Kampeni ya Cheyo kuongoza kamati Bungeni yaanza rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya Cheyo kuongoza kamati Bungeni yaanza rasmi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Feb 8, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Pamoja na Bw. Mapesa kueleweka kwa utendaji mbovu wa kutetea serikali ya kifisadi ya CCM na kuzima hoja za kimsingi alipokuwa mwenyekiti wa kamati za usimamizi wa mapesa yetu yanayohujumiwa na mafisadi wa CCM bado anaonekana ana shauku nene ya kuchaguliwa kuongoza Kamati nyingine kwa mgongo wa CCM ambao hawako tayari kugeuza kanuni ziendane na mahitaji ya wapigakura wa karne ya 21............................

  katika kipindi cha mpito cha mfumo wa vyama vingi chama tawala kilishiriki kuwachagulia wapinzani wenyeviti wa kamati ambazo hupaswa kuzisimamia..........hivyo ungelikitegemea

  mgogoro uliopo Bungeni ni kama wabunge wa CCM wanayo mamlaka ya kushiriki kupiga kura za kuchagua wenyevitebe vya kamati za kusimamia matumizi ya serikali kuu, serikali ya mitaa na mashirika ya umma......................kamati ambazo kwa mujibu wa kanuni zinapaswa zisimamiwe na upinzani...........

  CCM ikiongozwa na kanuni za mfumo wa chama kimoa imemtumia Spika Anne Makinda ambaye anakumbukwa kuwepo hata kwenye baraza la mawaziri la Nyerere...............................kuongoza katika kulipotosha Bunge ili likubaliane na kanuni ambazo zinawaruhusu wabunge wa chama tawala kushiriki katika chaguzi zinazohusu vyeo vya upinzani Bungeni.........................

  Lengo ni CCM kwa kutumia uwingi wao bungeni kuwachagulia mamluki kama Cheyo ili kupooza au ahata kuzima kabisa vuguvugu la mageuzi ya mfumo mzima wa uendeshaji wa taifa hili na kukwepa kukemea maovu hapa nchini.....................

  nguvu kubwa ambayo CCM wameitumia bungeni kurekebisha hizo kanuni lengo lake ni kuendelea na ufisadi na vyama haramu kiupinzani kama CUF ambayo sote tunajua ni CCM-B na UDP viendelee kukilinda.............................

  katika kampeni za kupata vyeo hivyo, Cheyo aliwaponda Chadema na kudaio uchaguzi ulikwisha na asiyekubali kushindwa siyo mshindani......................ikiashiria anaafiki Jk alichaguliwa bila ya zengwe jambo ambalo Chadema wanalipinga........

  Kamati zote huteuliwa na Spika lakini swali la kimsingi ni kuwa hivi Chadema watakuwaje chama rasmi cha upinzani Bungeni kwa kutokuwa na sauti ya kuchagua wenyevitebe wa kamati tajwa.............................na lipo swali jingine la kimsingi hivi Spika anatumia vigezo gani katika kuunda kamati hizo zinazopaswa kusimamiwa na upinzani.........kama haheshimu idadi halisi ya viti vya wabunge ili kuhakikisha wapinzani ndiyo wanakuwa ni wengi kwenye Kamati hizo ili wasije kuzidiwa nguvu na wabunge wa CCM ambao wanatoka chama tawala?

  Nionavyo Spika makinda hii kazi hataiweza kwa sababu ya malezi aliyoyapata ni ya mfumo wa chama kimoja na hivyo kakosa utashi wa kubadilika kwendana na mfumo wa vyama vingi.....................
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Cheyo is a fraud, cheyo is a political prostitute and a reckoned conman

  Siwaelewi wanamchagua kuwa mbunge wao wana akili gani
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Cheyo kaenda mbali zaidi kwa kumwambia Lissu shut your mouth. Kauli hii imewashangaza sana wageni toka bunge la Uingereza, na wao bila kujua kuwa Cheyo si mpinzani wakauliza kuwa hivi ndivyo wapinzani Tanzania wanavyojimaliza wenyewe? Kwa ukilaza wake wa lugha, Makinda naye, (nimemsikia asubuhi akisema hii iko very clearly) bila kujua kuwa waingereza walikuwa wanamshangaa Cheyo, akaliambia bunge kuwa wageni toka uingereza wameshangazwa na mwenendo wa CHADEMA.
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kweli mimi nimesikiaa jinc naibu spika alivyoelezea kuhusu wa bunge wa uingereza eti wameshangazwa na wabunge wa chadema kwa jinc wanavyojiiwakilisha kwa wananchi au ndivyo wanavyojichinja wenyewe kumbe ulikuwa ni mshangao wa cheyo kwa jinsi alivyokuwa anamfokea lisu nikazidi kushanga tena
   
 5. P

  Paul S.S Verified User

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Si lisu wala cheyo wote ni wapinzani wanao pinzana kwa cdm kudhani fikra sahihi ni za cdm tu, ukiwaza vinginevyo wewe chizi
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  machizi yanaendeleza uchizi hadi bungeni . Nitashangaa kama Cheyo sio mvuta majani
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Behind the scene kuna Genge la Wahuni walio kiteka CCM na kukiendesha kama nyumba ndogo.Pia wameliteka bunge na wabunge kwa nia ya kuendeleza uhuni ule ule waliotumia kukiteka CCM.Nia na madhumuni ya genge hili la kiibilisi ni kuwezesha tabaka lao la ELITE ALIEN kuitawala Tanzania milele.

  kuna njama za kuhujumu na kudhurumu utu wa Mtanzania.
  Binadamu mwenye akili timamu
  kwa nini aishii kama mnyama wa porini
  ambaye ishi yake,
  hutegemea ukali wa meno yake
  na urefu wa makucha yake
   
 8. e

  emrema JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM wana agenda gani na upinzani hata kulazimisha Chadema washirikiane na Tawi la CCM la CUF? Nadhani ni hatua nzuri ya KUSUSIA tena UFISADI wa CCM. CDM are right and keep it up. Nashauri CDM waisusie na nafasi hiyo ya kuongoza kambi ya upinzani wawe na kambi yao kivuli na iwe NEUTRAL kutetea wananchi tu.
   
 9. M

  Mndamba Namba 1 Senior Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CUF na vyama vingine vinavyounga mkono CCM hawaezi wakawa wapinzani coz tayari kuna familiarity threat,by that say no independence and objectivity CDM they are right, to be mpinzani you must be indendepent and free from any threat ni sawasawa na Auditor kwenda kufanya ukaguzi kwa kampuni ambayo ameshiriki kuandaa vitabu vyake vya fedha
   
 10. s

  smz JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halima Mdee alisema wazi: Kuwa mpinzani unatakiwa kuwa na ngozi ngumu, yaani ukomae kwenye hoja unyoiamini kuwa ni ya msingi. CDM are very right it is their right kuongoza hizo Kamati Nyeti.

  Huwezi kuaminin mpiganaji kama Hamad Rashid Mohamed kabadirika hivyo, hadi anatamka kuwa CDM wana issue za kitoto. Lakini kama alivyosema Tundu Lissu mtu halazimishwi ndoa na mtu asiyempenda, kwanza mtu mwenyewe keshaolewa tayari
   
 11. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndoa tamu mkuu kwa sasa ni mapenzi motomoto
   
 12. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Masuala ya Siasa ni vichekesho. Dhumuni la CUF liko wazi " Hatuwezi kumwachia shamba lote nguruwe (CCM) na sisi lazima tule"- Hamad Rashid.... Hivyo CUF wapo ili nao wale. CUF wamefanikiwa sana katika siasa zao kwa hilo. Mwafaka wa CUF na CCM ni mafanikio makubwa sana ya CUF kwa malengo yao na wameendelea kuutumia huo mwafaka ku influence CCM zaidi hadi katika BUnge na kufanya mabadiliko ya kanuni za Bunge. Mabadiliko hayo ni mafanikio makubwa sana kwa CUF. Ninawasifu CUF kwa mafanikio yao lakini kuendelea kupata influence kwenye chama kinachopoteza mvuto na imani kwa wananchi kama CCM kila siku ni mafanikio yenye njia pana ya kuelekea KUZIMU (Kupoteza imani kwa wananchi). CHADEMA wapo kwa ajiri ya ukombozi na mabadiliko ya wananchi. Nawashauri wabadili njia za mapambano yao. Waendelee kujenga imani za wananchi kwao. Watumie Bunge kujenga hoja hata kama zikikataliwa lakini baadae wazipeleke kwa wananchi na kuwaeleza umuhimu wa hoja zao. Wawe na mikutano mingi na wananchi. Ushindi upo kwa Chadema ila inabidi wawe na mtazamo mpana zaidi kwa wananchi.

