Kampuni nzuri ya fridge

Jstar1

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
1,389
1,337
Anaejua kampuni nzuri ya fridge, kuanzia matumizi ya umeme, kelele, na muda wa kudumu, hapa naomba kujua ubora wa fridge za Westpoint, LG na Samsung, ila hasa hasa Westpoint zipoje, kelele na matumizi ya umeme, na kampuni nzuri ya TV.
 
Hapa kwetu tunatumia mtungi ili kupoza maji ya kunywa, na nyama tuna chemsha kisha tunaweka chumvi na tunazianika ili kuzitunza kwa muda mrefu, maharage tuna chemsha kwa kuni kila mara tu tunapo hitaji kula kama mboga ya wali, na kwakuwa tunaishi karibu na ziwa hata samaki hakuna sababu ya kununuwa kwa wingi Bali tu pindi tunapo hitaji kula hiyo.

Na kila weekend tunakwenda mjini, hivyo basi hatupati tabu ya Ice cream, chocks tick na lambalamba pale dukani kwa mwarabu.

Huku kwetu hatu tumii majokofu, ila tu nakupongeza kwa kufikia maendeleo ya kumiliki kipozeo.
 
Jstar1, Kampuni nzuri ya fridge ni BEKO from Turky, wapo vizuri kwenye kelele, ulaji wa umeme na kugandisha.
Mkuu ni kweli kabisa hata mimi ninalo la mtumba mara ya kwanza kuleta geto nilizani ni bovu maana sauti haisikiki mpaka ulisogelee karibu ndo utasikia kwa mbaali

Wapo vizuri sana hawa jamaa
 
Fridge za kichina kama Solstar, westpoint (za kichina), aborder, singsung, pintec n.k hazifai hata kidogo. Najuta hadi leo.

Kwa kuwa Lg, Sharp, Samsung original ni ghali. Nakushauri uchukue Beko ya uturuki. Hii inakula umeme kidogo, imara na inatunza sana baridi.
 
kuanzia ubora, kuharibika, matumizi ya umeme, gas na tahadhari nyingine, pamoja na bei halisi
1573021326206.png
 
Hizo Singsung na za kichina nyinginezo zinakula umeme balaa, hasa vile vifupi
 
1. West Point
2. BEKO
3. Singsung
4. Sharp
5. LG
6. Whirlpool
7. Nk
Inawezekana kabisa hizo friji zote ziko vizuri ingawa zinaweza kupishana kidogo sana. Tatizo kubwa ni kupata kama ni Westpoint basi ni kuipata ile yenyewe ya ukweli. Nakumbuka mwaka jana tulikuwa tunaenda kumnunulia dada mmoja zawadi ya Send Off ilibidi tumtafute jamaa mmoja ambaye ana duka la vifaa kama hivyo na kutembea naye madukani kutafuta the real West Point tukazikuta kwenye duka moja tukachukua lakini along the way tulikutana na Counterfeit nyingi. Na hiyo ipo kwenye bidhaa nyingi za aina hiyo kama Washing Machines, Generators, Waterpumps, Tvs, na kadhaalika. Ikiwezekana kama kuna mtu unamfahamu kwenye hiyo sector mpoze hata Tshs 30k akusaidie kutafuta the real one. Maana bei huwa hazitofautiani sana kwa sababu wanaouza Counterfeit wanaogopa wakishusha bei bidhaa zao zitajulikana sio real
 
kila mtu anavutia upande wake

we unataka fridge kweli??

Nenda dukani huko huko utakutana na Fridge.

sema acha namimi nkuvutie upande wangu

Tukilia tulie wengi..

Ukienda dukani nunua HITACHI
 
Back
Top Bottom