Mossad: Nguzo imara nyuma ya ustawi wa taifa la ISRAEL dhidi ya hila za SYRIA.

Complex

Complex

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Messages
3,994
Points
2,000
Complex

Complex

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2013
3,994 2,000
North Korea 2004, Treni ya mizigo ilikuwa ikisafiri katika moja ya miji yake iliyopatikana kaskazini mwa nchi hiyo iliyogubikwa na inayoendelea kugubikwa na usiri mkubwa juu ya mambo yake yanayoendelea nchini humo. Ghafla ukasikika mlipuko mkubwa na wa kishindo kikubwa sana kiasi kwamba kudhaniwa ni tetemeko la ardhi. Mtikisiko ule ulikaribia ukubwa wa 3.2 katika vipimo vya richter, kipimo ambacho hutumika kuelezea ukubwa wa tetemeko la ardhi. Mlipuko na tetemeko lile halikuwa tetemeko la ardhi kama ambavyo ingedhaniwa, Bali ulikuwa ni mlipuko wa hiyo treni ya mizigo iliyokuwa imelipuka na kusababisha madhara kwa takribani watu 3000 waliokuwa maeneo ya karibu na mlipuko huo ulipotokea na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 700. Taarifa toka vyombo vya habari na toka serikali ya nchi hiyo viliripoti kuwa treni ile ilikuwa imebeba Petroli na mlipuko ule ulikuwa umesababishwa na hitilafu katika treni hiyo ambayo ilipelekea mabehewa yaliyokuwa ndani yake kuna petroli kulipuka kwa kishindo.

Katika ulimwengu wa ulinzi na usalama wa mataifa yote duniani na vyombo vyake vya ulinzi na ujasusi, huwa hakuna taarifa kubwa wala ndogo. kwani wanaamini kuwa jambo lolote lile lazima lianzie katika taarifa na mawasiliano, hivyo basi huwezi kupuuza mawasiliano kwani pengine mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kupata kile ulichokuwa ukikihitaji. Habari hii ilifuatiliwa kwa ukaribu sana na mashirika ya kijasusi duniani, na shirika lililoonesha kuvutiwa zaidi na tamko la serikali ya korea kaskazini ni shirika la kijasusi la kizayuni, nalo si jingine bali ni lile linalotambulika kwa jina la, Mossad. Mossad kwa ukaribu chini ya mkurugenzi wake wa kipindi hicho aliyejulikana kama MEIR DAGAN, wakaanza kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu, na katika kufuatilia kwa ukaribu huko wiki moja baada ya tukio walishangazwa na taarifa za mamlaka ya anga ya nchi yao kuona ndege iliyokuwa ikitoka Syria kwenda korea kaskazini. Kitu ambacho ni nadra sana na ukizingatia hakukuwa na ukaribu huo baina ya nchi hizo mbili(Syria na Korea kaskazini) kitu ambacho kiliongeza shauku ya wao kutaka kufuatilia zaidi. Baada ya hiyo ndege kutua katika uwanja wa ndege nchini Korea kaskazini, waliendelea kushangazwa zaidi na walichokiona uwanjani hapo. Mossad walitaraji kuona ndege ikiwa na misaada ya ama vyakula ama mavazi kwa waathirika wa mlipuko ule, Ila badala yake waliona majeneza yasiyo ya kawaida 12 kwa idadi yake yakipandishwa katika ndege hiyo. Majeneza yale yalikuwa yametengenezwa kwa madini ya risasi(Lead) huku waliokuwa wameyabeba majeneza yale wakiwa wamevalia nguo maalum kama zile ambazo huwa zinavaliwa na wafanyakazi wa viwanda vya nyuklia na kemikali ama wanaanga wanapokwenda anga za mbali.