  Cheyo anaeleweka alivyo mtu wa kutafuta ulaji, awezi na wala hana dhamira safi ya kupigania maisha bora ya Watanzania. CDM ingeanza kuandaa mtu wa kupambana nae huko Bariadi.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  CHADEMA watikisa Bunge
  • Wabunge CUF, NCCR, wapigiwa chapuo na CCM

  na Irene Mark, Dodoma


  [​IMG] KIKAO cha Bunge jana kiligeuka ukumbi wa mapambano na mabishano makali ya hoja baada ya Spika wa Bunge kuruhusu mjadala kuhusu tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
  Hatua hiyo ya spika kuruhusu mjadala huo iliyotokana na ombi la wabunge wawili, Hamad Rashid Mohamed (CUF) na David Kafulila (NCCR-Mageuzi) ilipokelewa kwa malalamiko makubwa na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
  Mjadala kuhusu suala hilo ulioanza asubuhi kwa wabunge kupigana vijembe, kuzomeana, kukejeliana na wakati mwingine kulazimishwa kufuta kauli zao ulihitimishwa na hatua ya wabunge wa CHADEMA kulazimika kutoka nje ya Bunge ili kupinga kushiriki katika mabadiliko hayo ya tafsiri.
  Wabunge hao wa CHADEMA wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, walitoka nje ya ukumbi muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha jioni.
  Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kufanya hivyo Novemba mwaka jana wakati walipoisusa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete.
  Kabla ya kutoka nje, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alilazimika kubadili uamuzi wake wa kutaka kumfanya Mbunge wa Viti Maalum Anna Abdallah kuwa ndiye mchangiaji wa mwisho wa hoja hiyo kutokana na ombi la muongozo wa spika lililotolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA).
  Akiomba mwongozo wa spika kwa mujibu wa kanuni ya 68 ya Bunge, Mnyika alimtaka Spika huyo kutoifunga hoja hiyo hadi hapo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, atakapopewa nafasi ya kuchangia hoja hiyo.
  "Mwongozo wa Spika… kuna taarifa za uhakika nimepata kwamba miongoni mwa wachangiaji wa hoja hii walioomba kuchangia lakini majina yao yamekatwa ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Sasa kwa mujibu wa Kanuni ya 68, hoja hii isifungwe hadi hapo kiongozi wa upinzani atakapopata nafasi ya kuchangia," alisema Mnyika.
  Spika aliridhia hoja ya Mnyika na Mbowe akasimama kuchangia mjadala akianza kueleza masikitiko yake na ya chama chake kutokana na hatua ya wabunge kuwalazimisha kuingia kwa nguvu katika ndoa wasiyoitaka.
  Mbowe alisema CHADEMA haiwezi kuingizwa kwenye ndoa wasiyoiridhia huku akifafanua kwamba maridhiano hayawezi kuchukua wiki moja au mbili na akawaonya wabunge wa CCM kutotumia wingi wao kupitisha kile alichokiita maovu.
  "Hatuwezi kuingizwa kwenye ndoa ambayo hatujaridhia. Napata hofu ya umoja wenu leo. Naamini kwamba maridhiano hayachukui wiki moja au mbili… leo mkitumia wingi wenu kufanya maamuzi mnafikiri mnajenga kumbe mnabomoa.
  "Tuache unafiki na kudanganyana, tatizo letu sio tafsiri kama mnavyotaka kuiaminisha dunia. Tatizo hapa ni dhana ya ushirika tunaoutaka… kuna mambo ya msingi ambayo tunayapigania na tutafanya hivyo ndani na nje ya Bunge.
  "Hatuna ugomvi na muafaka wa Zanzibar. Hatuna ugomvi na CUF, lakini tunatofautiana kimsimamo… Tunaamini kwamba siyo vizuri kubishana na kanuni, tunatakiwa kuziheshimu.
  "…Sitokubali kuongoza kambi ya upinzani kwa kulazimishwa. Huo ndiyo msimamo wa chama chetu," alisisitiza Mbowe kisha akasimama na kuwaongoza wabunge wote wa chama hicho kutoka nje kuwapisha wabunge wa vyama vingine kupitisha kanuni hiyo.
  Hata hivyo, wakati wabunge wa CHADEMA wakitoka nje wabunge waliobaki walisikika wakitoa maneno ya kejeli dhidi yao kama vile 'tumewazoea', 'weak politicians', 'waroho na wachoyo wa madaraka', 'wasichukue posho', 'wababaishaji', 'tulijua hilo', 'hawana pa kwenda' na maneno mengine.
  Akiwa nje ya ukumbi wa Bunge, Mbowe alisema kila wanapofanya maamuzi wanakuwa na taarifa za kuaminika hivyo hata uwepo wao ndani ya Bunge si bahati mbaya bali ni kuwakilisha wananchi.
  "Tunaliheshimu Bunge, tunawaheshimu wabunge, kanuni na watendaji wote wa Bunge lakini kamwe hatutowaheshimu kwa kuweka rehani haki zetu… tutalipigania hili ndani na nje ya Bunge," alisisitiza Mbowe.
  Hata baada ya kutoka nje ya Bunge, Naibu Spika Job Ndugai, aliwaongoza wabunge waliobaki kupitisha tafsiri ya kanuni husika huku akisema kwa CHADEMA kutoka nje si jambo la ajabu na wala mbingu haziwezi kushuka kwa ajili hiyo ambapo wabunge wa vyama vingine walikuwepo.
  Kwa mujibu wa Ndugai, hoja hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika na David Kafulila na Hamad Rashid wakitaka kuingizwa ndani ya kambi ya upinzani na kupinga kambi hiyo kuundwa na CHADEMA.
  Mchangiaji wa kwanza wa hoja hiyo kwa asubuhi ya jana alikuwa Kafulila ambaye alieleza kuwashangaa wabunge wenzake wa CHADEMA kwa uchoyo wa madaraka huku akisema hataaminika tena katika jamii.
  "Hivi ninyi mmeshinda kwa asilimia 20 mnakataa kushirikiana. Mngeshinda kwa asilimia 60 sijui ingekuaje! Mimi nadhani umoja wa kambi ya upinzani ni jambo muhimu. Tuache ubinafsi," alisema Kafulila aliyekuwa akishangiliwa na wabunge wa CCM, CUF na wa NCCR.
  Mchangia aliyefuata alikuwa ni Hamad Rashid (CUF), aliyesema suala la umoja wa kambi ya upinzani kushirikisha vyama vyote ni jambo jema, hivyo hakuna sababu ya wajumbe kukataa kupitisha ufafanuzi huo wa kanuni.
  Hata hivyo, mchangia huyu alilazimika kufuta kauli yake ya kuwataka wabunge waache kile alichokieleza kuwa ni mambo ya kitoto ya kuwanyoshea vidole wabunge wa Zanzibar kuwa wanaingia bungeni kwa kuchaguliwa kwa idadi ndogo ya kura.
  Alipotakiwa na kufuta kauli hiyo, Hamad alisema, "Mheshimiwa spika nafuta kauli hiyo, haya basi na tuache mambo ya kikubwa… hili la kusema mbunge kachaguliwa kwa idadi ndogo ya kura ni matusi. Zanzibar ni nchi kamili tuache dharau," alisisitiza Rashid ambaye katika Bunge lililopita alikuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
  Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), alikua miongoni mwa wabunge waliolazimika kukatisha mazungumzo yake kila mara kutokana na taarifa na miongozo ya Spika ambapo alilazimika naye kufuta kauli yake pale aliposema wabunge wa vyama vingine ni wanafiki.
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), alijikuta katika wakati mgumu pale alipokuwa akichangia baada ya wabunge wenzake (sio CHADEMA) kuomba muongozo wa spika kila wakati.
  "…Hao walioleta hoja waliandika barua wakiomba kugombea nafasi za uenyekiti wa kamati zile muhimu ndiyo maana leo tuko hapa, waseme ukweli.
  "Hapa hoja iliyopo ni uenyeviti wa kamati za kudumu hasa zile kamati zinazoongozwa na kambi ya upinzani… hatuwezi kukubali chama chenye mbunge mmoja kuwa mwenyekiti wa kamati kama PAC mathalani," alisema Tundu.
  Hatua hiyo ya Lissu ilisababisha Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP) kuingilia kati na kutoa maneno makali huku wabunge wengine wakisikika wakitoa kauli za miguno.
  "Nimeiongoza hiyo kamati kwa miaka mitano bila ya matatizo… shut up your mouth," alisikika Cheyo akimwambia Lissu.
  Alipopata muda wa kuchangia, Cheyo aliwataka wabunge wa CHADEMA kuwa wavumilivu na akawaasa kupunguza jazba kwa kuwa siasa si chuki bali ni ushindani wa hoja.
  "CHADEMA kuna watu wazuri sana lakini mkumbuke kuwa siasa siyo chuki hata kidogo… nawaombeni sana muwe wavumilivu. Hivi nani kasema mtu akitoka CCM akaenda CHADEMA ndo anakua mzuri?" alihoji Cheyo.
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  CHADEMA watikisa Bunge
  • Wabunge CUF, NCCR, wapigiwa chapuo na CCM

