Kampuni ya Tigo mnawaibia wateja!

Kampuni ya Tigo mnawaibia wateja!

haswaaaaa ila tigo ni washindi kuliko wote, last week niliweka buku 2 eti badala ya msg kunipa balance ya 2,000 inanijulisha kuwa balance yangu ni sh 446 tu kwamba wamekata deni lao, sijawahi kopa hata siku moja na hata kama ni charge ya mlio ndio iwe 1,600! sasa hivi naweka 500 tu kwa wiki nzima, niko kwenye mitandao yenye adabu kidogo angalao


Huo ndiyo mchezo wanaonifanyia hata mimi! naudhika kweli aisee.
 
saa 10:23 salio 598 tar 30.8.2013


saa 13:44 salio 306 tar 30.8.2013


saa 6:24 salio 23 tar 31.8.2013

hapo sijampigia mtu au kumtumia sms

jamaa wezi
 
nilishaacha kutumia mtandao wa tigo siku nyingi sana kwasababu hiyo.
 
Tigo tuna wateja wengi sana. Hata nyie wote mnaodai kuibiwa mkihama tigo haidhuriki
 
Wanajamvi mjihadhali na wizi wa kampuni ya Tigo,mimi nimekutana na mkasa wa kuibiwa na Tigo mara tatu,nimejaribu kuwapigia kwenye number yao ya customer care napata majibu ya computer kwamba nirecord malalamiko yangu halafu watanijibu baadae,sijawahi kukopa kutoka tigo lakini nikiweka pesa tu wanakata pesa kama sh mia mbili na kuniambia nimemaliza deni langu.Hiki kitu inaniudhi sana na sasa nimeamua kuachana Tigo kabisa! hata kama pesa kidogo lakini ni wizi na huenda wanaibiwa watu wengi na huo ni utapeli,kwanini mteja akiwa na malalamiko arekodi ili ajibiwe baadae?

Kampuni za simu zinabidi kuchunguzwa sana kwa style za namna hii za wizi na nina wasiwasi hata kwenye tigo pesa watakua wanaiba pesa nyingi sana bila watu kujua.:disapointed:

Mkuu hata mimi yamenikuta!

Kuna siku niliongeza sh. 500 ili niweze kujiunga na extreme. Namaliza tu ku recharge ikaja msg kuwa nimewezeshwa sh. 500 hivyo nitalipa shi. 630. Ajabu ni kuwa wameniwezesha wakati sijaomba, na pia nina credit kwenye simu!

Hata hivyo nikaamua tu kujiunga extreme.

Baada ya muda wa extreme kumalizika, nikagundua na ile sh. 500 haiko. Nikaongeza sh. 500 nikitegemea wangekata sh. 130, nayo wakachukua. Nikaongeza sh. 500 nyingine nayo wakaichukua. Nilipoongeza sh. 500 mara ya tatu wakakata sh. 160. Toka siku hiyo nikaamua tigo basi!! Sasa hivi nimehamia Airtel naona wako fair!

Sasa najiuliza hawa TCRA wanafanya kazi gani wakati haya makampuni yanatuibia kiasi hicho?!
 
Na nyie mmezidi, laini ulionunulia boom wakati wa chuo mpk leo miaka 3-5 bado una tigo tu? Kwani umefunga nao ndoa?

Tigo line za wanafunzi
 
Na nyie mmezidi, laini ulionunulia boom wakati wa chuo mpk leo miaka 3-5 bado una tigo tu? Kwani umefunga nao ndoa?

Tigo line za wanafunzi

Wanaokumbatia Tigo huwa hawatoki nje ya Dar? ebu tokeni nje ya Dar muone kama mnaweza enjoy mkiwa Tigo Mambo yote yapo huku kwenye Baba lao!
 
Kuna mtandao mwingine siutaji jina, nao hawajakaa vizuri kwa suala zima la vifurushi, hawakuambii umetumia kiasi gani, ukiongea kidogo tu sms zinaingia eti kifurushi kimeisha. sijajua ndo kodi ya line inakatwa kila siku, wajirekebishe, tutaanza kutumia mtandao mmoja, kwanza vidakika vyenyewe viduchu kuliko mitandao mingine bado wanatuibia
 
Leo yani kuna mwenzangu mmoja analalamikia hayo hayo na akanambia haweki tena salio la.maongezi tigo. Mana juzi kaweka elfu 10 hajui hata kaongea na nani hela yote kushneh
 
Back
Top Bottom