download-2-jpg.444631

Bw. Meir Dagan, Mossad spy chief 2002–2011

Hili lilimshangaza sana Bw Dagan, Na haikuishia hapo bali wakati wakiendelea kulitafakari hilo waliloliona uwanjani hapo, Dagan alipokea taarifa kuwa ndani ya majeneza yake hakukuwa na raia wa korea kaskazini, bali kulikuwamo na raia wa Syria, taarifa zilienda mbali zaidi kwa kusema kuwa na maiti zile zilikuwa ni za wanasayansi wa kisyria toka katika taasisi ya utafiti wa masuala ya kinyuklia ya siri iliyokuwa chini ya jeshi la syria. Kichwani mwa Bw Dagan kwa maana nyingine ilimaanisha kuwa ndege ya syria ilikuwa imekuja kufuata maiti za raia wake ambao uwezekano mkubwa walikuwamo katika mlipuko ule wa treni. Na hii ikapelekea Dagan kung’amua kuwa taarifa iliyotolewa na serikali ya Korea kaskazini kuwa treni ile ilikuwa imebeba mafuta ya petroli kuwa nayo itakuwa ni ya uongo. Hii ilipelekea Dagan kujiuliza swali ambalo alikosa jibu kwa muda huo, na swali hili halikuwa jingine bali ni “ Je hii inamaanisha Korea kaskazini wanawasaidia serikali ya syria kujenga kiwanda cha kutengeneza silaha za nyuklia.?? ”. Hii ilipelekea mossad kuunda kikosi kwa ajili ya kufuatillia suala hili kwa ukaribu 24/7/365.

London 2016, Miaka miwili baadaye, wakiwa bado wanalifuatilia hili swala la ukaribu, Mossad walipata taarifa za uwepo wa nia ya kusafiri kwa mmoja wa wanasayansi wa ngazi za juu kabisa wa masuala ya nyuklia kuelekea katika jiji la London. Alikuwa amepanga kusafiri peke yake, na hivyo akiwa bado nchini syria akabook kwa jina bandia chumba cha hoteli atakayofikia ambayo ilikuwa ni hoteli iliyojulikana kwa jina la KENSINGTON inayopatikana katika mji wa London. Baada ya kupata taarifa hiyo, bila kupoteza muda Mossad waliona hii ni taarifa tyenye manufaa kwao na wanaweza kuitumia vizuri kupata kile ambacho wamekuwa wakikifuatilia tangu miaka miwili iliyopita. Hii ilipelekea Mossad kuandaa timu tatu za takribani watu kumi kwa ujumla ambao waligawanywa katika makundi matatu. Timu ya kwanza ilijumuisha timu ya wachunguzi (spotters) ambayo ilitumwa katika uwanja wa ndege wa heathrow kwa ajili ya kumtambua na kuthibitisha utuaji wa mwanasayansi huyo pindi atakapotua nchini uingereza. Timu ya pili ilipangwa kwenda kufanya booking katika hoteli ambayo mwanasayansi alikuwa amepanga kufikia, na timu ya tatu ilikuwa kwa ajili ya kuangalia wale wote watakaokuja kumtembelea na kufuatilia nyendo za mwanasayansi huyo pindi atakapokuwa anazunguka katika mitaa ya London. Na timu hizi zilikuwa zimebeba watu wa aina mbili ambao wanapatikana katika nyanja za ujasusi. Miongoni mwa watu 10 wale wa mossad, ndani yake kulikuwa na watu kutoka katika kitengo cha KIDON ( hawa wanasifika kwa uuaji wa kimyakimya na kudungua) na pia kulikuwa na watu toka kitengo cha NEVIOT ( Hawa ni watu wa kuingilia mifumo ya milango, kufuli na kupandikiza visikilizi (bugs))

Baada ya kutua tuu jijini London, Timu ya mossad iliyokuwepo uwanjani hapo ilifanikiwa kumng’amua na kuwapa taarifa timu nyenzake kuwa mwanasayansi huyo amekwishatua. Hivyo kupelekea kwa timu ya pili kuianza kazi yake ya kumfuatilia kila anapokwenda. Kwa bahati alikwenda moja kwa moja mpaka hoteli aliyokuwa amepanga kufikia na baada ya kupaki mizigo yake, aliamua kutoka na kwenda kupata kinywaji katika baa ya karibu kwa jioni ya siku hiyo. Akiwa mwenyewe katika baa hiyo, ghafla alimuona msichana mrembo akiingia peke yake katika baa hiyo huku mrembo yule akionekana mwenye bashasha na furaha alikwenda kuketi karibu na alipokuwa ameketi mwanasayansi yule. Kama wahenga (wahenga wa kisasa) walivyopata kusema kuwa hakuna mkate mgumu mbele ya supu. Mwanasayansi yule alianza kubadilishana maneno mawili matatu na mrembo yule na kujikuta wakiwa katika lindi la maongezi. Alichoshindwa kugundua mwanasayansi yule ni kuwa, mwanamke yule hakuwa pale baa kwa bahati mbaya kama alivyodhania, bali alikuwa ni mmoja wa majasusi wa mossad na alikuwa pale kwa lengo maalumu, nalo si lingine bali ni kumpumbaza mwanaayansi yule huku wenzake toka kikosi cha Neviot wakijaribu kupenya kuingia katika chumba cha mwanasayansi yule kuangalia alichokuwa amekuja nacho na watakachokutana nacho.