  na Irene Mark, Dodoma


  [​IMG] KIKAO cha Bunge jana kiligeuka ukumbi wa mapambano na mabishano makali ya hoja baada ya Spika wa Bunge kuruhusu mjadala kuhusu tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
  Hatua hiyo ya spika kuruhusu mjadala huo iliyotokana na ombi la wabunge wawili, Hamad Rashid Mohamed (CUF) na David Kafulila (NCCR-Mageuzi) ilipokelewa kwa malalamiko makubwa na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
  Mjadala kuhusu suala hilo ulioanza asubuhi kwa wabunge kupigana vijembe, kuzomeana, kukejeliana na wakati mwingine kulazimishwa kufuta kauli zao ulihitimishwa na hatua ya wabunge wa CHADEMA kulazimika kutoka nje ya Bunge ili kupinga kushiriki katika mabadiliko hayo ya tafsiri.
  Wabunge hao wa CHADEMA wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, walitoka nje ya ukumbi muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha jioni.
  Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kufanya hivyo Novemba mwaka jana wakati walipoisusa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete.
  Kabla ya kutoka nje, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alilazimika kubadili uamuzi wake wa kutaka kumfanya Mbunge wa Viti Maalum Anna Abdallah kuwa ndiye mchangiaji wa mwisho wa hoja hiyo kutokana na ombi la muongozo wa spika lililotolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA).
  Akiomba mwongozo wa spika kwa mujibu wa kanuni ya 68 ya Bunge, Mnyika alimtaka Spika huyo kutoifunga hoja hiyo hadi hapo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, atakapopewa nafasi ya kuchangia hoja hiyo.
  “Mwongozo wa Spika… kuna taarifa za uhakika nimepata kwamba miongoni mwa wachangiaji wa hoja hii walioomba kuchangia lakini majina yao yamekatwa ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Sasa kwa mujibu wa Kanuni ya 68, hoja hii isifungwe hadi hapo kiongozi wa upinzani atakapopata nafasi ya kuchangia,” alisema Mnyika.
  Spika aliridhia hoja ya Mnyika na Mbowe akasimama kuchangia mjadala akianza kueleza masikitiko yake na ya chama chake kutokana na hatua ya wabunge kuwalazimisha kuingia kwa nguvu katika ndoa wasiyoitaka.
  Mbowe alisema CHADEMA haiwezi kuingizwa kwenye ndoa wasiyoiridhia huku akifafanua kwamba maridhiano hayawezi kuchukua wiki moja au mbili na akawaonya wabunge wa CCM kutotumia wingi wao kupitisha kile alichokiita maovu.
  “Hatuwezi kuingizwa kwenye ndoa ambayo hatujaridhia. Napata hofu ya umoja wenu leo. Naamini kwamba maridhiano hayachukui wiki moja au mbili… leo mkitumia wingi wenu kufanya maamuzi mnafikiri mnajenga kumbe mnabomoa.
  “Tuache unafiki na kudanganyana, tatizo letu sio tafsiri kama mnavyotaka kuiaminisha dunia. Tatizo hapa ni dhana ya ushirika tunaoutaka… kuna mambo ya msingi ambayo tunayapigania na tutafanya hivyo ndani na nje ya Bunge.
  “Hatuna ugomvi na muafaka wa Zanzibar. Hatuna ugomvi na CUF, lakini tunatofautiana kimsimamo… Tunaamini kwamba siyo vizuri kubishana na kanuni, tunatakiwa kuziheshimu.
  “…Sitokubali kuongoza kambi ya upinzani kwa kulazimishwa. Huo ndiyo msimamo wa chama chetu,” alisisitiza Mbowe kisha akasimama na kuwaongoza wabunge wote wa chama hicho kutoka nje kuwapisha wabunge wa vyama vingine kupitisha kanuni hiyo.
  Hata hivyo, wakati wabunge wa CHADEMA wakitoka nje wabunge waliobaki walisikika wakitoa maneno ya kejeli dhidi yao kama vile ’tumewazoea’, ’weak politicians’, ’waroho na wachoyo wa madaraka’, ’wasichukue posho’, ’wababaishaji’, ’tulijua hilo’, ’hawana pa kwenda’ na maneno mengine.
  Akiwa nje ya ukumbi wa Bunge, Mbowe alisema kila wanapofanya maamuzi wanakuwa na taarifa za kuaminika hivyo hata uwepo wao ndani ya Bunge si bahati mbaya bali ni kuwakilisha wananchi.
  “Tunaliheshimu Bunge, tunawaheshimu wabunge, kanuni na watendaji wote wa Bunge lakini kamwe hatutowaheshimu kwa kuweka rehani haki zetu… tutalipigania hili ndani na nje ya Bunge,” alisisitiza Mbowe.
  Hata baada ya kutoka nje ya Bunge, Naibu Spika Job Ndugai, aliwaongoza wabunge waliobaki kupitisha tafsiri ya kanuni husika huku akisema kwa CHADEMA kutoka nje si jambo la ajabu na wala mbingu haziwezi kushuka kwa ajili hiyo ambapo wabunge wa vyama vingine walikuwepo.
  Kwa mujibu wa Ndugai, hoja hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika na David Kafulila na Hamad Rashid wakitaka kuingizwa ndani ya kambi ya upinzani na kupinga kambi hiyo kuundwa na CHADEMA.
  Mchangiaji wa kwanza wa hoja hiyo kwa asubuhi ya jana alikuwa Kafulila ambaye alieleza kuwashangaa wabunge wenzake wa CHADEMA kwa uchoyo wa madaraka huku akisema hataaminika tena katika jamii.
  “Hivi ninyi mmeshinda kwa asilimia 20 mnakataa kushirikiana. Mngeshinda kwa asilimia 60 sijui ingekuaje! Mimi nadhani umoja wa kambi ya upinzani ni jambo muhimu. Tuache ubinafsi,” alisema Kafulila aliyekuwa akishangiliwa na wabunge wa CCM, CUF na wa NCCR.
  Mchangia aliyefuata alikuwa ni Hamad Rashid (CUF), aliyesema suala la umoja wa kambi ya upinzani kushirikisha vyama vyote ni jambo jema, hivyo hakuna sababu ya wajumbe kukataa kupitisha ufafanuzi huo wa kanuni.
  Hata hivyo, mchangia huyu alilazimika kufuta kauli yake ya kuwataka wabunge waache kile alichokieleza kuwa ni mambo ya kitoto ya kuwanyoshea vidole wabunge wa Zanzibar kuwa wanaingia bungeni kwa kuchaguliwa kwa idadi ndogo ya kura.
  Alipotakiwa na kufuta kauli hiyo, Hamad alisema, “Mheshimiwa spika nafuta kauli hiyo, haya basi na tuache mambo ya kikubwa… hili la kusema mbunge kachaguliwa kwa idadi ndogo ya kura ni matusi. Zanzibar ni nchi kamili tuache dharau,” alisisitiza Rashid ambaye katika Bunge lililopita alikuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
  Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), alikua miongoni mwa wabunge waliolazimika kukatisha mazungumzo yake kila mara kutokana na taarifa na miongozo ya Spika ambapo alilazimika naye kufuta kauli yake pale aliposema wabunge wa vyama vingine ni wanafiki.
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), alijikuta katika wakati mgumu pale alipokuwa akichangia baada ya wabunge wenzake (sio CHADEMA) kuomba muongozo wa spika kila wakati.
  “…Hao walioleta hoja waliandika barua wakiomba kugombea nafasi za uenyekiti wa kamati zile muhimu ndiyo maana leo tuko hapa, waseme ukweli.
  “Hapa hoja iliyopo ni uenyeviti wa kamati za kudumu hasa zile kamati zinazoongozwa na kambi ya upinzani… hatuwezi kukubali chama chenye mbunge mmoja kuwa mwenyekiti wa kamati kama PAC mathalani,” alisema Tundu.
  Hatua hiyo ya Lissu ilisababisha Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP) kuingilia kati na kutoa maneno makali huku wabunge wengine wakisikika wakitoa kauli za miguno.
  “Nimeiongoza hiyo kamati kwa miaka mitano bila ya matatizo… shut up your mouth,” alisikika Cheyo akimwambia Lissu.
  Alipopata muda wa kuchangia, Cheyo aliwataka wabunge wa CHADEMA kuwa wavumilivu na akawaasa kupunguza jazba kwa kuwa siasa si chuki bali ni ushindani wa hoja.
  “CHADEMA kuna watu wazuri sana lakini mkumbuke kuwa siasa siyo chuki hata kidogo… nawaombeni sana muwe wavumilivu. Hivi nani kasema mtu akitoka CCM akaenda CHADEMA ndo anakua mzuri?” alihoji Cheyo.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CHADEMA watoka tena bungeni


