Kampuni ya Apple yaiba features kutoka Android, Google na Microsoft

Kampuni ya Apple yaiba features kutoka Android, Google na Microsoft

Atlantis

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2015
Posts
383
Reaction score
514
Kampuni kubwa ya vifaa vya kielektroniki duniani Apple, inasemekana imeiba mawazo ya wapinzani wake kama Samsung, Google na Microsoft ili kufanya maboresho katika software platforms za bidhaa zao kama iPhone na Tablets.

==============================

Kampuni ya Apple Yaiba Mawazo 6 ya Washindani Wake
2.jpg

Kampuni kubwa ya vifaa vya kielektroniki duniani Apple, inasemekana imeiba mawazo ya wapinzani wake kama Samsung, Google na Microsoft ili kufanya maboresho katika software platforms za bidhaa zao kama iPhone na Tablets.

Ni dhaihiri kwa baadhi ya wapenzi sugu wa bidhaa za Apple features hizo zitaonekana kama mawazo mampya toka Apple lakini kwa wazoefu na watumiaji wengine wanaweza kufahamu fika kabisa kwamba si kitu kipya!

Features hizo zimekuwa updated na Apple ni katika matoleo mapya kabisa ya iOS, OS X, watchOS na Apple Music.
Features hizo ni kama zifuatazo:

1) Public Transit Information (toka Google)

Iko wazi kuwa Google Maps ndiyo Software ya kwanza kabisa duniani katika masuala ya ramani (hata kwenye semu za Apple zenyewe kuanzia I-phone 5 kushuka chini). Moja wapo ya sababu ni kwamba Google inatoa live public transit information.

Jumatatu iliyopita, Apple ilitangaza kuwa itafanya maboresho katika Apple Maps ambayo imekuwa na matatizo kwa muda mrefu sasa. katika maboresho hayo itaweka feature mpya ambayo ni Eureka – ambayo na yenyewe itakuwa inatoa live public transit information. Feature ambayo imeiiba kutoka Google Maps.
zl7jrwwdh8jyqspodhsrt2pstrk.png

Apple Maps (kushoto) and Google Maps (kulia).2) Multi-Tasking Tablets (toka Microsoft Surface)
cg80vyrecdzpaimkdd9pi_orrxa.png

Microsoft Surface (juu) na iPad yenye iOS 9

(chini).iPad zilizo na mfumo wa kuongoza wa iOS 9 zinamuwezesha mtumiaji wa kifaa hicho kuweza kfungua applications mbili kwa wakati mmoja yaani multi-tasking zimepokelewa kwa shangwe na wadau mbalimbali wa msuala ya teknolojia.

wazo hili kwanza lilibuniwa na Microssoft kwenye mfumo wao wa kuongoza kompyuta wa wa Windows 8 na kwa kitambo kirefu sana!

Hata hivyo, feature hii itaboreshwa zaidi katika Windows 10, ambapo mtumiaji wa kifaa chochote kinachotumia mfumo huu ataweza kubadilisha ukubwa wa muonekano wa application iliyofunguliwa katika screen yake.

3) Picture-in-picture video (Kutoka Samsung Galaxy Note).

nnn.png

Samsung Galaxy Note II (kushoto) na iPad yenye iOS 9 (kulia).

Apple pia imejibosti kwa feature yake nyingine mpya ya picture-in-picture kwa kifaa chake cha iPad Jumatatu hii. Ni nzuri lakini ukweli ni kwamba feature hii ilishakuwepo katika simu za Samsung Galaxy Note na tablets kwa muda mrefu sasa.

Kwa upande mwingine, feature hii katika Android inamuwezesha mtumiaji kucheza video files za kawaida na si kutumia applications za TV za moja kwa moja yaani live. Kitu ambacho katika Apple wameboresha na kufanya iwezekane katika bidhaa zao.

4) Contextual searches (Google Now on Tap)

hh1.png

Now on Tap ya Android (kushoto) na Siri kwenye iOS 9 (kulia).

Wiki mbili tu zilizopita, Google ilizindua feature mpya iitwayo Google Now, kama Siri mpya, toleo hili jipya la Android voice assistant inaweza kupitia barua-pepe zako au jumbe fupi za maneno na hata kufanya makumbusho au reminders za matukio ambazo za kalenda ambazo mtumiaji mwenyewe anaziweka.

Na huduma hizi mbili za Apple na Google zinaweza kufanya uchambuzi wa mazingira kwa amri za sauti yaani voice commands.

