Kampeni: Napinga Juma Nkamia kuwa Mwenyekiti wa Simba, hana uwezo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,236
Taarifa inaonyesha kwamba Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba imepitisha majina mawili ya kuwania Uenyekiti wa Simba , huku wagombea wengine wakienguliwa (sifahamu vigezo vilivyotumika ) , waliopitishwa ni Mangungu na Juma Nkamia , maana yake ni kwamba kati ya wawili hawa mmojawapo atakuwa Mwenyekiti wa Simba.

Simfahamu Mangungu kwahiyo sitamjadili .

Bali Juma Nkamia hana uwezo na wala hajawahi kuwa na uwezo wa kuongoza timu kubwa kama Simba , Nkamia ni mtu aliyejaa ubinafsi asiyeamini katika umoja , ni mtu wa majungu ambaye akipewa nafasi hiyo ataigawa Simba mapande mapande , hapaswi kupewa cheo kikubwa kama Uenyekiti wa Simba , Nkamia amekuwa kiongozi wa chini wa Simba miaka iliyopita , lakini tabia yake ya kuropokaropoka ilimfanya akang'olewa.

Pamoja na kuwa Mbunge katika bunge lililopita , lakini Nkamia hakuwa na ushawishi wowote ndani na nje ya bunge , hoja zake bungeni zilizimwa kama mshumaa jangwani , huku wananchi wa Jimbo lake wakiongoza kwa umasikini nchini Tanzania , mtu kama huyu hafai kuongoza timu ya Kimataifa kama Simba

Itaendelea...

UPDATES :

Ameangukia pua .
 
Japo una element za siasa ndani yake ila nakubaliana na wewe 100%. Juma Nkamia hafai kwenye uongozi wa watu wenye mihemko kama mashabiki wa mpira.

Ataanza kuwatukana na mwisho wa siku ataigawa timu na kuanza kuwa na wachezaji wake na ataanza kupanga kikosi. Mengine siwezi kuyasema ila Nkamia akiingia Simba ataiharibu mno.
 
Japo una element za siasa ndani yake ila nakubaliana na wewe 100%. Juma Nkamia hafai kwenye uongozi wa watu wenye mihemko kama mashabiki wa mpira. Ataanza kuwatukana na mwisho wa siku ataigawa timu na kuanza kuwa na wachezaji wake na ataanza kupanga kikosi. Mengine siwezi kuyasema ila Nkamia akiingia Simba ataiharibu mno.
unisamehe kwa kuwa kwangu mwanasiasa , lakini pia mimi ni Simba damu
 
Jinsi Nkamia anavyopenda kusifia sifia. Anaweza kuhamisha makao makuu ya simba kuwa chato.
Na kubadili jina toka Simba mpaka chato sports club. Ili watumie ule uwanja wa mpira wa Chato utakaojengwa.
Kwani nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom