Tetesi: Kamishna wa Madini Asimamishwa kimya kimya

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,846
Kuna Taarifa ambazo si rasmi kwamba, kamishna wa madini wa wizara ya nishati na Madini alisimamishwa kimya kimya bila habari zake kutangazwa.

Vile vile, kamishna wa Nishati wa wizara hiyo naye alisimamishwa kimya kimya, Gazeti la Mtanzania limelipoti kwamba,.

"Kwa taarifa walizonazo ambazo bado hazijathibitishwa ni kwamba makamishna hao wamesimamishwa kimya kimya".
 
huyo aliyewekwa nae atakuja kusimamishwa tuuu. It is a vicious circle. Utumbuaji hautaisha kama bado CCM ndio wenye majipu na watumbuaji ni wao wenyewe.
 
Wanaosimamishwa si makada wa CCM. Ni majizi na manyang'au

Vipi yule waziri aliyeagiza mafuta bila tender mpaka leo mafuta yamegoma kushuka bei wakati huko soko la dunia ni karibu na bure? Kibaya zaidi hata kusema hiyo shehena itaisha lini ili tukutane na unafuu haisemwi. Lakini yeye hawezi kutumbuliwa kwani ni mwanaccm mwenzetu.
 
Hao mabwana ni kweli wamesimamishwa na Katibu Mkui husika. Sababu hazijapatikana rasmi na si za kiutendaji kabisaa wala za kifisadi..kwa kifupi hao jamaa hawakuwa majipu na hawatakuwa majipu asilani. WATEULE wa Awamu hii wana dalili ya kumwangusha JPM sababu hawaelewei chakufanya. Activity plan ni hawana sijui wanfanyeje kazi
 
Duu, kweli Tanzania mpya inatengenezwa sasa.

Kimyakimyaa...R.I.P. yule mbongofleva aliyeimba "kimyakimya" alifia sauz akazikwa moro
 
Makada weru
Wanaosimamishwa si makada wa CCM. Ni majizi na manyang'au

Makada wetu hawawezi kuonekana katika mikasa kama hii wao wanatoa vimemo tu watendaji wanakufa wenyewe huko. Kumbuka tuna makada wacheche katika serikali wengi wanatudis. Sema makada wetu hasa wafanya biashara wanatumia hawa watumishi kuhujumu uchumi wetu kisha wanaonekana watumishi ndio tatizooo...
 
Huo ndiyo mfumo wa uendeshaji wa serikali kwa sasa.Nasikia wateule wa serikali hii ukipita mwezi mmoja bila ya kumfukuza Kazi au kumsimamisha mtumishi yeyote aliye chini ya mamlaka yake,basi mteule huyo atapaswa kuandika barua ya maelezo kwa nini hajafukuza au kusimamisha mtu kazi.
 
Hao mabwana ni kweli wamesimamishwa na Katibu Mkui husika. Sababu hazijapatikana rasmi na si za kiutendaji kabisaa wala za kifisadi..kwa kifupi hao jamaa hawakuwa majipu na hawatakuwa majipu asilani. WATEULE wa Awamu hii wana dalili ya kumwangusha JPM sababu hawaelewei chakufanya. Activity plan ni hawana sijui wanfanyeje kazi
Wewe ndio hujui kazi.
leseni ya msingi unapewa mathalan miaka mitatu uwe umeshaanza uchimbaji.
mtu anakaa miaka 10,tena anahodhi vitalu zaidi ya sita,wachimbaji wadogo wanahitaji maeneo wewe kamishna kwa nini usitumbuliwe kwa kushindwa kazi
 
Kwa nini wamesimamishwa kimya kimya??
Kuna madudu mengine hayafai kuwekwa hadharani mkuu. Ni hivi mkeo akikufumania akaamua kukuacha kimyakimya we ukiulizwa utasema sababu? Sana sana utasema muulizeni mwenyewe.
 
Hao mabwana ni kweli wamesimamishwa na Katibu Mkui husika. Sababu hazijapatikana rasmi na si za kiutendaji kabisaa wala za kifisadi..kwa kifupi hao jamaa hawakuwa majipu na hawatakuwa majipu asilani. WATEULE wa Awamu hii wana dalili ya kumwangusha JPM sababu hawaelewei chakufanya. Activity plan ni hawana sijui wanfanyeje kazi
Wewe ndio hujui kazi.
leseni ya msingi unapewa mathalan miaka mitatu uwe umeshaanza uchimbaji.
mtu anakaa miaka 10,tena anahodhi vitalu zaidi ya sita,wachimbaji wadogo wanahitaji maeneo wewe kamishna kwa nini usitumbuliwe kwa kushindwa kazi
Kamishna yupi aliyesimamishwa.?? Kwa maana ambaye yupo ni Ally Samaje alikuwa anakaimu nafasi iliyoachwa na Paul Masanja baada ya kupandishwa cheo cha unaibu katibu mkuu mwishoni mwa utawala wa Kikwete. Baada ya Magufuli kuingia, alipangua teuzi zote zilizofanywa na Kikwete kipindi cha mwisho. Sasa hivi wakina Paul Masanja na Omar Chambo wanasubiri wapangiwe kazi. Lakini nafasi ya ukamishna wa madini bado iko wazi na Paul Masanja hakuondoka kwa skendo yoyote zaidi ya kupandishwa cheo na akatolewa baada ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom