Kampuni ya 'Mo' yaingia mkataba kuidhamini klabu ya Coastal Union

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
"Leo tunatangaza kwa furaha kubwa ushirikiano rasmi kati ya MO na Klabu ya Coastal Union kwa msimu wa 2025/2026!

Kwa MO, kauli mbiu yetu imekuwa daima: Tunagusa Maisha Yako.
Na leo, dhamira hiyo inapanuka zaidi tunaposimama bega kwa bega na moja ya timu kubwa kabisa nchini.

Kupitia MO Taifa Detergent na vinywaji vyetu vya MO, hatujadhamini tu mpira wa miguu—tunagusa nyumba, tunagusa jamii, tunaleta matumaini kwa vizazi vijavyo".
1758367042560.png

1758367068836.png
 
Mbinu flani za kijasu kuwakimbia mikia staa, yule mwamba miakili mingi sanaa...
 
Waseme ukweli mapema. Wamedhamini au wanamiliki hiyo team kama inavyomilikiwa simba
 
Simba na Yanga ni mali ya serikali inayotawala—Hakuna pesa inayoweza kununua hizo team( achana na propaganda umekuwa ukizisikia)

Hongereni kwa uwekezaji Mo, nitaleta kijana wangu kwa majaribio hapo.
 
"Leo tunatangaza kwa furaha kubwa ushirikiano rasmi kati ya MO na Klabu ya Coastal Union kwa msimu wa 2025/2026!

Kwa MO, kauli mbiu yetu imekuwa daima: Tunagusa Maisha Yako.
Na leo, dhamira hiyo inapanuka zaidi tunaposimama bega kwa bega na moja ya timu kubwa kabisa nchini.

Kupitia MO Taifa Detergent na vinywaji vyetu vya MO, hatujadhamini tu mpira wa miguu—tunagusa nyumba, tunagusa jamii, tunaleta matumaini kwa vizazi vijavyo".
Ajitahidi adhamini angalau timu nane
 
Naona visingizio sasa vitakosekana. Au ni mpaka zifikie timu 8 za Ligi kuu?
 
Back
Top Bottom