Uchaguzi 2020 Kampeni inayosambaa Iramba ni "Kumi ya Dkt. Mwigulu Yatosha"

Mnambua

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
246
233
Watu wanaombea Dkt na Waziri wa Sheria na Katiba Lameck Madelu Mwigulu Nchemba akatwe na Halmashauri Kuu ili asigombee Ubunge ili apate nafasi ya kujijenga akisubiri mpaka 2025 aje kugombea Urais ili kutimiza ndoto yake.

Watu wanatarajia watu wapya kujitokeza kuchukua Fomu na kumpa changamoto Dkt Mwigulu. Kuna ambao wameshaonesha waziwazi kuwa wanagombea akiwepo Jumbe Katala ambaye tayari kishajitangaza sana kwa kupitia shule yake ya Sekondari iliyoanzishwa hivi karibuni. Wengine ni kama Dkt. Zaipuna Yona ambaye anasafiria nyota ya mke wake ambaye kwa sasa ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB ambayo inafanya vizuri kwenye soko.

Mpinzani wa siku zote wa Dkt Mwigulu Profesa Kitila Mkumbo anaonekana yupo katika hali isiyo nzuri kwani Katibu Mwenezi wa CCM amekuwa akiwatisha wanaCCM wale ambao wamepewa nafasi zingine za kiutendaji wasijaribu kwenda kugombea kuwa watakatwa tu. Habari za ndani zinadai Prof. Kitila Mkumbo anaelekea kuwa tayari hata kurudi kwenye chama chake cha Act Wazalendo ili agombee ubunge Iramba kwani tayari ana uhakika na wafuasi wa kutosha ama ndani au nje ya CCM.

Msisitizo wa wananchi wengi niliokutana nao kwa takribani majuma mawili sasa wanashauri kuwa Dkt. Mwigulu inabidi atoke kwanza baada ya kukamilisha miaka kumi ya ubunge ili arudi baadaye kumpisha hata mtu ambaye atamwandaa yeye mwenyewe. Kuna watu ambao inaonyesha Dkt. Mwigulu amekuwa na ukaribu nao ili wamuunge mkono katika harakati hizi lkn pia watu hao inaonyesha wanastahili kushika nafasi hiyo. Hawa ni pamoja na William Shila wa Ulemo, aliyekuwa Katibu Mkuu Mambo ya Ndani Kanali Kingu, Richard Mkumbo Mkuruenzi Sera Wizara ya fedha, Bwana Kitandu Ugula, Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Mmiliki wa Chuo cha Ualimu Singida na baadhi ya wafanyabiashara wa Singida Mjini.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Iramba kwa awamu moja na sasa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Juma kilimba naye anapambana kivyake na huku akimchafua Dkt. Mwigulu Nchemba kwa chinichini ili arudi bungeni mwaka huu. Juma Kilimba wanashirikiana na Jesca Kisho - Mke wa Kafulila ili kuhakikisha angalau Dkt. Mwigulu anaishia miaka kumi tu ambayo Kampeni yake (kumi ya Mwigulu yatosha) imeanza rasmi Iramba.
 
Mwigulu ni kama nembo ya singida Mkuu si rahisi kumtoa
Kila mkoa unambunge ambaye ni nembo ya mkoa fulani
 
Labda urais wa Iramba.
 
Nakubaliana na wewe!
2025 atatokea Zenji, possibly Hussein Mwinyi. 2035 itabidi atoke magharibi ya Tanzania (Mbeya, Iringa, Kigoma, Rukwa) kama huyo Mwigulu bado atakuwa relevant labda hiyo 2035 awe PM au Waziri mwandamizi kwenye wizara nyetinyeti..

President hapana, he isn't worthy it!!
 
Kwa maono yangu, Katala Jumbe anafaa sana kuwaongoza wana Iramba mjengoni. Ni mtu makini na msomi mwenye vyeti vya darasani, tofauti na jamaa wanao jiita wachumi wa phd ambao haijulikani walizipatia wapi..
Pia Jumbe ni mcha Mungu na mwenye mapenzi mema na Iramba kimaendeleo.
 
Namfahamu kweli ni mzuri huyu jamaa
 
Back
Top Bottom