Muendelezo..

Wakati bar maongezi yakiwa yamekolea, mossad walishafanikiwa kuingia katika chumba cha hoteli alichokuwa amefikia mwanasayansi yule kwa njia za kufoji security system za vitasa vya hoteli ile. Baada ya kufanikiwa kuingia wakakutana na kompyuta mpakato ya mwansayansi yule ikiwa mezani bila ulinzi wowote. Bila kupoteza muda, waliifungua na kuanza kazi ya kukopi kila kitu kilichokuwamo katika harddisk ya kompyuta ile na wakati huohuo wakitumia internet hawakupoteza muda walituma mjini Tel Aviv, Israel vyote walivyovipata toka katika kompyuta ya mwanasayansi yule, Baada ya kumaliza kutuma taarifa zile, walipandikiza katika kompyuta ile kirusi ambacho kitakuwa kinatuma taarifa kwao pindi tuu watakapokuwa yule mwanasayansi atakapokuwa antumia kompyuta ile, baada ya kumaliza yote hayo, walimuarifu yule mwanadada kule bar kupitia vispika vidogo ambavyo walikuwa wamevitumbukiza ndani wa masikio kasha wakaondoka, huku bar napo yule mwanadada alimuaga yule mwanasayansi na kumuacha solemba kwani kazi waliyokuwa wametumwa kuifanya ilikuwa imekwisha.

Iliwachukua takriban nusu saa kumaliza kukopi kila kilichokuwemo katika kompyuta ile na kukituma makao makuu. Baada ya nyaraka hizo kufika mezani kwa Bw Dagan, kazi ya kuanza kizichambua ikaanza. Miongoni mwa taarifa zile, kulikuwamo na picha ya jengo moja kuukuu ambalo kwa muonekano lilikuwa kwenye ujenzi, huku kukiwa na mtiririko wa picha nyingine zinazoonesha hatuakwa hatua ujenzi wa jingo hilo. Kwa kukadiria jingo lile lilifika takribani futi 150 kwa urefu na mapana huku likiwa na wastani wa futi 70 kwenda juu. Bw Dagan kwa haraka alishindwa kuelewa lilikuwa ni jingo la nini, lakini baada ya kuangalia vyema mtiririko wa picha zile alikuja kugundua picha ile ilikuwa ina ufanano mkubwa na jengo la YONG BYON linalopatikana korea ya kaskazini. Jengo hili la Yong Byon ni jengo ambalo ndani yake tafiti na utengenezaji wa makombora ya nyuklia unafanyika kwa korea ya kaskazini, hivyo ilikuwa ni dhahiri kuwa wasyria walikuwa wanatumia ramani za jengo la YONG BYON kujenga jengo kama hilo nchini mwao. Pia katika picha zile, zilionekana picha za baadhi ya wataalamu wa masuala ya nyuklia wa korea ya kaskazini na Syria wakiwa wamepiga picha za kumbukumbu. Hii ilibu swali alilokuwa akijiuliza Dagan na ilileta picha kuwa North korea wanawasaidia Syria kutengeneza mitambo ya kuchakata na kuunda makombora ya nyuklia.

Bila kupoteza muda Dagan aliiwasilisha taarifa ile kwa waziri mkuu wa kipindi hicho wa Israel Bw EHUD OLMET juu ya tishio hilo lililopiga hodi mlangoni mwao kama taifa. Jibu na maoni toka kwa Olmet kwenda kwa Dagan lilikuwa moja tuu, Kuwa ni dhahiri hicho kiwanda kinatakiwa kikome uundwaji wake. Na namna pekee ya kukiondoa ilikuwa si nyingine bali kukilipua. Lakini kaba ya kutekeleza hilo, Olmet alihitaji kujibiwa baadhi ya maswali na kufahamu baadhi ya mambo toka kwa mossad. Mambo hayo ni:

1. Je kiwanda hicho kimeshaanza kufanya kazi
2. Kiwanda hicho kipo eneo gani la Syria

Hayo yalikuwa ni maswali magumu kujibika, kwani picha walizokuwa nazo toka kwa mwanasayansi wa kisyria zilikuwa ni za miezi 15 iliyopita hivyo ilimaanisha kuwa yawezekana tayari kiwanda kilikuwa kishamalizika kujengwa na katika muda huo ambao walikuwa wanazungumza kilikuwa tayari kimeshaanza kufanya kazi. Hii ilimaanisha kukilipua kungeweza kuleta madhara makubwa kama kingekuwa tayari kimeshaanza kufanya kazi.

