Kampuni ya Kiwi Shoe Polish Mjitafakari

Kampuni ya Kiwi Shoe Polish Mjitafakari

uko sahihi,

in fact hata ile ya KIWI ya maji, kile kisponchi kinachomoka haraka na mapema mno wakati rangi bado ni nyingi kwenye chupa,
na kulazimika kutumia labda kitambaa kung'arisha kiatu, kitu ambacho matokeo yake ni kujifua mikono na kila mahali matone ya rangi yanapodondokea ,

nadhani ni muhimu kubadilika na kuongeza ubora na uimara wa vifungashio hivyo :NoGodNo:
Kweli mkuu , watupe vitu ambavyo tutatumia tukifurahia matumizi yake
 
Ni kweli. Kiwi changamoto yake kubwa ni kwenye hiyo kitu ya kufungulia, mara nyingi siyo imara. Inakàtika au chomoka na kuleta usumbufu wakati wa kufungua mkebe. Wanatakiwa waboreshe hapo.
Yaan hako kakitu kakikatika 🤣 asee kuna na ile situation ya kujigawa vipande vipande
 
Tuko mwaka 2026 jamani, lakini Kiwi shoe polish bado manatuuzia makopo yanayofunguliwa kama vile ni mtihani wa mwisho! 😂

Simu zimekuwa smart, magari yanajiendesha yenyewe, AI inafanya vitu vya ajabu… lakini huo mkebe wenu kufungua ni kama unafanya mtihani wa practical
Kwanini Kiwi msijaribu mbinu mpya wateja wenu wakubwa ni wanafunzi au ni kwamba hii mikebe mlitengeneza hadi 2030.

Yaan hako Kakitu kakivunjika ndo kipengele kinaanza 🤣 ni either ugonge huo mkebe chini unaanza na kiwi iliyomwagika baada ya hapo utakua unatumia vipande vipande

Labda the manufacturer wanted to maintain originality, security, patience and 'carefulness in one product ila sasa hapana

Niko nabrushia watoto hapa waende kanisani
muwe na Dominika njema 🤣 Utani wa Jumapili
View attachment 3622821
Mbona zipo kopo za kufungua mfuniko? Hiyo uliyonunua ni ya bei rahisi. Nenda supermarket utazikuta za kisasa. Na hazigandi.
 
Hapo ni sawa sawa useme kampuni ya Michelin ijitafakari tumechoka matairi ya rubber sasa tunataka matairi ya chuma sababu zama zimebadirika barabara ni za zege na chuma inatembea juu ya zege
Wao wamebadilika fikiria kutoka Tairi za kujaza upepo mpaka Tubeless sio kitu kidogo mkuu 🤣 ila kiwi hapana
 
Oooh sawa mkuu, huku kwetu naona ni mtihani kupata vitu vizuri

Hamwezi pata vitu vizuri huko uswahilini. Zipo Kiwi kwenye kikopo kama cha mafuta na katika hali ya umate mate. Halafu kuna zile za kwenye kichupa mbele kina sponge, halafu kuna za ku spray. But hizo tunanunua supermarkets hasa za Obay, M.City.Mikocheni.

Huwezi zikuta Mchambawima, Makunduchi, Bwegeni, Mnyamani, Tandale kwa Tumbo, Yombo Vituko, Temeke kwa mfuga mbwa, Keko n.k huwezi zikuta huko.
 
Jamaa wana heshima yangu kwa wakati wote 🙏
 
Back
Top Bottom