Kampuni ya Ardhi Plan yapigwa marufuku kupima viwanja nchini kwa sababu za udanganyifu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Sakata la Mgogoro baina ya kampuni ya uuzaji viwanja ya Reding Farm ltd na Kampuni ya upimaji viwanja ya Ardhi Plan Ltd zilizopo wilayani Arumeru, limechukua sura mpya kufuatia kampuni ya Reding kudai kuwa kampuni ya Ardhi Plan ilishapigwa marufuku na serikali kufanya shughuli ya ipimaji viwanja hapa nchini.

Akiongea na waandishi wa habari wakati akijibu tuhuma zilizoibuliwa na kampuni ya Ardhi Plan kupitia Mkurugenzi wake,Gombo Simandito kuwa kampuni ya Reding Farm ltd kwa kushirikiana na halmashauri ya Arusha wamegushi hati ya viwanja na kujipatia kiasi cha sh,milioni 30.

Wakili wa kampuni ya Reding Farm ltd,Goodluck Peter alikanusha tuhuma hizo akidai kwamba zinalenga kuichafua halmashauri ya Arusha na kuingilia uhuru wa mahakama kwani shauri la mgogoro huo lipo ngazi ya mahakama ya rufaa .

Alisema Gombo ameamua kuingia mlango wa nyuma na kufungua kesi nyingine mahakama ya Mwanzo jijini Arusha ,alimtujumu afisa Ardhi mteule wa halmashauri ya Arusha dc,kuwa ameghushi hati ya viwanja vyake viwili na kujipatia kiasi cha sh,miliomi 30 jambo ambalo si kweli .

Alisema kesi hiyo ni chokochoko dhidi wa mteja wake( kampuni ya Reding Farm ltd),ili aweze kufunguliwa milango ya kuuza viwanja 103 vilivyozuiwa na mahakama ya rufaa hadi kesi ya rufaa itakaposikilizwa.

Akifafanua mgogoro unaoendelea baina ya mteja wake na kampuni ya Ardhi plan ltd, wakili Peter alidai kuwa kampuni ya Ardhi Plan ilifungua kesi ya madai mahakama kuu kanda ya Arusha,ikitaka ilipwe kiasi cha shilingi bilioni 2 baada ya mteja wake kampuni ya Reding Farm kukiuka makubaliano ya upimaji wa viwanja.

"Mahakama kuu ilitoa uamuzi kuwa Reding farm ltd ilipe kiasi cha sh,bilioni 1.3 kwa kampuni ya Ardhi Plan ltd kutokana na kukiuka mkataba wa makubaliano, hata hivyo mteja wangu aliamua kukata rufaa mahakama ya rufani kupinga hukumu hiyo"alisema

Alisema pamoja na mteja wake kukata aliamua kutoa dhamana ya viwanja 103 vyenye thamani ya sh,bilioni 1.3 iliyoamuriwa na mahakama ili aendelee na mchakato wa kuuza viwanja vingine zaidi ya 300 alivyokuwa navyo.

Pamoja na kwamba viwanja 103 vilitolewa dhamana ya thamani hiyo ,kampuni ya Reding Farm ltd ilipinga uamuzi wa mahakama kuu na kuweka zuio la viwanja hivyo hadi shauri hilo lisikilizwe mahakama ya rufani.

Alisema hatua hiyo ilimkasirisha Gombo na kuamua kufungua kesi mahakama ya Mwanzo, Maromboso akimshtaki afisa Ardhi mteule wa halmashauri ya Arusha alidai ameghushi hati ya viwanja vyake viwili na kuviuza.

"Hii ni chuki dhidi ya halmashauri baada ya afisa ardhi kukataa kutoa hati ya viwanja hivyo kwa kuwa mahakama imesimamisha uendelezaji hadi shauri la rufaa likamilike"

"Kwa sasa tunashangaa kuona Gombo akifungua kesi ndogo ndogo akisumbua watu wa halmadhauri na hii ni kutaka afunguliwe milango ya kuuza viwanja vilivyozuiwa kuuzwa na mahakama ya rufaa"alisema.

Aliongeza kuwa kampuni ya, Ardhi Plan Ltd ilishazuiwa kujishughulisha na upimaji wa viwanja wilayani humo na hapa nchini kutokana na ukiukaji wa utaratibu kwa kupima na kuuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja na kusababisha migogoro isiyoisha kwa wananchi.
..

20220406_154754.jpg
20220406_152349.jpg
 
Nchi ngumu sana hii, huyo Gombo alishawahi kuwa Mkurugenzi wa halmashauri, sarakasi zote za halmashauri anazijuwa, hawamuwezi.
 
Prince Ritz1 atakuwa anahusika katika hii hujuma. Kwasababu anataka asilimia 88% ya viwanja nchini amiliki jinsi sheli zote ziko chini yake.
 
Back
Top Bottom