Kampuni ya migodi ya North Mara (ACACIA) kupunguza wafanyakazi 1200

Embu fafanua hizi hesabu, ndo package waliyowapa wote 1200 au ni makisio yako kutokana na uzoefu?

Hapa buzwagi gemu ni gumu zaidi, ila hawa jamaa wanachelewesha kuwapa watu barua zao wajipange na maisha mengine
 
Mlianza na africa mashariki gold mine (amgm), later on mkabadili kuwa placerdome, baadae kidogo mkaitwa barrick, sasa acacia, karibuni kijiweni, uzuri mm nili resign mwenyewe kwenye retrenchment ya global world economic crisis early 2009. Hiyo ndio ccm
 
shida iko wapi kama mwenye mali anaamua kufanya hivyo kwa future ya biashara yake,,, "tuchukulie wewe ndio barrick sasa na unaona ili biashara iende lazima watu wapungue utafanyaje" lazima tuishi kulingana na maendeleo ya dunia, kuongezeka kwa automation kunapunguza soko la ajira hivyo lazima tuwe flexible kupambana na hii hali, pia makampuni mengi ya migodi yanatumia sana CONTRACTORS ambao hulipwa vizuri na kutumikishwa kupita kiasi ili malengo yafikiwe---.
wafanyakazi wengi wa ACACIA kama kampuni mama MLIBWETEKA sana nakuwa lazy kwa kujiona hapo ndio mwisho wa maisha, lazima ukweli usemwe, ACACIA imeamua kuwekeza kwa contractors ambao wanapiga kazi kimbwa mfano BINERCUT, SANVIC, MANTRAC pale buly na North mara.. PANAF na ATLASCOPCO pale buzwagi... sasa nyinyi ACACIA ukampuni mama uliwalemaza na kujiona maisha yenu ndio hivyo miaka nenda rudi.

Vilevile tunapouwa kazini tujifunze kutunza hela na kuishi kulingana na vipato,,, tunapokuwa kazini tujifunze na maisha ya mtaani hata kumiliki magenge ya nyanya na sio muajiri anaamua kuachana na wewe na kukulipa stahiki zote nakuja kulia lia...
 
Ungechagua lowassa yote haya yasingewafika! Si mlisema hapa kazi tu! Eeh?! Kazi ndo hiyo imeanza!
 
Kule Manyara, kuna kampuni inaitwa TanzaniteOne Mining Ltd, wao nasikia wanapunguza wafanyakazi 600 mwezi huu wa 11. Sababu za kuwapunguza wafanyakazi bado sijafahamu.
 
mwendelezo wa kuisoma namba tu mwaka huu

Hawa watingaji hawanaga shukurani, mwaka jana mwenzao alitumbukia shimoni Maige akaweka kambi hadi akapatikana cha kushangaza kwenye kampeni walimshambulia kwa mawe, wale jamaa wa "mama mkanye mwanao" wakiongozwa na Ray walikimbia na kuvua majezi yao. Leo wanapunguzwa wanaanza kuomba msaada wa serikali.
 
Sioni shida hapo, kwani mlitaka mfanye kazi katika hayo machimbo hadilini?, ingekuwa mnafukuzwa bila kosa it's another issue, lakini kama ni redundancy haina shida just check out how much will you get, I mean terminal benefits then kajipangeni upya na maisha mapya.
 
Ginyaginya liko mgodi wa Bulyanhulu,unaingia kazini barua ya kuachishwa kazi inakufuata shimoni hukohuko. Jana mkuu wa kituo polisi Bugarama ambacho kinahudumia maeneo ya vijiji vinavyozunguka mgodi alisema hivi sasa anasuruhisha kesi za wanawake kupigwa na waume zao lkn anahisi chanzo ni stress za lindandasi.
 
sehemu yoyote duniani bepari anaangalia maslahi yake tu ndio maana akipata hasara kidogo anapunguza wafanyakazi hii ipo duniani kote lakin kabla hajapunguza kwa sheria za nchi zilizoendelea lazima atoe barua miezi 3 kabla na pia wakipungizwa wanalipwa haki zao
 
Uko nako kuna JIPU ni bora litumbuliwe tufaidi dhahabu zetu....maswala ya kuingiza mafuta bure iwe mwiko maswala ya kutolipa kodi na kubadili majina ya kampuni ze BULDOZER huo ujinga na uhuni anaujua watuambie BARICK GOLD MINE imekuaje ikawa ACACIA km sio kukwepa KODI???
 
Tetesi nyingine ni kuwa wanataka kufungasha virago kwa kuwa wanadaiwa kodi na kwa miaka mingi wamekuwa hawalipi na hawana imani utawala wa JPM maana wanajua JPM hatawavumilia.

Vv
 
Kwenye nchi inayo linda ajira za raia wake zinge anza na kupunguza wafanyakazi wageni kwanza,pili serikali ingekaa na huuo mwekezaji na kutafuta nchia bora ya kunusuru ajira za raia wake...mathalani baadhi ya kodi zina simamishwa kwa muda ili kulinda ajira
mwaka 2009 mkodi wa madini ya nikeli pale Francistown Botswana walitaka punguza wafanyakazi baada ya bei ya nikeli kuporomoka ..serikali yao ilisimamisha baadhi ya kodi ili kulinda ajira za raia wake mpaka mambo yalipotengemaa
 
Safi, waende kule bagamoyo kuna malaki ya maeka ya mashamba hayajalimwa, na mvua zilikuwa nyingi, hiyo nguvu kazi ikalime sasa
 
Basic salary divide by 7 months work si haba. Maana nimefanya miaka 12, pesa ya kuweka costa barabarani ipo. Wala sishtuki, bado NSSF, bado termination benefits, nachekelea tu wala siogopi kuingia mtaani. Ni kiasi cha kubadili lifestyle tu.
Kama uliwahi kujitambua mapema. Kuna jamaa yangu yuko huko hata kodi tu huwa inamzingua. Sijui akipunguzwa hali itakuwaje?
 
Back
Top Bottom