Dagan ilibidi aamuru moja ya satellite yao ya mawasiliano ifanye kazi ya kuichunguza Syria toka angani ili kujua ni wapi haswa kiwanda hicho kipo. Baada ya muda waligundua katika mji wa Al-Kabar kulikuwa na mawasiliano ya simu yasiyo ya kawaida toka nchini humo kwenda North korea. Hii iliwafanya waipeleke satellite katika anga la Al Kabar, na satellite ikiwa hapo Al-Kabar ilifanikiwa kuona picha ya jengo sawa na lile waliloliona katika picha walizokuwa nazo. Hii ilitatua swali la pili aliloulizwa Bw. Dagan, kuhusu swali la kwanza Bw Dagan hakuwa na jinsi zaidi ya kutuma watu kwenda kuchunguza kama kiwanda hicho kimeshaanza kazi ama laa. Kwa hili jambo ilibidi awasiliane na kikosi maalum cha jeshi ambacho kimebobea kwa suala la kufanya ujasusi katika nchi hasimu pasipo kutambulika. Hicho kikosi si kingine bali ni SAYERET MATKAL, hiki ni kikosi cha makomamdo wabobezi sawa kabisa na SPETSNAZ wa urusi ama NAVY SEAL ya marekani. Baada ya kuteuliwa watu hao, usiku mmoja wa majira ya kiangazi mwaka 2007 Walipanda helikopta ya kijeshi yenye mlio mdogo na kwenda mpaka Al-Kabar. Walifanikiwa kutua salama na walitua umbali wa kama maili moja hivi toka kiwanda kilipokuwa kasha wakaanza kutembea kwa miguu kuelekea kiwanda kilipo. Wakiwa umbali wa mita chache walikishuhudia kiwanda, kwa macho na wakaanza kutimiza kazi waliyotumwa. Kazi yao ilikuwa ni kukusanya sampuli za udongo na maji maeneo mbalimbali na jirani kabisa na kilipokuwa kiwanda kasha kuvipeleka Tel Aviv maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Walifanya kama walivyoagizwa, wakachukua sampuli hizo na kuanza kutembea sehemu waliyokuwa wametua na kuanza safari ya kurejea Israel usiku huohuo.

Baada ya kuwasilisha sampuli hizo maabara kwa ajili ya uchunguzi, majibu yalitoka kuwa kiwanda hakijaanza kazi na ripoti hii ilipelekwa kwa Bw Olmet. Ilikuwa ni majibu yenye unafuu, kwani zoezi lilokuwa linafuata ni kukilipua kiwanda hicho ili kisiendelee kuwepo na kisianze kazi yake iliyokusudiwa. Hivyo Olmet aliitisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Israel ili kujadili ni namna gani watakamilisha zoezi la kulipua hicho kiwanda cha nyuklia. Baada ya kujadili plan kwa kina wakaona watumie ndege za mmarekani za kivita za F16 na F15, na kuamuru ndege 10 na marubani wakae tayari kwa ajili ya shambulizi ambalo hawakuambiwa ni wapi. Hakuna mtu yeyeote miongoni mwa marubani wale wala nje ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofahamu ni wapi haswa zile ndege zitakwenda kushambulia kwani taarifa hiyo ilifanywa siri ya kiwango cha juu sana(top secret). Usiku wa September 6 2007, ndege zile 10 zilitoka katika kambi ya kivita Israel tayari kwa kwenda kufanya shambulio nchini Syria. Walipanga njia ya ndege zile iwe kupitia bahari ya mediterenean, kisha kuingia kuingia Syria kupitia uturuki. Waliwaomba uturuki kutumia anga yao ili kufanikisha wao kuingia Syria. Katika kituo cha kuongoza ndege hizo walikuwemo waziri mkuu na viongozi wote wa ulinzi na usalama wakifuatilia suala hilo kwa karibu moja kwa moja katika television zao. Dakika 10 baada ya kuanza safari, viongozi walijiridhisha ndege zote zilikuwa sawa na hazikuwa na hitilafu yoyote, hivyo wakaziamuru ndege tatu kati ya zile 10 zirudi nyumbani Israel huku zikiacha 7 zikiendelea na safari.

