Kampeni ya #HarassBuhariOutofLondon yamweka under house arrest Rais wa Nigeria kwenye Ubalozi wa Nchi hiyo Jijini London.

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Rais wa Nigeria Muhammad Buhari alienda Uingereza kupata matibabu lakini Wanaharakati wakiongozwa na Reno Omokri ambae anaishi Marekani wakafunga Safari mpaka London wakajumuika na Wananchi wengine wa Nigeria wa Uingereza kwenda kwenye Ubalozi wa Nigeria Jijini London ambapo Buhari alifikia hapo kuweka kambia hapo ili Buhari asitoke kwenda Hospital kutibiwa.

Madai yao ni kuwa inakuwaje Rais anaachaje Hospital za Nchini mwake na kuja kutibiwa Ughaibuni wakati Wananchi wake wakiugua wanatibiwa kwenye hospital hizo hizo. Kwa hiyo wanataka Buhari arudi akatibiwe kwenye hospital za nchini mwake,leo ni siku ya 5 Buhari ameshindwa kutoka nje ya Ubalozi wa Nigeria, Abuja House na kwenda Hospital kutibiwa.

Huyu ndio Reno Omokri kiongozi wa Waandamanaji.
FB_IMG_16177258358728967.jpg
FB_IMG_16177257575501412.jpg
FB_IMG_16177258274253165.jpg
FB_IMG_16177258639447996.jpg
 
Viongozi wa Afrika shida sana. Utajiri wote ule wa Nigeria wanashindwa kuwekeza kwenye hospitali za maana!! Wamzuie tu ikibidi afie humo ubalozini ili akili zikae sawa kwa wengine.
 
Huko London hamna 'FFU' ? Hao wanaoandamana wanastahili kipigo...(just kidding...).

Ila kiukweli Africa kuna maajabu sana, taifa kubwa na tajiri kama Nigeria kukosa hospital ya kisasa yenye uwezo wa kumtibu Rais ni aibu na fedheha.
 
Buhari namkubali sana. Anajitahidi halafu kinachomsaidia zaidi anaungwa mkono na Yoruba ambao wengi ni wakristo. Ila vichwa ngumu na wajuaji na janjajanja nyingi Igbo hawampendi Buhari hii ni kutokana na uhasama wa muda mrefu tangu enzi za Biafra na fulani.

Ukienda hata kijijini kwao Buhari utashangaa na kujiuliza huyu jamaa ni rais ama mkulima hajajilimbikizia mali kabisa.

Udini, ukabila na majimbo ndio inawagawanya wanigeria. Na Muingereza alicheza sana hapa divide and rule. Lakini hadi leo wengi wanashangaa kwanini waingereza na Mabeberu waliamua kuwaunga mkono na kuwa upande wa wa Hausa Fulani na makabila ya kaskazini ambao karibu wote ni Waislamu na kuwakataa wakristo wa kusini?
Unajua yanayoendelea kwasasa Nigeria hasa zidi ya Wakristo?
 
Viongozi wa Afrika shida sana. Utajiri wote ule wa Nigeria wanashindwa kuwekeza kwenye hospitali za maana!! Wamzuie tu ikibidi afie humo ubalozini ili akili zikae sawa kwa wengine.
Tizama mfano wa UAE. Nchi Jangwa mwanzo mwisho, Jua kali unaweza kukaa na sufuria barabarani ukapika sembe. Hakuna Demokrasia. Viongozi wamejilimbikizia mali na kujimilikisha visima vya mafuta kama mali yao, lakini itizame nchi ilivojengwa sasa, tizama huduma bora za kijamii zinavyotolewa, Tizama raia wake wanavokula bata. Unakuta mtu anakibanda chake cha kibedui katikati ya jangwa huku anafuga mbuzi lakini anamiliki Hilux ya maana (icho kibanda ndo nyumba yake anachamba jangwani huyo sio kwenye TOILET). Hukuti raia akifagia barabara bali ni wageni ndio wanafuta barabara na kuondoa taka.

Sasa Tizama na Afrika. Bara lina utajiri wa kila kona lakini umasikini nao upo kila chochoro. Hili Bara limelaaniwa kuwa na watu wajinga wengi!
 
Back
Top Bottom