  *Ni kupinga bunge kubadili kanuni kuwabana

  Na Kulwa Mzee, Dodoma

  KIONGOZI wa Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe jana aliwaongoza na wabunge wa chama hicho kutoka nje ya bunge kupinga
  kubadilishwa kwa kanuni iliyokuwa inakitambua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichofikisha asilimia 12.5 ya wabunge kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

  Wabunge hao waliamua kutoka bungeni mara baada ya mchango wa Bw. Mbowe kuhusu mjadala wa kubadili kanuni hiyo, ambayo mtoa hoja, Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, alisema ni Azimio la kutafsiri kanuni maneno 'Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni'.

  Katika mchango wake Bw. Mbowe alisema wamba hawatendewi
  haki, watakuwa wanafiki kama watashiriki katika utaratibu wa mwisho wa suala hilo.

  Bw. Mbowe alilazimika kuwa mchangiaji wa mwisho baada ya Mbunge wa ubungo, Bw. John Mnyika kuomba mwongozo wa spika, kwa kuwa mjadala ulikuwa unaelekea kumalizika bila Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kupewa nafasi, na hivyo kuomba mjadala uahirishwe, lakini Spika Anna Makinda aliamua kumpa nafasi.

  Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA, alisema hawawezi kuingizwa katika ndoa wasiyoiridhia kwa kuwa wananchi walioamua kutoa ridhaa kwa CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani ndio hao waliamua kila chama kipate kura zilizopatikana katika uchaguzi mkuu.

  "Hatuna ugomvi na chama chochote, tunatofautiana kwa misimamo, tuheshimu kanuni lakini kanuni ikiua msingi wa haki ni batili," alisema.

  Alisema kila chama kina haki, katika hilo hawakutendewa haki hivyo watakuwa wanafiki kama watashiriki katika utaratibu wa mwisho wa kubariki hilo. Baada ya kauli hiyo, wabunge wote wa chama hicho waliinuka na kutoka ndani ya ukumbi.

  Akizungumzia hilo Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda alisema katika hilo CHADEMA wamepitiwa, hawana uhalali wowote na kuongeza kwamba siasa ni kuvumiliana na kuwa wakweli.

  "Kutoka nje hiyo si tabia ya kibunge, wanatakiwa kuonesha wanaweza kutawala na kuongoza baadaye," alisema na kuhoji kwamba hali itakuwaje ambapo kila panapokuwa na hoja ya kubishania wanatoka nje kwani hiyo ndiyo kazi waliyotumwa na wananchi?

  Baada ya CHADEMA kutoka nje, Bunge lilipitisha hoja kwa sauti za ndiyoooo, kutoka kwa wabunge wa vyama vingine, hivyo Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni itaundwa na wabunge wote wa vyama vya upinzani.

  Mapema akichangua hoja hiyo, Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee (CHADEMA) aliwashtukia baadhi ya wabunge wa upinzani akisema sasa wamegeuka kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) B, baada ya muafaka wa Zanzibar kuonekana kuingizwa kinyemela kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mjadala huo ulihusu hoja ilizowasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafula (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Wawi, Bw. Ahmad Rashid (CUF) waliotaka neno 'Kambi Rasmi ya Upinzani' lifutwe kwenye Kanuni za Bunge za mwaka 2007 na wabunge wote wa upinzani waunde kambi ya upinzani badala ya chama chenye viti vingi bungeni.

  Kutokana na hoja hiyo, bunge liliwasilisha azimio la kutaka 'kutafsiri' kanuni hiyo na kufanya maneno 'Kambi Rasmi ya Upinzani yamaanishe wabunge wa vyama vyote, ambao si wa chama tawala.

  Kulingana na kanuni hizo, kambi Rasmi ilikuwa imaanisha wabunge wa chama ambacho kimefikisha asilimia 12.5 ya wabunmge wote, ambacho kwa bunge hili ni CHADEMA, bila kukilazimisha kuwajumuisha wapinzani wengine.

  Bi. Mdee alisema kwa mara ya kwanza wapinzani wanapigiwa makofi na wabunge wa CCM wakati wakiunga mkono hoja hiyo, hali aliyosema inaonesha wabunge wanajivisha viremba vya wawakilishi kama wapinzani, leo wanageuka CCM B.

  Alisema anachoona ni muafaka Zanzibar unataka kuletwa bungeni kinyumenyume kuzimisha nguvu ya CHADEMA kwani haiwezekani kuwaongoza watu wanaotofautiana kisera, lakini kwa kuwa wako wengi wanaopigia kura azimio la mabadiliko hayo litapita, ukweli utabaki pale ple.

  "Tunajua wenyeviti wa kamati kazi yao ni kupata ajenda za bunge, upepo huu wa ushirikiano na CCM tutakuta ajenda zinazoletwa ni zile za mtawala anazotaka," alisema.

  Akichangia mabadiliko hayo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), Bw. John Cheyo alisema lazima nchi itawalike kwa amani, hivyo kitu chochote kinachowasilishwa kwa ajili ya kufanya nchi isitawalike kwa kuwepo kwa migomo na mauaji lazima kikataliwe.

  Alisema Watanzania wanataka kambi ya upinzani yenye nguvu, kama kuna vipengele vya kudhoofisha hivyo vinakwenda kinyume na kanuni, aliwaomba CHADEMA kupunguza hasira watengeneze bunge litakalotegemewa na wananchi, wasiendeleze uadui.

  "Nanyi chama tawala mambo ya kura myaache, mtawale nchi, Rais Jakaya Kikwete tawala nchi baada ya miaka mitano wengine wapigiwe kura," alisema.

  Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tindu Lissu (CHADEMA) alisema waliowasilisha maombi hayo lengo lao kupata madaraka wakati Watanzania hawakuwapa nafasi katika vyama vyao.

  Alisema chama cha upinzani chenye viti vingi bungeni ndio chenye nafasi ya kushika nafasi za uenyekiti katika kamati za kusimamia fedha za umma, chama chenye kiti kimoja kupata nafasi hiyo ya ulinzi wa fedha za umma haiwezekani.

  "Hatuko tayari kuwa na ndoa na chama chenye ndoa na chama kingine ukivuka Bahari ya Hindi, sheria inaruhusu ndoa ya wake wengi lakini si ndoa ya wanaume wengi," alisem na kuongeza kwamba hawako tayari CHADEMA kuburutwa katika hoja hiyo ya mabadiliko.

  Bw. Kafulila akichangia alisema upinzani kutofautiana wenyewe kwa wenyewe ni jambo la aibu, wale wanaopinga mabadiliko hayo haoni sababu zaidi ya ubaguzi.

  "Tunashinda kwa asilimia 20 tunakataa mseto, tukipata asilimia 60 hali itakuwaje, ukipata kidogo uoneshe una busara ya kufanya kazi pamoja, kwa hali hiyo ukipewa kikubwa huwezi kuaminika," alisema.

  Naye Bw. Mohamed alisema kuna dhana kwamba kuna watu wanabebwa na CCM, hakuna anayebebwa na chama hicho kufanya mabidiliko pale panapoonekana kuna haja, ni jambo la kawaida, hizo tofauti za ubaguzi zinazojengwa si wanazotaka Watanzania kusikia.