Wakiwa wanaimaliza anga ya uturuki tayari kwa kuingia Syria, marubani wale walipokea coordinate za eneo husika la kulipua. Kwani mpaka muda huo walikuwa hawafahamu ni wapi wanapoenda kulipua, kwa wakati huohuo waliziactivate katika ndege zao codes walizokuwa wamepewa kwa ajili ya kuzifanya ndege zao zisionekane na mfumo wa ulinzi wan chi ya Syria. Codes hizi waliuziwa na urusi, Bila ajizi ndege zile 7 zilifika katika eneo husika na kuachia mabomu yale na kuteketeza kabisa kiwanda kile na kubakisha majivu tuu. Kisha baada ya kumaliza, safari ya kurudi Israel ikaanza, walirudia kupitia njia waliyokuja nayo. Baada ya kufika Israel Olmet alikuwa kimya akisubiri Syria wangejibu vipi mapigo ingawaje alijua wazi kuwa hawangeweza kulalamika katika jumuia ya kimataifa juu ya uvamizi ule. Na kweli vyombo vya habari vya Syria kesho yake viliripoti kuwa majeshi ya Syria yamefanikiwa kuzifuruusha ndege vamizi toka katika anga yake na ndege hizo hazikuleta madhara. Huu ulikuwa ushindi mkubwa sana kwa Olmet na mossad. Lakini swali kuu liliibuka tena, nalo si jingine bali ni kwa namna gani kwa miaka saba Syria wamefanikiwa kuufanya mpango huo wa kiwanda kuwa siri hata vyombo vya kijasusi vya kimagharibi visiweze kuushtukia.?

Baada ya operation ya kulipua vinu vya nyuklia kukamilika katika ardhi ya Al Kabar, kwa mossad kazi ilikuwa ndiyo kwaanza inaanza. Kwani walitaka kujijibu swali lao la kuwa ni kwa namna gani serikali ya Syria ilifanikiwa kutekeleza jambo hilo kwa miaka saba bila ya vyombo vyao vya ujasusi kujua. Baada ya uchunguzi mrefu walifanikiwa kupata jibu la swali hilo. Na jibu lenyewe ni kwamba, serikali ya Syria walifanikiwa katika hili kwa kurudi zama za Ujima. Hii ina maana kwamba mawasiliano juu ya chochote kile kinachohusiana na mradi ule, basi mawasiliano yalifanyika kwa njia ya barua. Ilikwa mfano kuna mchoro unahitajika kutumwa toka syria kwenda korea, basi ulikuwa unaandaliwa mchoro ule, unawekwa katika bahasha kisha anapewa mtu kuupeleka mpaka korea akiwa na vitambulisho na passport yenye jina feki. Vivyo hivyo wakitaka kujadiliana juu ya maendeleo ya mradi, ilikuwa wahusika na wataalamu wanasafiri na kwenda kujadiliana. Hakukuwa na simu, email, fax wala chochote kile kinachohusiana na teknolojia katika ustawi wa huu mradi. Hivyo walikuwa wameandaa watu/wabeba mizigo na bahasha maalum. Hii ilizuia udukuliwaji wa taarifa za mradi. Na nyuma ya huu mradi na mipango yote alikuwa ni General MOHAMMED SULEIMAN.

Mossad hawakushangazwa kuibuka kwa jina la General Suleiman kama ndiye aliye nyuma ya mipango hiyo ya vinu vya nyuklia, kwani alikuwa halipendi taifa hilo Israel. Wakati mossad wakiwa katika furaha ya kuwazidi ujanja maadui wao wa Syria, ghafla walipokea taarifa za kijasusi kuwa Syria wamepanga tena kuanza kutengeneza kiwanda kama kile cha nyuklia ambacho kililipuliwa. Taarifa hii ilikuwa ni ya kushtusha sana kwa mossad. Ilibidi waitane tena wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kujadili nini cha kufanya juu ya jambo hili jipya linaloibuka. Baada ya kutafakari kwa kina, uamuzi ulioafikiwa ni kumuua mtu aliye nyuma ya mradi huo. Kwa maana nyingine walikuwa wameafikiana kumuua General Suleiman. Lakini Gen Suleiman hakuwa mtu ambaye anazagaazagaa hovyo tuu, isitoshe alikuwa na ulinzi ulokuwa ukikaribiana kabisa na raisi wake BASHIR AL ASSAD na ni watu wachache sana ndani ya serikali waliofahamu nyendo na ratiba zake za kila siku. Hii iliwalazimisha mossad kuanza kufuatilia nyendo zake. Haikupita muda, mwaka 2009 walipata taarifa kuwa General Suleiman atakuwa mapumzikoni katika nyumba yake iliyopo katika pwani ya mji wa Tartous. Hii ilikuwa ni habari njema kwa mossad, kwani ndiyo ulikuwa muda muafaka kwao kumuondoa bwana Suleiman duniani.

