Kampuni ya mafuta ya Total kuanza ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanzania hadi Uganda

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo amemuhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha Mafuta kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga hapa Tanzania haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

Bw. Javier Rielo ametoa ahadi hiyo leo tarehe 14 Machi, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.

Katika Mazungumzo hayo Bw. Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.

Pamoja na kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, na itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wake.

Prof. Mhongo amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania, ambazo zikikamilika kwa mafanikio inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
 
image.jpeg
 
__320x320_56de68b88fe4c.jpg
james-mataragio.jpg


Construction of the long-awaited Tanzania-Uganda crude oil pipeline is expected to start in August this year, and will be completed in 2019.

James Mataragio, Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) Executive Director said last week the $4 billion project will speed up the socioeconomic development between the two East African nations.

Sources say theTanzanian and Ugandan Presidents approved the project ahead of the just concluded 17th EAC Summit in Arusha.

The 1,403-kilometre pipeline will link oil fields in Uganda’s Lake Albert, Hoima region from the Tanga port in Tanzania. According to the TPDC official, the construction of the crude oil pipeline will be carried out by three oil firms, namely: UK’s Tullow Oil PLC, France’s Total E&P and China’s Cnooc.

Mataragio was optimistic that the project would start and complete within the time-frame. Once completed, the oil pipeline will be able to transport up to 200,000 barrels per day passing through a number of Tanzanian regions from the Indian Ocean port of Tanga to Uganda.

“It is anticipated that over 200,000 tonnes of bare pipes, materials and equipments such as pipe insulation, pump, bulk heating and trace heating stations will be imported through Tanga port,” he said.

The pipeline construction is expected to create more than 15,000 jobs.

He said the crude oil pipeline project will also increase the Foreign Direct Investment (FDI) to Tanzania by more than 50% per annum
.

He said the construction will lead to installations of 200km of permanent new roads and corresponding bridges, and upgrades to 150km of existing roads.

The project will also open up regional integration in the energy sub-sector in which Uganda is expected to import natural gas from Tanzania.
Huu ni mradi mkubwa saaannaa !
 
They need us more than we need them. Wala tusishoboke Sana,they shud do it on our terms, hawataki waende wakanywe hayo mafuta yao kwa mkate wa siagi.
 
They need us more than we need them. Wala tusishoboke Sana,they shud do it on our terms, hawataki waende wakanywe hayo mafuta yao kwa mkate wa siagi.
Ha ha ha ha
Mkuu punguza hasira mkuu,nimeona kwenye taarifa moja kwamba wameamua kujenga kwa gharama yao almost $ 4 bn japo mwanzo walipewa offa ya kujenga kwa ku share gharama na Kenya lakini walikataa.

Wameamua kugharamika bomba lote tangu Uganda mpaka Tanga, Mwanzoni walitakiwa kujenga mpaka mpakani mwa Kenya lakini wamestuka.
Magufuli naye kaamua kuwapoza wakenya kwa kuwapanulia barabara ya Mombasa Arusha
 
Samahani jamani, mie sijaelewa vizuri katika hilo bomba Tanzania tunanufaikaje? Au ndo kama lile bomba ia TAZAMA Pipeline? Manake sie tunaishia kulitazama tuuu likipita, hizo ajira zinapatikanaje kwa kupitisha bomba? Twawaoma ma GT watujuze.
 
Ajira za vibarua wa kazi za kutumia nguvu na kuchafuka kwa malipo kiduchu unashangilia, jamani jamani jamani mweeeee
 
JPM atatusaidia sana this time kupambana na fitna za Wakenya,hii habari itakuwa ina ukakasi sana kwenye media za Kenya na serikali yao kwa ujumla,wakati wao wanaandaa ujumbe kwenda Uganda ndani ya siku 10 kumshawishi M7,huku Dar es salaam Boss wa Total ameitwa Ikulu na kupewa neno,JPM inaonekana hizi siasa za hivi amebobea na amesisitiza kuwa muda wa miaka 3 kumaliza mradi huu ni mwingi sana hivyo upunguzwe!,fedha zipo tayari na kazi inatakiwa ianze mapema iwezekanavyo."well done Mr President and God bless Tanzania"
 
JPM atatusaidia sana this time kupambana na fitna za Wakenya,hii habari itakuwa ina ukakasi sana kwenye media za Kenya na serikali yao kwa ujumla,wakati wao wanaandaa ujumbe kwenda Uganda ndani ya siku 10 kumshawishi M7,huku Dar es salaam Boss wa Total ameitwa Ikulu na kupewa neno,JPM inaonekana hizi siasa za hivi amebobea na amesisitiza kuwa muda wa miaka 3 kumaliza mradi huu ni mwingi sana hivyo upunguzwe!,fedha zipo tayari na kazi inatakiwa ianze mape
ile barabara ya arusha~taveta/holili nayo itakua tayari mnamo december 2018 nowdays nchi yetu inasonga mbele ati
 
Samahani jamani, mie sijaelewa vizuri katika hilo bomba Tanzania tunanufaikaje? Au ndo kama lile bomba ia TAZAMA Pipeline? Manake sie tunaishia kulitazama tuuu likipita, hizo ajira zinapatikanaje kwa kupitisha bomba? Twawaoma ma GT watujuze.
kwa kuwa haya ni mafuta ghafi, sidhani kama itasaidia kwa upande wa upatikanaji mafuta Moja kwa Moja, ila kama tutaweza kufufua TIPA ili tuyanunue Moja kwa Moja kwenue bombs then tuyasafishe inaweza kuwa faida, ila this is very unlikely coz Uganda wenyewe wanauza ghafi. Labda faida tutapata kwenye ajira za vibarua Wa ujenzi. Au labda tutakuwa na supremacy na heshima toka Uganda kwa kuwa tuna-host mshipa wao Wa damu, wakizingua tu tunautumbua huo mshipa.Nevertheless, 4bn$ will be injected into our economy sort of, that's 8trn tshs, now that's a big deal
 
kwa kuwa haya ni mafuta ghafi, sidhani kama itasaidia kwa upande wa upatikanaji mafuta Moja kwa Moja, ila kama tutaweza kufufua TIPA ili tuyanunue Moja kwa Moja kwenue bombs then tuyasafishe inaweza kuwa faida, ila this is very unlikely coz Uganda wenyewe wanauza ghafi. Labda faida tutapata kwenye ajira za vibarua Wa ujenzi. Au labda tutakuwa na supremacy na heshima toka Uganda kwa kuwa tuna-host mshipa wao Wa damu, wakizingua tu tunautumbua huo mshipa.Nevertheless, 4bn$ will be injected into our economy sort of, that's 8trn tshs, now that's a big deal

8 trillions will be injected into our economy if we supply labor and materials used to lay down the pipeline.

It will be the vice versa if they import everything.
 
Back
Top Bottom