BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,144
Kampuni ya mikopo ya nyumba yaanza nchini
Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,July 17, 2008 @00:04
Kampuni ya kutoa mikopo ya Nyumba ya Tanzania Mortgage imezindua shughuli zake nchini huku ikiwataka wananchi kujitokeza kununua nyumba mahali kokote nchini huku wakilipia pole pole.
Mtendaji Mkuu wa T Mortgage, Charles Inyangete, alisema jana kuwa kampuni yake imedhamiria kutoa mikopo kwa kila mwananchi ili mradi awe na kipato kinachoeleweka hata kama biashara yake ni ndogo.
Alisema Watanzania walio wengi wanahitaji nyumba, lakini kutokana na gharama za nyumba kuwa juu wengi wao wameshindwa kujenga huku taasisi za kifedha zilizoko zikiweka masharti magumu ya kuwakopesha.
Inyangete alisema kampuni yake inaweka utaratibu rahisi wa kuharakisha ununuzi wa nyumba kama mteja anavyonunua simu ya mkononi. Kwa miaka mingi iliyopita imekuwa dhahiri kwamba soko la kumiliki nyumba nchini halihudumiwi vya kutosha.
Alisema upungufu wa nyumba unakadiriwa kuwa kati ya milioni mbili na tatu na huongezeka kila mwaka. Alisema wameanzisha T mortgage kusaidia kukabili upungufu huo kwa kuwapatia watu kama mkopo. Kama kampuni tuna lengo moja tu la kuwasaidia Watanzania kupata nyumba wanazohitaji kwa urahisi kwa kawaida umiliki wa nyumba nchini ni mchakato mrefu, sisi tunabadili hali hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Mauzo wa T Mortgage Chriss Gumbe alisema anachotakiwa kufanya mteja anayetaka kununua nyumba kwa mkopo ni kwenda kuonana na uongozi wa kampuni hiyo na kueleza namna anavyopata kipato chake. Alisema kampuni hiyo inawasiliana na kampuni na watu binafsi ambao wanauza nyumba, hivyo mteja ambaye anaingia mkataba na T mortgage ananunuliwa nyumba hiyo na jina la umiliki linakuwa la kwake.
Aliongeza kuwa mteja anachotakiwa kufanya ni kuiweka bima nyumba hiyo ili hata akifukuzwa kazi au biashara zake zikiyumba asije akanyanganywa nyumba hiyo badala yake kampuni za bima zinachukua jukumu hilo la kuendelea kulipa mkopo huo. Sisi mtu anakuja anatuambia kipato chake na sisi tunatathmini kuwa nyumba anayostahili kukopa thamani yake ni ya kiasi fulani tunaanzia kutoa mkopo wa Sh milioni 15 kwenda juu, alisema Gumbe.
Alisema kwa sasa wanazo nyumba zaidi ya 1,000 ambazo kampuni yake imeshawasiliana na kampuni katika miji mbalimbali nchini hivyo watu ambao watahitaji kukopeshwa nyumba hizo wanalazimika kuwasiliana na T-Mortgage ili waweze kupatiwa mikopo hiyo. Utaratibu huo pia unawahusu Watanzania wanaoishi nje ya nchi ambao wanahitaji kununua nyumba wanaweza kuwasiliana na kampuni hiyo ili kurahisishiwa upatikanaji wa fedha.
John Tate ambaye ni ofisa wa fedha wa T-Mortgage alisema watawasadia zaidi wateja wa kipato cha chini na cha kati wanaopata shida kumudu kodi kubwa na fursa chache za kukimbilia. Alisema kwa kutoa njia rahisi na ya haraka kwa wateja hawa kununua nyumba na kulipia polepole kwa kipindi fulani wanaweza kuhitimisha ndoto zao za kumiliki nyumba kuwa za kweli.