Mossad waliandaa wadunguaji wao wawili toka katika kikosi cha wadunguaji wa KIDON. Kisha baada ya hapo wadunguaji wale walisafiri kwa njia ya maji mpaka pwani karibu na ilipo nyumba yake, baada ya kufika pwani majira ya saa 3 ya usiku, huku bado wakiwa katika maji, na Gen suleiman akiwa barazani kwake, wadunguaji wale kwa pamoja walifurumusha risasi moja kila mmoja kuelekea alipo Gen Suleiman. Boooom, ilikuwa bahati kwa wadunguaji wale. Risasi moja ilimpata katika paji la uso, na nyingine ilimpiga katika shingo. General Suleiman alianguka chini palepale na kufariki dunia. Jambo hili lilifurahiwa sana Tel Aviv, na ndiyo ukawa ukomo wa mradi huo wa nyuklia kwa Syria kwani mtu aliyekuwa akiuendesha kwa mawazo na kimkakati alikuwa amekwishaondolewa duniani.

MWISHO
 
Boniphace Bembele Ng'wita

Boniphace Bembele Ng'wita

Verified Member
Joined
Dec 25, 2013
Messages
2,772
Points
2,000
Age
40
Boniphace Bembele Ng'wita

Boniphace Bembele Ng'wita

Verified Member
Joined Dec 25, 2013
2,772 2,000
mkuu unamaana kuwa umeikatisha?
 
Msafirishaji

Msafirishaji

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2016
Messages
1,260
Points
2,000
Msafirishaji

Msafirishaji

JF-Expert Member
Joined May 28, 2016
1,260 2,000
Ngoja ni subscribe huu uzi mkuu unitag ukiendelea weekend njema
 
dudupori

dudupori

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
1,364
Points
2,000
dudupori

dudupori

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2012
1,364 2,000
Mkuu Complex mie nasubiria ukimaliza unitag
 
busegwe

busegwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Messages
506
Points
250
busegwe

busegwe

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2013
506 250
Dah! Imeishia sehemu tamu kweli mm nashauli kwacbabu hatulipii hizi story ni bora ziwe zinaandikwa hadi mwisho akina shigongo wanafanya hivi ili magazeti yao yaendelee kuuzika ila ni tamu usisahau kunitag mkuu complex
 
NYIRO

NYIRO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2014
Messages
248
Points
225
NYIRO

NYIRO

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2014
248 225
kumekua na mfululizo wa stori nyingi za MOSSAD siku hizi hatupati na stori za mashirika mengine ya kijasusi kama ya Pakistani, UK ambako nako pia tunaambiwa wana intelijensia ya hali ya juu sana.
 
chinyika

chinyika

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2016
Messages
515
Points
500
Age
42
chinyika

chinyika

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2016
515 500
Fanya fasta wewe, umenikatisha utamu.
 
lwamu

lwamu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2015
Messages
930
Points
1,000
lwamu

lwamu

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2015
930 1,000
kumekua na mfululizo wa stori nyingi za MOSSAD siku hizi hatupati na stori za mashirika mengine ya kijasusi kama ya Pakistani, UK ambako nako pia tunaambiwa wana intelijensia ya hali ya juu sana.
Pekenyua nawewe u2letee...sa unasubiri nan akuletee kila siku...hangaisha akili yako kidogo mkuu
 
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
18,737
Points
2,000
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
18,737 2,000
North Korea 2004, Treni ya mizigo ilikuwa ikisafiri katika moja ya miji yake iliyopatikana kaskazini mwa nchi hiyo iliyogubikwa na inayoendelea kugubikwa na usiri mkubwa juu ya mambo yake yanayoendelea nchini humo. Ghafla ukasikika mlipuko mkubwa na wa kishindo kikubwa sana kiasi kwamba kudhaniwa ni tetemeko la ardhi. Mtikisiko ule ulikaribia ukubwa wa 3.2 katika vipimo vya richter, kipimo ambacho hutumika kuelezea ukubwa wa tetemeko la ardhi. Mlipuko na tetemeko lile halikuwa tetemeko la ardhi kama ambavyo ingedhaniwa, Bali ulikuwa ni mlipuko wa hiyo treni ya mizigo iliyokuwa imelipuka na kusababisha madhara kwa takribani watu 3000 waliokuwa maeneo ya karibu na mlipuko huo ulipotokea na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 700. Taarifa toka vyombo vya habari na toka serikali ya nchi hiyo viliripoti kuwa treni ile ilikuwa imebeba Petroli na mlipuko ule ulikuwa umesababishwa na hitilafu katika treni hiyo ambayo ilipelekea mabehewa yaliyokuwa ndani yake kuna petroli kulipuka kwa kishindo.