  "Mkuki kwa nguruwe kumbe, CUF mbona hatukulalamika? Tushirikiane tumepata ridhaa kwa wananchi," alisema na kuunga mkono azimio hilo.

  [​IMG]


  10 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Baadhi ya wananchi hatujaelewa kwanini bunge limefanyia marekebisho ya hicho kifungu! Kwa mdomo wake spika makinda alisema haitawezekana kwa kile alichopendekeza kafulila na rashid (CUF) kuwa kuwe na kambi ndogo ya upinzani bungeni na kwamba CHADEMA wana haki ya kuunda kambi rasmi kwakuwa wamekidhi vigezo hivyo, sasa imekuwaje spika ukaruhusu hiyo haki itengeliwe? huoni unajichanganya mwenyewe badala ya kusema kuwa chadema wamepotoka kwa kutoka nje? either hujui kanuni mwenyewe au unaburuzwa au unapata shinikizo kutoka mahali vipi ufanye kazi zake ambapo hautofika kwa mpango huo mama bora angekuwepo SITTA hata kama hutopenda hilo tutalisema kwakuwa unaonekana kujichanganya na maneno yako na wewe usipoangalia utakuwa mwanzo wa vurugu usidhani tumelala wananchi tunaangalia na kusikiliza na kupima sie sio wa mwaka 47 mnatudanganya, huko misri na tunisia etc unadhani wananchi wana uroho wa madaraka wanavyoshinikiza watawala wao waondoke madarakani? Hapna, wamechoshwa na utendaji wa kubahatisha kama huu, naomba mtende haki na mwenye haki apewe haki yake na si kutumia wingi wengi kuwanyima haki watu wengine
  February 8, 2011 9:23 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Jamani chadema wapo sahihi CUF ana ndoa na ccm na ndio maana jana walipigiwa debe na wenzao ccm ili kuuyumbisha upinzani bungeni.

  wakae wakijua wananchi hatuungi mkono hatua ya ccm kutoa tafsiri tata kuwapa wenzao nafasi ya kuingia upinzani kama hatua ya kupunguza makaLI YA UPINZANI, WAKIWEMO KENGE KWENYE MSAFARA WA MAMBA AMBAO NI NCCR MAGEUZI,TLP,UDP wasio na mtazamo mpana wa nini watanzania tunataka.

  February 8, 2011 9:45 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Wakati kambi rasmi ya upinzani ilipopitishwa kwa vigezo vilivyowekwa, CUF walikuwa walifurahia kwa kuwa ndio walikuwa wengi, baada ya kushindwa kwa vigezo, huyohuyo aliyependekeza vigezo hivyo viwekwe anageuka na kutaka vigezo hivyo vivunjwe huoni kama nimvurugaji anayetaka madaraka. Chadema kaza buti msikubali kwani wanataka kuwadhoofisha.hata sisi wananchi tunaona hilo
  February 8, 2011 9:49 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... cuf inajifariji na wabunge wa zanzibar ambao ni wawakilishi wa watu 7000-10,000 kwenye jimbo hii ni aibu. ndio maana tunataka tuwa na serikali moja au tatu tumechoka na ubabaishaji huu wa muungano
  February 8, 2011 9:50 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Kafulila ana hoja ya Richmond anasubiri kuileta bungeni.CCM wameshampa rushwa.Kwa msingi huo atakaa kimya.Yaani atafyata mkia,jamani njaa hizi!!!!!
  February 8, 2011 10:10 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Chadema kaza buti! Ukiona kitu ccm wanashabikia ujue hapo kuna kitu. Na wanainchi wengine walivyo mambumbumbu yanawaponda chadema. Hivi kweli unategemea kambi ya upinzani ipi hapo wakati cuf na ccm wao lao ni moja, haya Mrema yeye ni ccm damu hilo siyo siri. Mzee mwenzangu cheyo, utakumbuka bunge liliopita ni kwanini ulivuliwa uwaziri kivuli baada ya kushabikia ccm. Yaani hakuna kambi ya upinzani zaidi ya chadema wengine ni wanafiki tu hakuna upinzani hapo. chadema kazaa butiiiiiiii tweeeeeeeeeeendeeeeeeeee!
  February 8, 2011 10:14 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... chadema wana hoja za ubinafsi, washirikiane na wenzao, wanaowaunga mkono chadema kwa hili wanalenga kugawa nchi, huu ni ubinafsi Mbowe aache tabia hii hivi akipewa nchi si atawapiga risasi watakaopinga serikali yake ?, niliwapenda chadema lakini sasa wananitia mashaka kwa hili.katika bunge la 2005 Cuf ndio ilikuwa na wabunge wengi wakati chadema walikuwa wachache sana, lakini kwa kuwa Cuf iliwathamani na uchache huo katika kambi la upinzani kazi ilikuwa nzuri wakati hoja nyingi za ufusadi zikiibuliwa.iweje leo chadema kwa kuwa wamepata wabunge wengi katika kambi la upinzani wawakatae wenzao kwa mwamvuli kuwa wako kwenye muafaka,hivi wana hofu gani?wakati wananchi ndio wenye uamuzi sasa wao wanataka kulazimisha mambo, huo ni ubabe na ubinafsi, chadema wanayo ajenda ya siri na kwa hali hii mjadala bungeni itawashinda na watawaboa wananchi kwa migomo yao kwani hadi sasa asimia yao ya kukabidhiwa nchi imeanza kushuka tena kwa sababu wananchi wanaona leo kura ikipigwa tena kura za chadema zitapungua tena kuliko wakatim wa uchaguzi mkuu, ninawaomba chadema wawe na busara kwa masuala ya kitaifa sio hivyo jamani mnataka kupita kiasi.
  February 8, 2011 11:07 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Mama Anne Makinda mtihani wako wa kwanza umefeli. Hapa ndipo wananchi wanapoona wazi kabisa kuwa ulipandikizwa na chama chako kwa maslahi zaidi ya chama na si kwa kile walichokisema ni fursa sawa kwa wananwake.

  Hamadi ndiye aliyeweka maneno Kambi rasmi ya upinzani wakati huo akitaka CUF wawe vinara. Leo hii Hamad huyu huyu analiondoa na kumkubalia. You are weak madam, tena umewadhalilisha sana wanawake wenzake. HUFAI ANNE! Uko kwenye kiti cha uspika kimaslahi ya chama zaidina si kwa maendeleo ya nchi.

  Ole wenu CCM, wananchi wa leo si wa miaka ile ya ujinga wa kikondoo. CHADEMA kina dira sahihi ya ukombozi. CUF mnadanganywa ili muwatumikie CCM daima. Mnafikiri ndoa ya visiwani na huku bara itakubalika? Mna ndoto za ndaria. Hamad wewe mwenyewe unakiri Zanzibar ni nchi kamili, sasa huku bara mnafuata nini?

  Wananchi tuamke, saa ya ukombozi ni sasa. Tukiunge CHADEMA mkono - MAANDAMANO NCHI NZIMA TUFIKISHE UJUMBE KWA JK!!!!

  February 8, 2011 11:18 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... nisaidien jaman eti hivi chadema ni chama tawala au ni chama cha upinzani kwenye bunge la jamhuri ya muungano? kuna mbunge yeyote wa CUF kateuliwa na JK kuwa waziri? hii inanfanya nikumbuke maneno ya mtikila kuhusu serikali ya tanganyika
  February 8, 2011 11:33 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... we **** kabisa
  February 8, 2011 11:34 PM
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Ni vita ya Chadema, CUF bungeni
  Tuesday, 08 February 2011 21:10
  Comments

  123  +1 #37 Beano 2011-02-09 10:34 Hivi nani aliwaambia kwamba CUF ni chama cha upinzani? Hizi [NENO BAYA][NENO BAYA] za kambi ya upinzani ni kazi ya CCM kupitia mamluki wao waliobatizwa jina la upinzani. Jaribuni kukumbuka maneno ya yule mzee Chipaka wa chama fulani kidogodogo wkt wa kampeni akihojiwa na star tv, hapo utaona tuna shida na hawa ndugu zetu wanaoishi kwa kutegemea siasa hususan wakati unapokuwa umewaendea.
  Quote

