Kampuni ya LG Electronics yazindua duka la bidhaa za Majumbani Dar es Salaam

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kampuni ya LG Electronics imesema ina mpango wa kuimarisha uwepo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kufungua maduka mapya katika nchi nne ili kukidhi mahitaji ya wateja wa vifaa vya nyumbani na viyoyozi.

Kampuni hiyo, ambayo Juni 7, 2021 imezindua duka jipya katika mitaa ya Posta karibu na mnara wa saa Jijini Dar es Salaam, imesema miendendo ya wateja inaonesha ongezeko kubwa la uhitaji wa bidhaa zake hapa nchini.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, Bw. SaNyoung Kim alisema hili ni duka la kwanza jijini Dar kwani dula la pili linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City.

Kwa mujibu wa Bw. SaNyoung Kim, maduka haya yataimarishwa vilivyo ili kuongeza mauzo na kuwapa wateja nafasi nzuri ya kufurahia teknolojia na bidhaa mpya za kampuni hiyo kama vile TV ya OLED, friji ya InstaView, mashine ya kufulia ya TWINWash, mashine ya kupashia chakula aina ya Neochef na mashine za kufulia yenye nguvu ya AI DD AI.

“Posta na Mlimani City ni maeneo mwafaka kabisa kwa sababu ya wateja wengi wanatembelea maeneo hayo na tumejionea namna mazingira ya biashara Tanzanaia yalivyochangamka.

Tunaahidi kuwapa wateja wetu huduma na bidhaa nzuri ili wajisikie fahari wakati wanafanya manunuzi kwani watahudumiwa na wafanyakazi wetu wenye utaalamu wa hali ya juu,” alisema Kim, huku akiwaomba Watanzania watembelee maduka hayo mawili ili wajionee wenyewe.

Kuhusu kufungua maduka mengine mikoani, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, David Kessy alisema kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara katika soko la vifaa hivyo, wanafikiria kufungua maduka mikoani katika siku za usoni.

“Katika miaka michache iliyopita, tumekuwa tukitanua wigo na uwepo wetu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tuna mpango wa kuendelea kukuza bidhaa zenye hadhi ya premium na kuwapa wateja wetu bidhaa wanazotarajia wao binafsi na kama biashara kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa zaidi ya daraja la kwanza,” alisema Kessy.

Kessy alisema mauzo ya vifaa vya umeme yameongezeka kutokana na wateja wengi kununua vifaa vya kiteknoojia zaidi kwa matumizi ya nyumbani na pia kwa masomo, mapishi na burudani.

“Ni wazi kuwa wakati huu wa janga la Corona, teknolojia imekuwa muhimu sana katika maisha ya watu huku tukishuhudia uvumbuzi mbalimbali ambao unaendana na ufanisi na afya bora,” aiongeza Kessy.

Alisema LG kwa sasa inasambaza vifaa vya hadhi ya premium vyenye uwezo wa kutumia nishati kidogo katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuhakikisha utunzaji wa mazingira na rahisi kutumia. Mwaka jana, LG ilizindua maduka maalumu ya mtandaoni nchini Kenya ili kukidhi mahitaji ya wateja wanaopendelea kununua vifaa vya umeme kwa njia ya mtandao.

Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, Bw. SaNyoung Kim (kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo katika mitaa ya Posta karibu na Mnara wa saa jijini Dar. Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa LG –Tanzania, Manish Jangra.Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, Bw. SaNyoung Kim akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka hilo.Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya LG Electronics, David Kessy akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani.Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni ya MeTL, Fatema Dewji ambayo ni mshirika wa kampuni ya LG akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka hilo.Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa duka hilo jipya la bidhaa za LG lililopo Posta jijini Da
IMG-20210608-WA0009.jpg
IMG-20210608-WA0006.jpg
IMG-20210608-WA0004.jpg
IMG-20210608-WA0007.jpg
IMG-20210608-WA0005.jpg

View attachment 1812137
 
Katika picha ya kwanza, huyo kushoto ni mdogo wake na Mo, anaitwa Hussein Dewji.. Ni Director of Sales and Marketing- METL
Huyo unaemsema ni Hussein Dewji ndio! Ila Hussein sio director wa Sales and Marketing pale METL! director of sales and marketing-METL ni Fatema Dewji,mdogo wake Mo mwisho! Ni huyo binti kwenye picha ya nne hapo kavaa nguo kama za njano hivi
 
Hilo duka la LG, lilikuwepo Mkwepu street kitambo, au wamelihamishia Posta location tofauti??

Basi sawa kazi iendelee!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kwahiyo wale wapuuzi wa Kariakoo wanaosemaga wao ni Authorized Sellers ni wahongo?
 
vijana tuache kulialia, tutafute mitaji tulete ushindani kww hawa weupe...tuachane na hang'over ya ukoloni...
 
Back
Top Bottom