Katika ulimwengu wa ulinzi na usalama wa mataifa yote duniani na vyombo vyake vya ulinzi na ujasusi, huwa hakuna taarifa kubwa wala ndogo. kwani wanaamini kuwa jambo lolote lile lazima lianzie katika taarifa na mawasiliano, hivyo basi huwezi kupuuza mawasiliano kwani pengine mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kupata kile ulichokuwa ukikihitaji. Habari hii ilifuatiliwa kwa ukaribu sana na mashirika ya kijasusi duniani, na shirika lililoonesha kuvutiwa zaidi na tamko la serikali ya korea kaskazini ni shirika la kijasusi la kizayuni, nalo si jingine bali ni lile linalotambulika kwa jina la, Mossad. Mossad kwa ukaribu chini ya mkurugenzi wake wa kipindi hicho aliyejulikana kama MEIR DAGAN, wakaanza kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu, na katika kufuatilia kwa ukaribu huko wiki moja baada ya tukio walishangazwa na taarifa za mamlaka ya anga ya nchi yao kuona ndege iliyokuwa ikitoka Syria kwenda korea kaskazini. Kitu ambacho ni nadra sana na ukizingatia hakukuwa na ukaribu huo baina ya nchi hizo mbili(Syria na Korea kaskazini) kitu ambacho kiliongeza shauku ya wao kutaka kufuatilia zaidi. Baada ya hiyo ndege kutua katika uwanja wa ndege nchini Korea kaskazini, waliendelea kushangazwa zaidi na walichokiona uwanjani hapo. Mossad walitaraji kuona ndege ikiwa na misaada ya ama vyakula ama mavazi kwa waathirika wa mlipuko ule, Ila badala yake waliona majeneza yasiyo ya kawaida 12 kwa idadi yake yakipandishwa katika ndege hiyo. Majeneza yale yalikuwa yametengenezwa kwa madini ya risasi(Lead) huku waliokuwa wameyabeba majeneza yale wakiwa wamevalia nguo maalum kama zile ambazo huwa zinavaliwa na wafanyakazi wa viwanda vya nyuklia na kemikali ama wanaanga wanapokwenda anga za mbali.

View attachment 444631

Bw. Meir Dagan, Mossad spy chief 2002–2011

Hili lilimshangaza sana Bw Dagan, Na haikuishia hapo bali wakati wakiendelea kulitafakari hilo waliloliona uwanjani hapo, Dagan alipokea taarifa kuwa ndani ya majeneza yake hakukuwa na raia wa korea kaskazini, bali kulikuwamo na raia wa Syria, taarifa zilienda mbali zaidi kwa kusema kuwa na maiti zile zilikuwa ni za wanasayansi wa kisyria toka katika taasisi ya utafiti wa masuala ya kinyuklia ya siri iliyokuwa chini ya jeshi la syria. Kichwani mwa Bw Dagan kwa maana nyingine ilimaanisha kuwa ndege ya syria ilikuwa imekuja kufuata maiti za raia wake ambao uwezekano mkubwa walikuwamo katika mlipuko ule wa treni. Na hii ikapelekea Dagan kung’amua kuwa taarifa iliyotolewa na serikali ya Korea kaskazini kuwa treni ile ilikuwa imebeba mafuta ya petroli kuwa nayo itakuwa ni ya uongo. Hii ilipelekea Dagan kujiuliza swali ambalo alikosa jibu kwa muda huo, na swali hili halikuwa jingine bali ni “ Je hii inamaanisha Korea kaskazini wanawasaidia serikali ya syria kujenga kiwanda cha kutengeneza silaha za nyuklia.?? ”. Hii ilipelekea mossad kuunda kikosi kwa ajili ya kufuatillia suala hili kwa ukaribu 24/7/365.