  0 #36 mswahili safi 2011-02-09 10:16 WaBongo, ili tufike kwanza. hebu tupange STATICS zetu. kweli wasomi wengi TZA. wanapofikia suala la vyama vya upinzani hukumbwa na maneno mabaya /[NENO BAYA]/ vunja heshima/ tuhuma za wizi....! hayo makaribisho ya namna hiyo ni njia moja ya kuto washirikisha wenye uwezo wa kuongoza chombo cha siasa kwa jamii. mfumo huu ndiyo una sababisha kuelekea kwenye ukumbi wa DINI au Chama chenye Kabila. Ubaguzi huu tuumalize na tuufute kwanza ndipo tuta weza kupiga hatua kubwa ya maendeleo. CHADEMA ina weza kupanda kwenye utawala haraka, pindi tu watakapo chakachua mambo fulani madogo na kuweza kunyakua upendo wa wananchi mbalimbali hiyo ni wazi CHADEMA ijue kwanza? Wapinzani wengine nao wajue kupangusa(POLIS H) mikono yao kuwapokea wananchi kitaaluma ili wadumu kiuhakika na sera za wazi zenye masililahi ya nchi hii. CCM hapo ina weka marekebisho na kuikita vizuri isipoteze Dira na mwongozo wa utawala. Kweli hapo ndipo tutaona na kupata matunda ya ARDHI hii ya TANZANIA panapo tija ya kuwajibika na kuheshimu haki za wananchi kwa usawa.......Poleni kama nimewagusiya msiyo yapenda. NAFASI humu nchini bado ipo kubwa mtaenea wote..!
  Quote

  +1 #35 albert 2011-02-09 10:13 Malumbano ya nini bungeni.Tunawaomba sana sasa siyo wakati wa kampen za kutafuta kura tunataka kuona maendeleo yenu.Sisi wote ni watanzania ujue wakati unapokuwa bungeni watanzania wote wanakusikiliza yale unayoongea na siyo kwenda kujisifu.ama kushambuliana vyama vyote vipewe haki na siyo kupendeleo.Bungeni ni mahali pa kila mbunge kutoa maoni yake ya sehemu anayewakilisha wananchi wake walio mchagua,sasa kama vyama vingine vitakuwa havina uwezo wa kutoa maoni yao bungeni hakuna maana ya yule mbunge kuwa bungeni.Tunawaomba sana wabunge watanzania wanataka kuona maendeleo yenu,vita, malumbano,hatut aki bungeni,wale wanaotaka waende kwenye uwanja wa mapambano siyo bungeni.mnawakatisha tamaa watanzania waliowapa kura.Ni wakati wa mapambano ya kupambana na kuleta maendeleo ya katiba mpya.SAWA. SAWA.
  Quote

  +1 #34 waiti 2011-02-09 10:11 Quoting Mwaniiii P/ Mwana P.:
  Quoting Chitaka:
  Hamna kitu kipya CHADEMA. Kama ni kutoka tumewazoea Mtakuwa mnatoka then mnarudi.

  Tulia kijana mwenzangu tunataka kiona Tanzania inaepukana na ubadhirifu wa mali ya uma, mimi nawunga mkono CHADEMA, CUF ni mamluki kama ulikuwa hujui, wanajiita wapinzan... wanatekeleza maauzi ya wapinzani wao..... umeshawahi kuona wapi hiiiii, MUDA WA KUCHEZEANA AKILI UMESHAPITA WE NEED CHANGES, AND INDEED VISIBLE CHANGES, YOU HAVE TO CHANGE YOUR DIRECTION, OTHERWIZ YOU ARE LOSTTTTTTTTTTTT TTT
  We dogo kweli umefungwa speed governor ya ubongo...
  HeHeHee!
  unashangilia wanaokutia majeraha? Du! au mwenzetu kuna mgao unaomegewa?

  Quote

  +1 #33 waiti 2011-02-09 10:06 Wanangu eeee,nimegundua ! hakuna Wapinzani wa kweli hapa tanzania,vyama vyote nivibaraka vya chama cha jangwani:
  Mpinzani ni CHADEMA tu,.....
  Fikirieni kwa makini ndugu zangu tunaibiwa hivi hiiiivi kiusaniii,wakij a kwetu wanajifanya wanalia na kudondosha machozi wakiondoka....
  Mtanzania mwenzangu fuatilia BUNGE uone utumbo unaofanywa na hao wawakilishi wetu ndipo uamue.

  Na ninyi DOMO WANSI, oh! sory ninyi mnaosimamia umeme, msikate basi umeme ili angalau tuone one kabunge ketu kataarabu....

  Quote

  +1 #32 margareth 2011-02-09 09:52 yaani huyu aliyesema tununue mziki ni kiziwi kabisa hajaissikia bendi ikipigwa, hata Arusha? hiyo ndo bendi subirini. Alima lisu munyika tunawatazama kwa jicho la tofauti watanzani mnadizevu kuwa bungeni. kwanza mna akili pili mnazitumia akili zenu. tuko pamoja wananchi.
  Quote

  +1 #31 Pastor D. Mkenda 2011-02-09 09:46 Mimi nafikiri Vyama vya Upinzani walipopeleka hoja hiyo Bungeni ndipo walipochanganya mambo kwani walipeleka mahaliambapo ni upande mmoja wa upinzani ungeumizwa tu, na ndio imetokea hivyo. Nashauri kama kweli lengo sio maslahi binafsi ni kwa nini wasikae wenyewe kuanzia ngazi ya wenyeviti wa Kitaifa hadi kufikia mwafaka? Hapa naona wamepeleka mambo yao ya ndani barabarani ambapo hata mtu ambaye hakustahili kuyajua ameyajua.
  Quote

  +1 #30 john 2011-02-09 09:39 Jamani hebu 2angalie ki2 kimoja hapa hawa chadema wameanza kuwakana wenzao bungeni na kutaka kuunda kambi yao kivyao je lengo lao na nini?mm nilifikiria ili wapate nguvu wangewashawi wenzao wa upinzani wawe ki2 kimoja sasa kama wameanza malumbano mm sipati picha itakuaje mbele ya safari ina2bidi watanzania 2we makini,kama lengo ni kuleta maendeleo kwani taratibu c zipo?mbunge wa upinzani anapoenda kinyume dhabu c zipo?kwani mbona cheyo walimtoa kipindi kile?waliona ccm waliingilia kati?zisiwe wanatafuta sababu za ku2peleka ndiko siko?
  Quote

  -1 #29 george 2011-02-09 09:38 ila sikujua tanzania hii kuna vijana wa[NENO BAYA] kiasi hicho afadhali mwannii umepata akili sasa.usiwe mvivu wa kufikiri kama chitaka na wasiwasi kama anaweza kuimudu familia huyu.hii nchi si swala la chama ni swala la maslahi ya taifa .hivi haya yote hiki chama cha washenzi kimefanyia watu hawaoni au wamekula limbwata.umree hakuna ila dowans inalipwa.wamechukua pesa BOT no one caught guilt.wamenunua rada feki hakuna aliyekamatwa na huyu raisi kama si [NENO BAYA] ni na mashaka naye una jeshi mahakama unaogopaje watu wachache kisa wana pesa aaah nipeni hii nchi ndani ya masaa matatu kitaeleweka ushenzi wote utakwisha.
  Quote

  -1 #28 george 2011-02-09 09:31 chitaka unajua we nimshenzi wa adabu nini CCM WANAKUPA WEWE mama sikutofautishi na mwanamke anayegombana na mumewe akilazimisha mambo fulani ndani ya nyumba.
  Quote

  -1 #27 george 2011-02-09 09:28 wewe mwannii acha u[NENO BAYA]i unachokiongea unajua?kama hujui hii nchi imefika wapi huwezi support CCM hata kwa chembe ni ushenzi mtupu unaoendelea hapa.kutoka kwa chadema nje ni message tosha kuuonyesha ulimwengu kuwa tanzania inawashenzi kama wewe usiyejua unaloongea.nyamaza kuongea u[NENO BAYA]
  Quote

  0 #26 Sheria na uhuru 2011-02-09 09:16 So What...?
  SASA tumeanza upya SUALI la wazi.
  Kwani adui wa rafiki yangu ni adui wangu?????
  Politics siyo hivyo wandugu....!
  CHADEMA ni chama cha Democrasia na Maendeleo...hivyo tuzingatie democrasia na freedom na tujiendeleze kitaifa na nchi hii iwe na Maendeleo, vipi tena tuna rudi kinyamela nyuma na kutangaza uzembe na vita visivyo kuwa na maana awa grounds. hii ni TEST (mitihani wa pili )katika chama hiki. Kweli hatujifunzi SIASA. Chuki zenu ni wazi- funika ubaya wako.

