Kampuni ya Afromark inavyowawazungusha malipo warembo

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Salaam wakuu. Hii kampuni ni kubwa, inaitwa Afromark Communication (T) Ltd. Miongoni mwa shughuli zake ni kusimamia mauzo ya vinywaji, zikiwemo bia kwenye baa mbalimbali.

Shughuli yao hii huifanya na warembo ambao huvaa sare. Lakini wapo warembo wanaidai hii kampuni toka mwaka jana, Desemba mpaka Machii hii. Kila siku kiswahili. Mara tutatuma. Hawatumi! Mara tukituma jina litatokea nani? Wakitajiwa jina, bado hawatumi!

Hii mimi naiona siyo sawasawa hata kidogo. Kazi yenyewe ya kuingia saa 10 jioni kutoka saa 6 usiku!!! Halafu malipo kiswahili!!!
 
Sio vizuri kulimbikiza malipo. Ukimfanyia mtu kazi usisubiri malipo yajikusanye sana. Baada ya muda ili ulipwe 'Kibatala' itabidi ahusike
 
Back
Top Bottom