London 2016, Miaka miwili baadaye, wakiwa bado wanalifuatilia hili swala la ukaribu, Mossad walipata taarifa za uwepo wa nia ya kusafiri kwa mmoja wa wanasayansi wa ngazi za juu kabisa wa masuala ya nyuklia kuelekea katika jiji la London. Alikuwa amepanga kusafiri peke yake, na hivyo akiwa bado nchini syria akabook kwa jina bandia chumba cha hoteli atakayofikia ambayo ilikuwa ni hoteli iliyojulikana kwa jina la KENSINGTON inayopatikana katika mji wa London. Baada ya kupata taarifa hiyo, bila kupoteza muda Mossad waliona hii ni taarifa tyenye manufaa kwao na wanaweza kuitumia vizuri kupata kile ambacho wamekuwa wakikifuatilia tangu miaka miwili iliyopita. Hii ilipelekea Mossad kuandaa timu tatu za takribani watu kumi kwa ujumla ambao waligawanywa katika makundi matatu. Timu ya kwanza ilijumuisha timu ya wachunguzi (spotters) ambayo ilitumwa katika uwanja wa ndege wa heathrow kwa ajili ya kumtambua na kuthibitisha utuaji wa mwanasayansi huyo pindi atakapotua nchini uingereza. Timu ya pili ilipangwa kwenda kufanya booking katika hoteli ambayo mwanasayansi alikuwa amepanga kufikia, na timu ya tatu ilikuwa kwa ajili ya kuangalia wale wote watakaokuja kumtembelea na kufuatilia nyendo za mwanasayansi huyo pindi atakapokuwa anazunguka katika mitaa ya London. Na timu hizi zilikuwa zimebeba watu wa aina mbili ambao wanapatikana katika nyanja za ujasusi. Miongoni mwa watu 10 wale wa mossad, ndani yake kulikuwa na watu kutoka katika kitengo cha KIDON ( hawa wanasifika kwa uuaji wa kimyakimya na kudungua) na pia kulikuwa na watu toka kitengo cha NEVIOT ( Hawa ni watu wa kuingilia mifumo ya milango, kufuli na kupandikiza visikilizi (bugs))

Baada ya kutua tuu jijini London, Timu ya mossad iliyokuwepo uwanjani hapo ilifanikiwa kumng’amua na kuwapa taarifa timu nyenzake kuwa mwanasayansi huyo amekwishatua. Hivyo kupelekea kwa timu ya pili kuianza kazi yake ya kumfuatilia kila anapokwenda. Kwa bahati alikwenda moja kwa moja mpaka hoteli aliyokuwa amepanga kufikia na baada ya kupaki mizigo yake, aliamua kutoka na kwenda kupata kinywaji katika baa ya karibu kwa jioni ya siku hiyo. Akiwa mwenyewe katika baa hiyo, ghafla alimuona msichana mrembo akiingia peke yake katika baa hiyo huku mrembo yule akionekana mwenye bashasha na furaha alikwenda kuketi karibu na alipokuwa ameketi mwanasayansi yule. Kama wahenga (wahenga wa kisasa) walivyopata kusema kuwa hakuna mkate mgumu mbele ya supu. Mwanasayansi yule alianza kubadilishana maneno mawili matatu na mrembo yule na kujikuta wakiwa katika lindi la maongezi. Alichoshindwa kugundua mwanasayansi yule ni kuwa, mwanamke yule hakuwa pale baa kwa bahati mbaya kama alivyodhania, bali alikuwa ni mmoja wa majasusi wa mossad na alikuwa pale kwa lengo maalumu, nalo si lingine bali ni kumpumbaza mwanaayansi yule huku wenzake toka kikosi cha Neviot wakijaribu kupenya kuingia katika chumba cha mwanasayansi yule kuangalia alichokuwa amekuja nacho na watakachokutana nacho.

........ itaendelea

CC:
Punainen, MTOTO WA KUKU, scorpnose, Mbimbinho, Daudi Mchambuzi, Mussolin5, the-sniper, MO11, upupuwapwani, Geniveros, Raimundo

Usisahau pia Mossad hata wewe watakutoa kizazi siku ukikanyaga Israeli, kama wanavyowafanyia watu weusi wote wenye asili ya Afrika waishio Israeli, na Waisraeli wanatuchukia sisi watu weusi zaidi kuliko binadamu yoyote yule, hivyo usijidaganye ukiona wanapigana na Waarabu ukafikiri wewe wanakupenda, ukiwauliza Waisraeli wachague kati ya Msyria na Muafrika kama mimi na wewe watachagua Msyria, na ndiyo maana hakuna Mwarabu aliyetolewa kizazi Israeli lkn Waafrika wote wamedungwa sindano na Mosad!
 
Great 4g

Great 4g

Member
Joined
Aug 25, 2016
Messages
31
Points
125
Age
48
Great 4g

Great 4g

Member
Joined Aug 25, 2016
31 125
Daah mkuu nilishaanza kuifurahia weekend halafu ghafla ukabadilisha hali ya hewa...kwenye hizo mambo wengine tumekuwa kama mateja, haishi bila_____.! Njoo uimalizie mkuu
 
Forum statistics

Threads 1,285,901
Members 494,777
Posts 30,878,319
Top