Hii inamaanisha kuwa, wakati unaperuzi tovuti yenye habari kuhusu mlima Kilimanjaro, mtumiaji unaweza kuuliza "Itanichukua muda gani mpaka kileleni?" na itakupa jibu sahihi kwa maneno. Ndo mambo ya Artificial Intelligence hayo!

5. Smarter watch faces (Kutoka Android Wear)
hhhh.png

Navigation kwenye Apple Watch (kushoto) na navigation on Android Wear (kulia).

Apple imekuwa ikizindua watchOS kuongeza mambo kama vile uwezo wa kubadili muonekano wa uso wa saa hii kulingana na matakwa ya mtumiaji (custom photo watch faces) na navigation kulingana na uelekeo wa mtumiaji (turn-by-turn navigation), lakini features hizi zilikuwepo katika Android kwa kitambo sasa.

6) Apple Music (Kutoka Beats Music)

hhhh1.png

Beats Music (kushoto) naApple Music (kulia).

Ingawa Apple ilinunua Kampuni hii ya Beats Music kwa $3 bilioni, imeweza kuchukua vitu vingi kutoka kwake. Muonekano wake na navigation nzima imefanana kabisa na aplication hiyo.

Chanzo: wordpress
 
Sio kila news ukisearch google huwa ni reliable mzee, umekula maharage ya wapi mzee?
dah kaka si unajua mie ndo nagusa kompyuta leo, sijazoea mambo yenu haya:iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::A S 103::A S 103:
 
hakuna cha ajabu hapo, wanaibiana idea kila siku kwa hiyo ni kawaida... unasahau apple ndo wa kwanza kuja na smartphone na app store android wakaiba, wataibiana mwisho wa siku chagua kinachokufaa tu
 
usiseme sio kweli huku hujatoa ukweli unaoujua

Smartphone zilikuwepo before iOS kuja, ever heard of Symbian Os, Windows Mobile na Blackberry Os.. Sema tu apple ilikuwa kampuni ya kwanza kutengeneza smartphone ya kwanza yenye "Capacitive" touch screen in 2007.
 
usiseme sio kweli huku hujatoa ukweli unaoujua

In early 2000, the Ericsson R380 was released by Ericsson Mobile Communications, and was the first device marketed as a "smartphone".
It combined the functions of a mobile phone and a PDA, supported limited web browsing with a resistive touchscreen utilizing a stylus .

In early 2001, Palm, Inc. introduced the Kyocera 6035 , which combined a PDA with a mobile phone and operated on Verizon . It also supported limited web browsing.

Smartphone before Android, iOS and BlackBerry, typically ran on Symbian , which was originally developed by Psion. It was the world's most widely used smartphone operating system until the last quarter of 2010.

Smartphone - Wikipedia, the free encyclopedia

Ndivyo Wikipedia inavyoniambia.
 
hio transit si kweli nokia na here maps wanafanya siku nyingi tu na zamani google alikua anategemea navteq kupewa map data ambayo navteq ikaja ikawa nokia map.
 
In early 2000, the Ericsson R380 was released by Ericsson Mobile Communications, and was the first device marketed as a "smartphone".
It combined the functions of a mobile phone and a PDA, supported limited web browsing with a resistive touchscreen utilizing a stylus .

In early 2001, Palm, Inc. introduced the Kyocera 6035 , which combined a PDA with a mobile phone and operated on Verizon . It also supported limited web browsing.

Smartphone before Android, iOS and BlackBerry, typically ran on Symbian , which was originally developed by Psion. It was the world's most widely used smartphone operating system until the last quarter of 2010.

Smartphone - Wikipedia, the free encyclopedia

Ndivyo Wikipedia inavyoniambia.

baba wa smartphone(feature wise) ni nokia communicator japo wakati zinatoka neno smartphone lilikuwa halijaanza kutumika. ina kila kitu cha smartphone ya kisasa

1.kioo chenye resolution kubwa (ilikuwa na wvga)
2. software za office kama word na excel
3. simu ya kwanza duniani kuwa na browser
4. full qwerty keyboard nk

no9110_00.jpg

ilikuwa ni mwaka 1996 kipindi hiko hata simu za rangi bado, then baadae siemens akaja kutoa simu ya kwanza yenye kioo cha rangi then ikaja symbian kwenye erricson. kutokea symbian ndo zikatoka communicator za kisasa zaidi

phpThumb.php
 
Duh..nami nimetumia hzo mkuu,.
 