  Quote

  -1 #25 Frank 2011-02-09 09:12 Clement S. umegusa suala ambalo hakika linaonyesha ni namna gani CCM na CUF ni kitu moja, wala si mchanganyiko wachai ya rangi na sumu, ni sumu mbili zimechanganywa kuwa sumu kuu. Hawakuona ni busara kushikisha vyama vingine kwenye muafaka Zanzibar, muafaka ni wao wawili tu! Linapokuja na huku bara nchi tunayosherekeag a uhuru kila 9 Disemba hata bila kuwaenzi walopigania uhuru kwa kupandisha bendera ya Tanganyika, CUF wanataka kushikishwa. Hivi CUF waliwashirikish a CHADEMA kwenye kambi yao ya upinzani bunge lililopita? Nini mbaya nyie CUF? La muujiza ni hili la Kafulila, kijana udandia mtumbwi ulotoboka,kuzam a ni lazima si kubahatisha wala kutabiri.
  Quote

  0 #24 GZZLE4SURE AJAJA 2011-02-09 09:09 CHADEMA TUNAWASHUKURUNI SANA;MDEE TUMEKUTUMA KIUKELI, CHAPA KAZI USIOGOPE CCM WALA CCM B
  Quote

  0 #23 Mwaniiii P/ Mwana P. 2011-02-09 09:08 WeeeeWEeeeeee unaakili sanaaaaa, walishaolewa, then wanataka kuolewa, duuuuuuuuuuuuuu uuuu, CCM wameangalia point of weakness kwa CUF wakapigilia ile kitu inatwaaaaa...........wakalegea
  Quote  123
  Refresh comments list
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Chadema wachafua hali ya hewa bungeni
  Tuesday, 08 February 2011 21:29

  [​IMG]Exuper Kachenje, Dodoma na Sadick Mtulya, Dar
  WABUNGE wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe jana walichafua hali ya hewa bungeni pale walipotoka tena nje ya Ukumbi ya Bunge kupinga azimio la kuondoa utata wa tafsiri ya Kanuni ya Bunge inayotoa fursa kwa chama chenye asilimia 12.5 ya wabunge wote kuunda kambi rasmi ya upinzani.

  Tukio hilo linalofanana na lile la Novemba 18, mwaka jana, Rais Kikwete alipozindua Bunge lilifanywa na Chadema baada ya Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro kuchangia mjadala wa huo akiwa mchangiaji wa mwisho.

  "Madamu Bunge limeona busara kuleta hoja hii, na vijembe vile, kwa masikitiko nasema hatutashiriki kumalizia hoja hii, naomba kutoa hoja," alimalizia maelezo yake Mbowe na kuanza kutoka nje akifuatiwa na wabunge wa chama hicho.

  Hata hivyo, wakati wabunge hao wa Chadema wakitoka nje, wabunge waliobaki wengi wakiwa wa chama tawala CCM, walisikika wakitoa maneno ya kebehi dhidi ya wabunge wa Chadema.

  "Tumewazoea kukimbia, kwisha, uchoyo, weak politicians, na kwenye posho msije, mnadaiwa na mabenki,"walisikika wabunge wakisema kwa kupiga kelele.

  Awali Mbowe akichangia mjadala huo alisema kuwa ushirika ni jambo la msingi, lakini katika Bunge la Kumi kuna tofauti za msingi.

  "Bunge la Kumi kuna tofauti za msingi, haki ya kila chama haiondolewi kwa dhana za juu juu. Kuchagua mshirika ni haki yetu kikatiba na hatuwezi kulazimishwa ndoa, tumeona vijembe vilivyotokea leo tutawezaje kuwa na kambi moja?. Tunahitaji muda zaidi" alisema Mbowe na kuongeza:

  "Ni vigumu ukalazimishwa uchumba na mtu hivyo hivyo hatuwezi kulazimishwa katika ushirikiano,'' alisema na kuongeza: " Hakuna trust(uaminifu) katika ushirika huu.''

  Aliongeza: "Viongozi wa vyama kushirikiana ni vizuri, tupeane muda, maridhiano hayawezi kuwa ndani ya wiki moja au mbili. Uamuzi wenu unabomoa, kwani hapa tatizo si tafsiri bali dhana ya ushirika tunaotaka bungeni. Yapo ya msingi, lakini si kutulazimisha kuingia katika jambo ambalo hatujaridhia."

  Mbowe alisema tofauti zilizopo zinazungumzika huku akionya kuwa wingi usitumiwe kugandamiza Chadema na kwamba kanuni zisitumiwe kuua msingi wa haki ambapo pia alieleza kuwa chama chake hakitakubali hilo na ndiyo dhamira ya Chadema.

  Wakati wakitoka kwenye ukumbi huo, majira ya saa 11:30 jioni wabunge wengine wa CCM, TLP, NCCR-Mageuzi, UDP na CUF walioonekana kushikwa butwaa kwa kitendo hicho.


  Mkutano na Waandishi wa Habari

  Baada ya kutoka nje, Mbowe alizungumza na wanahabari, mkutano ambao ulirushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Star (Star TV).

  Katika mkutano huo, Mbowe alisema wataendelea kupinga vitendo vyote vinavyovunja Kanuni za Bunge kwa maslahi ya Bunge na Taifa.

  "Hatutawaheshimu kamwe wabunge 'wanaocompromise' haki zao (wanaokubali haki zao kudhulumiwa), na tutaendelea kupinga kilichotokea leo, ndani na nje ya Bunge," alisema Mbowe.
  Hata hivyo, baada ya kumalizika na kupitishwa marekebisho hayo ya kile kilichoelezwa kuwa kuondoa utata wa tafsiri katika kanuni ya 14 hadi 16 ya Bunge, wabunge hao wa Chadema walirudi ndani ya Ukumbi wa Bunge na kuzua tena maneno ya chini chini kutoka kwa wabunge.

  Kwa kupitishwa mabadiliko hayo na kwa mujibu wa kanuni ya 15(2) tafsiri ya Kambi Rasmi ya upinzani bungeni ni kambi inayoundwa na vyama vya upinzani vinavyowakilishwa bungeni.

  Hata hivyo, bado Chadema kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ndicho kitakachotoa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni na naibu wake. Pia kiongozi huyo ana mamlaka na uhuru wa kuteua Baraza la Mawaziri Kivuli kutokana na wabunge wa upinzani waliopo.

  Hata hivyo, azimio hilo linaondoa dhana iliyokuwepo kwamba Chadema ndicho kingetoa wenyeviti wa Kamati za Hesabu za Serikali ambazo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge zinatakiwa kuongozwa na wapinzani.

  Tofauti na ilivyokuwa ikifahamika awali, mabadiliko ya jana yanatoa fursa kwa mbunge yeyote wa upinzani kugombea nafasi hizo bila kuhitaji idhini ya uongozi wa kambi ya upinzani.

  Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaiona hatua hiyo kuwa ni kuwanyima Chadema nafasi ya kuongoza kamati hizo, kwani kwa kuzingatia uhusiano wake mbaya na CCM ni dhahiri nafasi za wenyeviti zitakwenda kwa vyama vya CUF, NCCR – Mageuzi , TLP au UDP ambavyo wabunge wake walikuwa wakiunga mkono azimio la kuingizwa kwa tafsiri hiyo katika Kanuni za Bunge.


  Spika Anne Makinda
  Kabla ya kuhitimishwa kwa hoja hiyo iliyopigiwa kura na kupitishwa, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema kuwa:
  "Katika hoja hii, Chadema haikuwa na ukweli, wananchi wajue hili. Wenzetu wamepitiwa. Kitendo kilichotokea hapa si utaratibu mzuri, watawaambia nini wananchi?."

  Spika alionekana kukerwa na kitendo hicho cha Chadema na kuhoji iwapo kweli wabunge hao wapo kwa ajili ya maslahi ya umma au maslahi yao wenyewe.

  Hata hivyo, mkutano wa Bunge uliendelea kwa Naibu Spika, Job Ndugai kufafanua baadhi ya vipengele vinavyohalalisha uwepo wa kambi ya upinzani bungeni.

