Kampeni za kujiandikisha na kuboresha daftari la wapiga kura: Kutakuwa na uchaguzi au ni yale yale ya serikali za mitaa?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana watu walihimizwa kwenda kujiorodhesha kwaajili ya uchaguzi huo. Baada ya kujiorodhesha kukatokea kituko cha karne ambapo wagombea wa upinzani zaidi ya asilimia 99 waliondolewa kwenye kinyang'anyiro na wale wa chama tawala kutangazwa kuwa washindi. Hivyo wapiga kura wakawa hawana kazi tena ya kuchagua kwakuwa wenye nguvu walishajichagua.

Sasa hivi tena kelele kama za mwaka jana zimeanza tena kuwa watu wakaboreshe na kujiandikisha kwa wale ambao hawana vitambulisho vya kupigia kura. Viongozi wa chama tawala wakiwamo katibu mkuu na makamu mwenyekiti wa chama tawala wametangaza kwamba chama chao kitwaa majimbo na kata zote na wembe watakao utumia ni ulele.

Sasa ndio najiuliza kama mipango imeshapangwa kuwa wao ndio washindi je kutakuwa na uchaguzi mkuu kweli au ni kuwachosha watu tu? Nchi haiishi vituko hii ukitilia maanani hata haki za vyama zilizofafanuliwa vizuri kwenye katiba na sheria za vyama zimezuiwa sasa itakuwa ajabu gani wakijitangaza washindi?

Kwa haya yaliyotokea uchaguzi uliopita wa 2015 na wa serikali za mitaa 2019 sioni kama uchaguzi huu utakuwa na hamasa yoyote na kama kweli utakuwa ni uchaguzi kweli kwa maana ya uchaguzi kwa sifa zake.
 
Tulimumu,
Mpige kura au msipige

Utangazaji wa matokeo kibabe upo pale pale.

NB. Wabunge wote lazima watatoka CCM iwe kwa ushindi halali au la
 
La Serikali za mitaa usipotoshe kila mwenye akili timamu alijua ni wapi mlipokosea. Ni halali kabisa ushindi uliopata CCM . Naamini uchaguzi huu mtakuwa makini kujaza fomu ili zisiwepo dosari za kuenguliwa
 
Back
Top Bottom