Kampeni ya ccm kuwalk- out kesho yapamba moto dodoma

wabunge wa CCM ni hasara tupu!! sasa wameaibika, wanatafuta pa kufichia sura zao, hawana namna ya kuchangia!!
 
wasira+chapa+usingizi+4%255B1%255D.jpg

Hii picha imepata umaarufu mkubwa sana. Namshauri aliyepiga hii picha aiwasilishe kwenye mashindano ya CNN Journalists Award atashinda. Ila akumbuke tu kulipia fee ushauri niliompa. Hahahahaaaa!
 
Ni wabunge wa dar pekee yao wanaoweza kutoka watoto wa mjini wanaoweza kumpinga waziri wa serikali yao ya ccm,mnacheza na zungu,azan,na bonge wa temeke wakiongozwa na mnyika

Hakuna upuuzi uliowahi kuandikwa hapa jf kama huo wako!!hao wa dar si wote ni kina mama hao?mwanamme dar ni mnyika tu kama sikosei hakuna sehemu yenye watu legevu kama dar
 
Eti mgombea urais wa CCM 2015 waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa za ufisadi naye awalk out hahahahahah haiwezekani
 

Wakuu naomba msaada hapo kwenye red; hivi Kikatiba ikitokea Rais akalivunja Bunge na kuitisha uchaguzi (mkuu?) je; uchaguzi huo unahusu pia kumchagua rais au ni wabunge tu?

Kama unahusu pia kumchagua rais sitegemei hilo la Rais kuvunja Bunge litokee kamwe kwa Tz ila kama urais hausiki hata mie nashangaa JK anaogopa au anasubiri nini? Hili bunge lilitakiwa liwe limevunjwa tangu siku ile ile alipolizindua kwani lilishaonesha kuchoka tangu wakati huo hasa uchaguzi wa Spika.

Naomba ufafanuzi tafadhali.
Kwa katiba ilivyo sasa Rais akivunja bunge anapaswa kuitisha uchaguzi mpya wa rais na wabunge
 
uchaguzi unakuwa ni kwa wote pamoja na Raisi lakini kwa mazingira ya kwetu yeye ana uwezekano mkubwa wa kurudi kuliko wabunge na pia ikiwa yeye ni bado Mwenyekiti kuna uwezekano mkubwa wa kuwapiga chini waliompinga katika mchujo chamani.
Naamiini wabunge wa CCM hawawezi kucheza kamari hiyo.
Uchaguzi ukifanyika leo JK hapiti acha kujifariji
 
Pumba hizo, juzi Kikwete kasema hata CCM wamempelekea mapendekezo manane ya marekebisho ya sheria.

Tena kumbuka, kwa sasa hatuongelei "muswada", tunaongelea sheria, usipotoshe.

Povu linakutoka,na ww ni mhusika wa ule wimbo wa kamata kuwa umeolewa na CCM
 
ww ndo unapost pumba, how comes wanapitisha muswada ambao hauna mashiko then wanapeleka marekebisho! I shows hw common and bogus they are, shame on them, their party and their families. Ungekuwa na akili ya kawaida usingejaribu hata kutetea uozo walioufanya wabunge wenu vilaza, unajidhalilisha
 

[WABUNGE WA CCM WASITUTISHE na wasipimane ubavu na Mkuu wa nchi, si bora alivunje BUNGE warudi uraiani kwani wana kazi gani hizo posho wanazozidai zinatosha kusimamia uchaguzi mwingine na hawatarudi mjengoni tena na bado Kikwete atazoa kura kwa 70%]

are sure?
 
kampeni imeendeshwa leo kwa wabunge wa CCM kuhakikisha kuwa nao kesho watatoka nje ya bunge ili kutuma ujumbe serikalini na kwa rais kikwete kuwa hawakufurahishwa,wamedhalilishwa na hawako tayari kujadili muswada wa katiba mpya uliorudishwa na rais kwa mapendekezo ambayo CHADEMA na wanaharakati mbalimbali waliyaratibu na kumshawishi rais kuona umuhimu wa kuweka pembeni ule muswada wa awali ambao tayari ulipitishwa na wabunge
huo ndio upepo wa leo hapa DODOMA

Haijawahi na Haitakaa itokee kwa wabunge wa CCM!!!! Usiwape ujiko. Hawana huo moyo wa kuthubutu. Kesho inabidi tuwaimbie, "wanainama, wanainuka, wanaona haya haoooooooooooooo!!!!!!"
 
kama taarifa hizi ni za kweli, katibu wa bunge amshauri spika, hoja hiyo iletwe mwishoni mwa awamu hii ya kusanyiko la bunge, ili mkuu wa kaya, apate nafasi ya kuwatuliza akina Mh.Shelukindo.
 
Back
Top Bottom