamba wanaita eti ni miamala batili, ndio mana wanaifyeka. Nini shida? Sheria gani hiyo na kwanini?