Kampuni za Clearing ziangaliwe kwenye sakata la TRA la Umiliki wa Magari ya nyuma

Djprezzo

Member
Jul 22, 2013
17
7
Ukiachana na swala zima la kuuziana magari huko nyuma ama magari kuwa garage pia kuna issue ya hawa watu wa Clearing.
Kwa kipindi kirefu huko nyuma kulikua na tabia kwenye haya makampuni ya clearing and forwarding kubaki na copy ya vitambulisho vya wateja wao wakati wanawaagizia magari.

Vitambulisho hivi pia kwa kiasi kikubwa vilikua vikitumika kuagiza magari mengine ambayo yalikuaga yanaenda yard ama kuletewa mteja mwengine ambaye hana documents za kutosha.
So kiukweli janga hili watanzania wengi sana wataumia na wengine kwa asilimia 100 kabisa hawana kosa lolote.
Unaweza jikuta una miliki magari hata 20 mjini hapa bila kujijua!!!!

Tuchukueni tahadhari
Unaweza kua unadhani wewe msafi kumbe huko nyuma kuna mtu amekuchafua sana unajikuta unadeni la mamilioni kadhaa.
Na hali ilivyo ngumu sasa hivi Mungu Atusaidie kwakweli!!!!
 
mkuu kweli kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa hapa tanga alitumia kitambulisho cha rafiki yake ambae aliwahi kuagizia gari kupitia yeye baadae jamaa akashikwa na TRA unadaiwa mil kadhaa kivip katika maelezo yake kumbe rafiki yake alitumia kitambulisho chake kuleta magari yardini ilikuwa kesi kubwa but yule mfanyabiashara akakubali kweli alitumia mgongo wa mwenzie kuleta magari na spea
 
Siku ikijulikana umeagiza gari kwa kutumia information zangu jua ya kuwa "umaskini nimeuaga" bila jasho!! Wao wafanye tu hivyo!!!
 
Mkuu, unaweza kufafanua inakuwaje documents za mtu fulani zinatumika kuagiza gari la mtu mwingine?

Vipi malipo ya hilo gari, Excise Duty, registration na road tax, vyote vinatumia original documents kutoka kwa mteja wa kwanza kwa clearing agents?

Ila nnavyofahamu hadi sasa ni kwamba kuna watu ambao waliingiza magari na mizigo miaka kadhaa bila kulipa kodi stahiki au wasilipe kabisa na hawa ndiyo wanaotafutwa.
 
Back
Top Bottom