Kampe mamako

Kampe mamako

WASIRA
avatar115449_1.gif
 
Kudadeki Bujibuji wewe naona mtu wa mipasho sana aise. Yaani nimecheka sana!! Kuna mtu alimnunulia mama mkwe khanga na maneno ya mshale yaani hadi leo ni miaka kama 30 yule mama hakuivaa!!! Alimpa live na ugomvi tukasuluisha wapi!! Yule mama hadi leo she is 79 anakumbuka!! Tuwe makini kwa hawa watu maana tunaweza nunua laana kwa watoto wetu.
 
Hivi kupendeza na kuwa mzuri si vitu vinne tofauti? Unaweza kuwa mzuri na usiwe unapendeza. . .
 
huyo jamaa yako alikuwa na ugomvi na mama yake?
Nini kisa cha kumtukana mama yake kiasi hicho?

Wakipendana sana wote wawili lakini kwa kutotambua jamaa alichagua rangi nzuri ya kanga ili ampendeze mzazi wake. Kosa lake hakulisoma jina,yeye alibeba na kupeleka tu.
 
Basi huu ni mwanzo wa ugomvi mpya

La! Kwa bahati nzuri mama ni mwelewa na mwenye heshima yake kiasi kwamba hakumkabili mwanawe akijuwa kuwa sasa ndio yatakuwa matusi. Alikwenda kwa mke wa mwanawe na kumuonyesha na mkwe alipomkabili mumewe ndipo ilipobainika tatizo. Ilibidi itafutwe kanga nyengine na kuanzia hapo jamaa alikuwa makini na majina ya kanga.
 
Lakini ana bahati, wa mama wa huku mtaani kwetu wana ongea hadi unaweza kupata kansa kwa maneno yao
 
Back
Top Bottom