Salunbote Lyevedu
JF-Expert Member
- Jan 5, 2015
- 669
- 478
Tigo pesa ni zaidi ya jipu. Nilifanya muamala tar 22 mwezi wa saba kwenda mpesa, hela kwangu ilitoka na kwa mlengwa haikwenda nilipopiga huduma kwa wateja walinijibu pesa ipo kuna tatizo la kiufundi wanashughulikia hivyo nisubiri masaa 72. Yakapita nikapiga tena wakasema tena nisubiri masaa 72 ikawa hivyo kila nikipiga naambiwa hivyo hadi mwezi ukaisha wakasema kwakuwa mwezi umeisha niende tigo shop nikaenda ikawa mwendo uleule hadi leo hawajarudisha... Last week nilifanya malipo kwenda azam tv hela nayo haijafika hadi sasa wananipa kiswahili kama mwanzo tu. Hadi sasa ni zaidi 87000 wanayo sijui ndo nimeshaliwa au kuna mwaka watarudisha kama kuna aliyewahi patwa na hii hali hebu tupeane uzoefu