Kampuni ya mikopo ya nyumba yaanza nchini
Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,July 17, 2008 @00:04
Kampuni ya kutoa mikopo ya Nyumba ya Tanzania Mortgage imezindua shughuli zake nchini huku ikiwataka wananchi kujitokeza kununua nyumba mahali kokote nchini huku wakilipia pole pole.
Mtendaji Mkuu wa T Mortgage, Charles Inyangete, alisema jana kuwa kampuni yake imedhamiria kutoa mikopo kwa kila mwananchi ili mradi awe na kipato kinachoeleweka hata kama biashara yake ni ndogo.
sizani kama hao watu wa kipato cha chini watafaidika. Kila Bishara inayoanza Tanzania tunaambiwa ni ya kunufaisha mtu wa chini matokeo yake tunaona taratibu, Bay Port finance ya Mama mkapa ilianza hivi hivi, unaskia waalimu wanavyolia huko? Mi nashauri watu wawe macho, unaweza ukakopeshwa nyumba, hio gharama ya amkopo ikawa ni sawa na kujenga nyumba nyingine tano, tuwe makini tusije TUKADANGANYIKA kwenye hili tena
Google ' Charles Inyangete' Mtendaji Mkuu wa T Mortgage, utapata http://www.mutualdevelopers.com/index.asp itakuwa ndiko ilikoanzia T Mortgage ...
hahhaa a mimi niliuwa na wazo moja....hawa NHC,Lapf,NSSF,PPF....na wengineoo..wote wakusanyike waunde kamati kufanya mradi mkubwa sana wa nyumba za wafanyakazi na wafanyabiashara,wakulima...waweze kukopa....ninaamini itafanya kazi...na tena italeta tija kubwa sana sana......wajenge hata maghorofa ya sieze tofauti kutokana na kipato na uwezo wa watu mbali mabli...low,medium,high...........watu wauziwe nyumba,................wakatwe kidogo kidogo na ukichukuliaa amana zetu zimelala tuu huko kwao wanawakopesha wenye "access" na wahindi wanaojifanya wana akili zaidii na wanaowahonga .............rushwa tupu........fanyeni kitu kwa nchi yenu mkiwa na madaraka na si kujilimbikizia mali.....yaani nchi ndio inakufanyia jambo......badala ya nyie viongozi kuiffanyia nchi yenu............inasikitisha sanaa.......
Hii si habari mbaya kwani anaonesha nia ya hawa watu kusaidia.
Je hawa jamaa wana tovuti yao?
Ningependa kuona kwamba hawa jamaa wanaeleza kila kitu pia kupitia mtandao au tovuti ili watu waelewe na wachanganue mchele na pumba.
Ni katika zama hizi ambapo teknolojia imekua sana na sioni tatizo kama jamaa zetu hawa watashindwa kuwa na tovuti.
Bila hivyo watakuwa hawaeleweki.
...Alisema wameanzisha T mortgage kusaidia kukabili upungufu huo kwa kuwapatia watu kama mkopo. "Kama kampuni tuna lengo moja tu la kuwasaidia Watanzania kupata nyumba wanazohitaji kwa urahisi…kwa kawaida umiliki wa nyumba nchini ni mchakato mrefu, sisi tunabadili hali hiyo."