  Kwa pamoja wabunge waliobaki walipitisha azimio la kuwepo kwa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

  Vijembe vya Mrema na Lusinde
  Mbunge wa Jimbo la Vunjo(TLP), Augustine Mrema pamoja na Livingstone Lusinde wa Jimbo la Mtera (CCM) waliwapiga vijembe Chadema wakati wakichangia hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Novemba 18 mwaka jana alipokuwa akizindua rasmi Bunge la Kumi.

  Mrema aliwapiga vijembe Chadema akisema alistahili kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kutokana na uzoefu pamoja na sifa alizonazo.

  "Nimekuwa mbunge mara tatu kwa vyama vitatu tofauti, nimekuwa naibu waziri mkuu, nikakamata kontena la dhahabu, niliweza kupambana na ufisadi hivyo nilistahili kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani," alisema Mrema.

  Naye Lusinde alikwenda mbali na kusema kutokana na viongozi kuonekana kuchoshwa na amani iliyopo, alipendekeza wabunge wapigane bungeni ili wajue uchungu wa kupoteza amani.

  "Nafikiri kuliko kuwashawishi kwanza wananchi wavunje amani kwanza ningependa kuona siku moja bungeni humu wabunge tukizichapa ili tujue uchungu wa kupoteza na si tu kuwashawishi wananchi halafu sisi viongozi hatudhuriki na tunajipatia sifa za bure,'' alisema Lusinde
   
 18. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... bahati mbaya sana kwa destiny ya nchi yetu TUMEFIKA HAPA licha ya kuanza vyema kwa rekodi za miafrika. Bahati NZURI upuuzi wote huu unatokea zama hizi au katika nyakati za HATUDANGANYIKI.

  Ndio, katika BUNGE la hii MIAFRIKA, wamo hata wale ambao siku za usoni watakuja na hoja ifuatayo:
  ... napendekeza kuanzia sasa marais wote waitwe ma-JK. Yaani huyu wa sasa ndo JMK1 akufuatiwa na wa 2015 kama JK2. Sintoshangaa kichaa mtoa hoja ya namna hiyo akashangiliwa vilivyo baada ya Bunge kutumia muda wake wote kujadili upupu kama huo, sambamba na template ya upupu unaoendelea sasa.

  Kiroja cha jana kule mjengoni kinanikumbushia mengi yanayaoandikwa humu. Sasa kina Sofi fyatu wamo kibao mle ndani. Kazi kwelikweli.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wakazi wa Bariadi hawaitaki CCM, hivyo tangu vyama vingi walikuwa na msimamo wa kuiondoa CCM kwani kabla mh John Momose Cheyo hajaingia kwenye siasa walikuwa wakikiunga mkono CUF chini ya Mapalala lakini baada ya Cheyo kuingia na Mapalala kupotea walihamia UDP naweza kusema ni kati ya majimbo ambayo CCM wameshindwa kuya rudisha tangu 1995, kwani kama ni rushwa itumika sana 1995 tena waziwazi mlikuwa mkikutwa mko zaidi ya watu 4 mna pewa siyo chini ya 20,000 kipindi hicho ilikuwa pesa nyingi sana watu wakawa wanajipanga kwenye center ili Paul Ngwani akipita awape pesa lakini baada ya matokeo ya 1995 CCM ikala mweleka, ingawa walijaribu kuiba kura kipindi furani baada ya alikuwa mbunge kupitia UDP (Daniel Makanga) kuhamia CCM hivyo vita ikawa makanga na Cheyo, kura zikapigwa wakachakachua mpaka cheyo alitomfano alienda yeye, mke wake na mama ya cheyo kupiga kura kwenye kitu kimoja wapo lakini cha ajabu cheyo alipata kura mbili tu kitu hicho kilimshitua akajiuliza je ni mke wake hakumpigia kura au mama yake je inawezekana!?, wakarichukua kwa miaka takiribani 2 lakini baada ya hapo limerudi UDP, Bariadi kuna maendeleo sana na nimafanikio ya Cheyo, na ndiyo maana wamepewa kuwa ndiyo makao makuu ya Mkoa mpya Simiu badala ya maswa ambako ndiko chimbuko la bariadi....wakazi wa Bariadi kwasasa wengi wanaiunga mkono CDM kutoka na UDP kukosa mwelekeo lakini bado wana tambua kazi nzuri ya bwana Mapesa.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Kafulila, Hamad waipiga vijembe Chadema
  Wednesday, 09 February 2011 22:08

  [​IMG]Hamad Rashid

  Mwandishi Wetu, Dodoma

  MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR) na Hamad Rashid wa Wawi(CUF) jana waliipiga vijembe Chadema wakieleza kuwa matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge yameonyesha chama hicho kutokuwa wakweli.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi wa wenyeviti hao jana, wabunge hao walisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha nia njema waliyokuwa nayo kwa kutaka marekebisho ya tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani katika kanuni za Bunge.
  "Labda niseme kwa ufupi, matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge nimeyapokea vizuri hasa kamati zile tatu zinazoitwa 'Watch Dog' ambazo hushikwa na wapinzani," alisema Kafulila.

  Vita ya maneno baina ya CUF na NCCR Mageuzi kwa upande mmoja dhidi ya Chadema kwa upande mwingine ilionekana dhahiri kuhamia bungeni kufuatia Chadema kuonyesha msimamo wa kutotaka ushirika na vyama vingine kwenye kambi yake ya upinzani, baada ya wabunge wa vyama hivyo kupeana mipasho katika kikao cha kwanza cha mkutano wa bunge la kumi unaoendelea mjini Dodoma.

  Hoja hiyo juzi ilifanya mkutano wa bunge la kumi kuanza kwa moto pale Naibu Spika, Job Ndugai alipowasilisha azimio linalotoa tafsiri ya nini maana ya ‘Kambi rasmi ya upinzani Bungeni' na baadaye azimio hilo kupitishwa na bunge hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni mkakati wa "kuivunja nguvu za kisheria Chadema".

  Jana Kafulila alisema juzi wakati wa mjadala wa azimio la Bunge kuhusu marekebisho ya tafsiri ya kanuni ya Bunge kuhusu maneno Kambi Rasmi ya Upinzani, wabunge wa Chadema walionyesha kuwa yeye Kafulila na Hamad Rashid walitaka nafasi za uenyekiti wa kamati hizo.

  Alisema tofauti na mawazo hayo ya Chadema, matokeo yamekuwa tofauti na kuchukuliwa na Chadema yenyewe, UDP na TLP akiongeza kuwa hiyo ni salamu kwa Chadema. Alifafanua kuwa kwa matokeo hayo Chadema inapaswa kufahamu kuwa wao walitaka mabadiliko hayo kwa faida ya wabunge wote na si vyama vya NCCR na CUF kama Chadema walivyodhani.

  "Hiyo ni salamu kwa Chadema, wajue kwamba sisi tulitaka mabadiliko kwa ajili na faida ya vyama vyote, umeona hata nafasi hizo zimekwenda kwa vyama vya UPD, TLP na Chadema yenyewe," alisema Kafulila. Hamad Rashid kwa upande wake alisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yamemfurahisha na kwamba yametokana na kazi waliyoifanya juzi kurekebisha kanuni za Bunge na kuwezesha Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP kuchaguliwa uenyeviti wa kamati.

  "Nimefurahi kazi yetu ya jana (juzi) imesaidia Mrema na Cheyo wamepata uenyekiti wa kamati zinazotakiwa kuongozwa na wabunge wa upinzani," alisema Hamad. Aliongeza:" Kelele zetu zilikuwa kuweka msingi ya demokrasia ambayo imetendeka, lakini dhana walizokuwa nazo wenzetu Chadema hazikuwa sahihi.

  Kilichofanyika ni demokrasia." Alisema kuwa kimsingi kila mbunge alishiriki uchaguzi huo na kwamba waliochaguliwa wamechaguliwa kadri ya matakwa yao, kwa kuwa ndiyo demokrasia na kwamba kilichobaki ni kuwapa ushirikiano na kujiamini.

  Alieleza kuwa hakuna haja kuwa na hofu na uongozi wa wenyeviti hao kwa kuwa wanaongozwa na taratibu na kanuni za bunge zilizopo ambapo zinamlinda kila mmoja.

  Injinia Stella Manyanya, alisema kuwa viongozi wa kamati hizo wamepatikana kwa ridhaa ya wabunge na kwamba wamechagua kwa busara. "Huu ulikuwa uchaguzi wa wabunge wenyewe, ndio wenye ridhaa, wamechagua kwa busara," alisema ambaye pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara.
   
Loading...