Kampuni ‘iliyomng’oa’ waziri Nundu yaibukia Bagamoyo

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,303
2,000
KAMPUNI ya China Merchant Holdings kutoka China, iliyoletwa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu ili iwekeze kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa gati mbili kwenye Bandari ya Dar es Salaam na Bandari mpya ya Mwambani, imeibuka tena.

Kampuni hiyo, ambayo ilikumbana na vikwazo vingi, inadaiwa kurejeshwa kiaina safari hii kama mwekezaji mpya kupitia Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji).

Awali kampuni hiyo iliyodaiwa kupigiwa chepuo na Nundu hadi kufikia hatua ya kutofautiana kwa kiasi kikubwa na menejimenti ya TPA, Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ilisababisha Nundu kupoteza nafasi yake ya uwaziri, kutokana na ‘kiwingu’ kilichoonekana kuwa kama Serikali ingekubali kuendelea na mwekezaji huyu kwa masharti aliyotaka, taifa lisingepata maslahi yoyote.

Mwekezaji huyo, alitaka ajenge kwa fedha zake na kuendesha mradi huo kwa miaka 43, kisha akabidhi bandari kwa TPA. Lakini itakumbukwa menejimenti ya TPA na bodi yake, walipendelea mradi huo ufanywe kwa mkopo, kutoka kwenye benki ya Exim ya China au kutoka kwa benki nyingine yoyote yenye masharti nafuu.

Benki ya Exim ya China, ilikubali kutoa mkopo na kupendekeza Kampuni ya China Construction Company (CCCC), ifanye upembuzi yakinifu, huku mkopo huo ungekuwa wa miaka 15, ikiwa ni pamoja na ‘grace period’ ya miaka mitatu kabla ya kuanza kulipa.

Ilidaiwa Nundu, alidai Kampuni ya CCCC ilipendekezwa na mkopeshaji Exim Benki, bila kushindanishwa.

“Cha kushangaza tumeona Waziri Nagu, akiueleza umma kuwa, kampuni ya China Merchant Holdings, inakuja kuwekeza kwenye ujenzi wa Bandari ya Mbegani..Bagamoyo bila kushindanishwa na kampuni nyingine yoyote na wala masharti ya uwekezaji huo hayajawekwa wazi,” kilisema chanzo chetu.

“Na kama ni Serikali inakopa kwa ajili ya mradi huu mkubwa ambao ni zaidi ya dola za Marekani bilioni 7, ni vema Waziri Nagu au waziri wa Uchukuzi, Dk. Mwakyembe akaliweka wazi zaidi.”

Habari za kuaminika zilizopatikana jana kutoka ndani ya Wizara ya Uchukuzi, zinasema tayari makubaliano ya awali yamefikiwa kwa Kampuni ya China Merchant Holdings, kwa ajili ya mradi huo. MTANZANIA ilimtafuta Waziri Nagu kupitia simu yake ya kiganjani, lakini iliita bila kupokelewa
 
Check-Mate

Member
Sep 27, 2012
10
20
Juzi nilsoma uzi humu jf kuhusu huu mradi na nilijua nimesoma vibaya nilipoona hiyo kampuni imepewa mradi wa bagamoyo. Lakini kama sikosei hii kampuni ilitaka kujenga hizo gati mbili kwa $250 million lakini TPA ilitaka kuchukua mkopo wa $500 million kutoka Exim bank.
 
monaco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,186
2,000
Jamani hebu watujuze zaidi,Hii kampuni mbona mkataba wake umefichwa sana,sana,kuna maswali kadhaa tunajiuliza

1.Ujenzi unatakiwa kuanza lini na Gharama kiasi gani?
2.je ni kweli unacover mbegani port,reli ya kati Dar mpaka Isaka Musongati Rwanda,pia na Tazara?
3.Tumesikia kutakuwa na kikosi kazi(Task force) kitatoa wapi hela?hazina? nini majukumu ya kikosi kazihicho?
4.Je wadau mf WB,AFDB Wameshirikishwa?au wanamchango wowote kimawazo ktk mradi mkubwa kama huo?
5.Waweke wazi that project,watangaze tenda,washindanishwe,hiyo china mechants wanatoa hela mfukoni au kuna harambee watafanya,coz siamini kama they will put out their money direct.
6.Malipo tutalipaje na muda gani?
 
Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,812
1,250

Bodi ya Tpa iliyovunjwa pamoja na management iliyosimamishwa iliweka priorities za uwekezaji kwenye bandari zetu kama ifuatavyo. 1.kujenga gati no 13 &14 za containers kutokana ongezeko kubwa la shehena ya container na nafasi bandarini kuwa finyu kitu kilichopelekea TRA kutoa licence kwa ICDS ( inland container depots) kusaidia kuhifadhi containers kama extension of the port.Priority nyingine ya haraka ni kujenga gati tatu Mtwara pamoja na kushauri serikali ijenge reli haraka toka Mtwara mpaka Mamma bay kutokana na makaa ya mawe huko Mchuchuma. Mtwara kwa sasa ni muhimu hasa kutokana na wingi wa gas uliopatikana.Priority ya mwisho ilikuwa ni kujenga bandari mpya Bagamoyo ambayo itakuwa kama bandari mbadala ( fall back position) baada ya bandari ya Dar na upanuzi wa hizo gati mbili za 13&14 kuzidiwa ikiwa ni pamoja na kutumika kwa matumizi ya mizigo mingine mbali na shehena ya containers.Priority nyingine ni kujenga bandari mpya ya Mwambani Tanga sababu ikiwa ni kukabiliana na ushindani wa kibiashara utakaokuwepo karibuni baada ya serikali ya Kenya kuanza kujenga bandari kubwa ya kisasa huko LAMU na tayari mkandarasi yuko site wakati sisi tuko kwenye michakato.
 
Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,464

Ni kweli!
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
5,491
2,000
Naamini kulikuwa na siri kubwa sana kati ya Jk na Nundu jk alivyoona linamchachia mwenziwe akamtosa du
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
9,910
2,000
Wenye moyo wanaijenga nchi,wenye meno wanaila nchi,na katibu mkuu wa chama tawala kesha sema haelewi A wala B ya matatizo ya watanzania na utatuzi wake,so is chairman,meno yanazidi kunolewa.
 
Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,412
2,000
Hii inji ukijua yanayoendelea unaweza kufa mapema sana. Ni heri wanakijiji wanaolala njaa na kutojua yanayosababisha wawe katika hali hiyo.
 
Bob

JF-Expert Member
Sep 10, 2007
286
225
Mambo ya Terminal 3, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Airport DSM ilikuwa hivi hivi!
Yangu macho.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Top Bottom