Kampuni ya Kukopesha

Kampuni ya Kukopesha

Wadau wa JF ,naomba mnisaidie ni hatua gani za kufata kuweza kusajili na kumiliki kampuni ya mikopo
Hatua ya kwanza ni kusajili kampuni BRELA. Mkurya mweupe Kampuni ya mikopo ina masharti ya kufuata ikiwemo jina la kampuni lazima liwe na "finance" au "Microfinance" au "financial services", au "credit"....

Ukishamaliza kusajili kampuni, hatua ya pili ni kuomba leseni ya Biashara ya mikopo kutoka Benki Kuu. Benki Kuu ina matawi kwenye Kanda, hivyo utaombea kwenye kanda iliyo karibu nawe. Lakini kabla hujaenda Benki Kuu lazima uwe na tax clearance... Kuna attachment kama 10+
,pia ni gharama kiasi gani zinahitajika mpaka kukamilisha kabisa usajili wake .....
Gharama kiasi gani... Hamna hamna angalau 3 million kwa ajili ya BRELA, muhuri wa Mwanasheria, TRA, photocopies, mihutasari ya vikao vya Bodi, forms za board members......

Hongera sana, fikra ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye mafanikio.
 
Hatua ya kwanza ni kusajili kampuni BRELA. Mkurya mweupe Kampuni ya mikopo ina masharti ya kufuata ikiwemo jina la kampuni lazima liwe na "finance" au "Microfinance" au "financial services", au "credit"....

Ukishamaliza kusajili kampuni, hatua ya pili ni kuomba leseni ya Biashara ya mikopo kutoka Benki Kuu. Benki Kuu ina matawi kwenye Kanda, hivyo utaombea kwenye kanda iliyo karibu nawe. Lakini kabla hujaenda Benki Kuu lazima uwe na tax clearance... Kuna attachment kama 10+

Gharama kiasi gani... Hamna hamna angalau 3 million kwa ajili ya BRELA, muhuri wa Mwanasheria, TRA, photocopies, mihutasari ya vikao vya Bodi, forms za board members......

Hongera sana, fikra ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye mafanikio.
Huu mlolongo labda mtaji uwe na million 100
Hadi uwe na bodi
 
Kampuni ni lazima iwe na Bodi. Bodi inaweza kuwa ya watu 4 tu; wewe ukiwa mmoja wao.
Hapana, si lazima uwe na kiasi hicho cha Mtaji, usitishike!
Mkuu board member wa kampuni huwa ni lazima wawe wataamu wa hio kazi ya kampuni?
Kwa mfano kampuni ya ujenzi ni lazima wawe mafundi au wahandasi?
 
Mkuu board member wa kampuni huwa ni lazima wawe wataamu wa hio kazi ya kampuni?
Kwa mfano kampuni ya ujenzi ni lazima wawe mafundi au wahandasi?
Ni lazima mmoja wao awe Engineer au Technician. Si lazima awe Board Member, anaweza kuwa mwajiriwa. Cha msingi lazima uwe na CV ya Mtaalam
 
Wadau wa JF ,naomba mnisaidie ni hatua gani za kufata kuweza kusajili na kumiliki kampuni ya mikopo ,pia ni gharama kiasi gani zinahitajika mpaka kukamilisha kabisa usajili wake .....
kwanza utatakiwa kuwa na jina la biashara au kampuni ambayo mwisho lazima iwe na finacial services,microfinance,micro credit na vitu kama hivyo.
2. uwe na kielelezo cha mtaji wako ambao sio wa mkopo usiopungua milioni 20.
3. Utaenda BOT Kanda uliyopo utapewa formu yenye mahitaji muhumu kama kuandaa sera ya ukopeshaji nk.
4. ukikamilisha hatua ndipo utaruhusiwa kuandika barua ya maombi BoT YA KUOMBA LESENI. lESENI YA BOT NI 500,000. kwa Huduma za usajili wa kampuni,Majina ya biashara, kufuatilia leseni unaweza wasiliana nasi kwa info@shabfinance.co.tz tunapatikana Arusha barabara ya ARUSHA - NAMANGA.
 
Back
Top Bottom