Kampeni ya Usafi wa Dar iendane na hili

ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,788
1,302
Niendelee kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa kusimamia maamuzi mbalimbali ya kuhakikisha Dar inasimama katika usafi na mpangilio wa biashara katika maeneo mengi.

Katika hili kuna haja ya kuhakikisha Dar inakuwa katika hali ya usafi na mpangilio wa biashara katika hili kuna haja ya kusimamia vizuri maeneo mengine ikiwemo wafanya biashara holela kwenye maeneo yasiyo rasmi.

Hii ikiwa ni pamoja na kupanga biashara maeneo ya barabara hasa wenye vibanda holela vya biashara, maduka ya vifaa vya ujenzi, wauza mbao, mafundi welding, fundi magari. nk. Ili Jiji la Dar likae kwa usafi kuna haja ya kuangalia na kuhakikisha kila kitu kinafanyika katka maeneo yaiyotengwa na kuondoa uholela.

Kongole kwa kazi nzuri.
 
Waanzishe pia kampeni za Vijana kupata ajira...Kampeni za Jamii kutumia bidhaa za nyumbani kuwaunga mkono Wajasiriamali wa nchini n.k.
 
Nitamsifia siku akifanikiwa kusafisha Kwamtogole pawe kama Magogoni
 
Niendelee kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa kusimamia maamuzi mbalimbali ya kuhakikisha Dar inasimama katika usafi na mpangilio wa biashara katika maeneo mengi.

Katika hili kuna haja ya kuhakikisha Dar inakuwa katika hali ya usafi na mpangilio wa biashara katika hili kuna haja ya kusimamia vizuri maeneo mengine ikiwemo wafanya biashara holela kwenye maeneo yasiyo rasmi.

Hii ikiwa ni pamoja na kupanga biashara maeneo ya barabara hasa wenye vibanda holela vya biashara, maduka ya vifaa vya ujenzi, wauza mbao, mafundi welding, fundi magari. nk. Ili Jiji la Dar likae kwa usafi kuna haja ya kuangalia na kuhakikisha kila kitu kinafanyika katka maeneo yaiyotengwa na kuondoa uholela.

Kongole kwa kazi nzuri.
Siamini kabisa kwenye hizi kampeni zinazoanzishwa na kiongozi mmoja akiondoka zinakwisha. Tunahitaji utaratibu wa kudumu wa kusimamia usafi na mambo mengine nchini.
 
Back
Top Bottom