Wikipedia ni most reliable source of info lakini huwa siyo yakuipa 100% of truth concerning habari zao zote, ila ingefaa sana Chief unipe source ya hiyo ishu.

at first lengo lilikuwa nikupinga tu kwamba sio apple walioanza kuleta smartphone, na nna uhakika kwamba jibu kamili la hili swala halitoweza patikana.
 
wamarekani wanapenda sana kubend history, apple alilipishwa fine dola milioni 600 na kila iphone, ipod na ipad inayouzwa apple anamlipa nokia dola 6 hadi 8 sababu ios ni copy and paste ya meego, apple ameiba touch technology toka nokia na tokea 2004/2005 maemo ilikuwa ina exist na ni os ya touch.

na hii ndio ilikua quote ya bloomberg kwenye hio kesi
“Our understanding is that the dispute was never really about Nokia’s essential patents,” such as those relating to GSM and 3G wireless technologies, Sarkamies said. “Rather they were used to arm-wrestle a solution on non-essential patents such as touchscreen user interface innovations.”

tukija kwenye communicator even wikipedia wameandika kuwa features zake zimekuja ku evolve na kwenye smartphones
Nokia 9000 Communicator - Wikipedia, the free encyclopedia

hizi source nyengine
https://medium.com/people-gadgets/the-gadget-we-miss-the-nokia-9000-communicator-ef8e8c7047ae
The evolution of the smartphone | Pocketnow

japo kuna watu wanasema ibm simon ndio first smartphone wengine wanapinga(mimi nikiwa mmoja wao) sababu ilikuwa haina browser. hivyo kama ilikuwa huna browser, hutumi email huwezi jidownloadia vitu vyako haiwezi kuwa smartphone.

kuna website moja nzuri sana inaitwa gsmhistory ni official website ya gsm jamaa wana rare documents za simu ambazo unaweza usizipate popote kwa dunia yetu hii iliotawaliwa na media za magharibi. tembelea hii page itakusaidia kuijua historia ya simu.

Vintage Mobiles | GSM History: History of GSM, Mobile Networks, Vintage Mobiles
 
GSM nao wanakubaliana kwamba Simon ilikuwa ndiyo the first smartphone.
angalia hapa The world’s first smartphone is now two decades old - GSMArena.com news

walitoa habari yenye heading kwamba Simon ni the first smartphone ikiwa inasheherekea miaka 20

japo kuna watu wanasema ibm simon ndio first smartphone wengine wanapinga(mimi nikiwa mmoja wao) sababu ilikuwa haina browser. hivyo kama ilikuwa huna browser, hutumi email huwezi jidownloadia vitu vyako haiwezi kuwa smartphone.

Huu ni uongo, mana Wikipedia wenyewe ulionipa hiyo link wanadai ulikuwa unaweza kutuma email, jaribu kuwa unazisoma vizuri link zako ambazo huwa unazitoa, hii itakusaidia sana.

Wikipedia - Iaddition to its ability to make and receive cellular phone calls, Simon was also able to send and receive faxes , e-mails and cellular pages . Simon featured many applications including an address book, calendar, appointment scheduler, calculator, world time clock, electronic note pad, handwritten annotations and standard and predictive stylus input screen keyboards.

kuna website moja nzuri sana inaitwa gsmhistory ni official website ya gsm jamaa wana rare documents za simu ambazo unaweza usizipate popote kwa dunia yetu hii iliotawaliwa na media za magharibi. tembelea hii page itakusaidia kuijua historia ya simu.

Vintage Mobiles | GSM History: History of GSM, Mobile Networks, Vintage Mobiles

GSMhistory na Arena wana uhusiano, kwahiyo nivip watoe habari kwamba first word smartphone inatimiza miaka 20 ? ambayo ni simon unayoipinga hapa.
 
Nyie ongeeniii Ila mpaka mwisho baba Apple yupo pale alipoamka wako ndo wanalala
 
baba wa smartphone(feature wise) ni nokia communicator japo wakati zinatoka neno smartphone lilikuwa halijaanza kutumika. ina kila kitu cha smartphone ya kisasa

1.kioo chenye resolution kubwa (ilikuwa na wvga)
2. software za office kama word na excel
3. simu ya kwanza duniani kuwa na browser
4. full qwerty keyboard nk

no9110_00.jpg

ilikuwa ni mwaka 1996 kipindi hiko hata simu za rangi bado, then baadae siemens akaja kutoa simu ya kwanza yenye kioo cha rangi then ikaja symbian kwenye erricson. kutokea symbian ndo zikatoka communicator za kisasa zaidi

phpThumb.php
Nokia kuua OS ya Symbian walaamiwe sana, mpaka sasa hakuna phone OS niliyoikubali kama Symbian OS
 
Back
Top Bottom