Kambi za Lowassa, Sitta zadaiwa kuipasua CCM


Prodigal Son

Prodigal Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2009
Messages
972
Likes
82
Points
45
Prodigal Son

Prodigal Son

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2009
972 82 45
Kambi za Lowassa, Sitta zadaiwa kuipasua CCM

HERI wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Huo ni usemi katika kitabu kitakatifu cha Biblia.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Pius Msekwa amesema, semi zenye maudhui ya upatanishi zilitumiwa na Kamati ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuzipatanisha kambi mbili za wabunge wa CCM zilizosigana ndani ya Bunge kwa muda mrefu.

Amezitaja kambi hizo kuwa ni ile iliyokuwa ikiongozwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta na ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.

Msekwa amewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa,Kamati ya Mwinyi imefanya kazi nzuri ya kutafuta kiini cha mpasuko miongoni mwa wabunge wa CCM ndani ya Bunge kama ilivyotumwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho.

Amesema,Kamati ya Mwinyi ilikutana na wabunge wa CCM kwa siku nne mfululizo kuanzia Novemba mosi hadi Novemba nne, mwaka jana mjini Dodoma na kuzungumza nao ili kudadisi kiini cha mpasuko baina yao bungeni.

Kutokana na maelezo ya wabunge hao wa CCM, Kamati ya Mwinyi ilibaini kuwa kulikuwa na makundi, la Lowassa na la Sitta, chanzo kikiwa ni hofu kutoka kila upande kuwa mwenzake ana mpango wa kumng’oa.

“Kutokana na maelezo yao, ilionekana kuwa uhasama hasa ulianza baada ya ripoti ya Richmond kuwasilishwa bungeni ambapo yaliibuka makundi hayo mawili yaliyoanza kushambuliana, kundi moja likiitwa la mafisadi na lingine likijiita la upambanaji dhidi ya ufisadi,” amesema Msekwa.

Msekwa amesema,kutokana na malumbano hayo, kila kundi liliingiwa na hofu kuhusu kundi lingine kuendesha mikakati ya chini chini ya kuwaondoa wenzao madarakani.

“Hawa wanaodai kupambana na ufisadi walianza kulalamika kuwa kundi la mafisadi lilikuwa linawatumia watu ili kuwang’oa katika ubunge kwa kumwaga mabilioni ya fedha kwa watu hao na kundi la pili lilikuwa likilalamika kwa kubatizwa jina la mafisadi, jina ambalo kimsingi linamaanisha rushwa, jambo ambalo ni kosa kisheria,” alisema.

Msekwa amesema,baada ya kubaini hilo, Kamati ilizungumza na kila kundi kwa nyakati tofauti kujadili namna nzuri ya kuondoa tofauti baina yao.

“Kimsingi hali sasa ni shwari, lakini bado ipo kazi ambayo imebakia na tumeiomba NEC ituongeze muda ili tuifanye, nayo ni ya kukutanisha makundi hayo na vinara wao (Sitta na Lowassa) ili wote watoe madukuduku yao mbele ya wenzao na kuhitimisha uhasama. Kazi hii tutaifanya karibuni na tutaleta taarifa katika kikao cha NEC mwezi ujao,” alisema Msekwa.

Amesema,Kamati ilibaini kuwa malumbano hayo yalipamba moto zaidi kutokana na Kamati ya Wabunge wa CCM kutofanya vikao kama kanuni zinavyoelekeza na hivyo wabunge kuligeuza Bunge kuwa sehemu ya kushambuliana badala ya kutumia vikao vya Kamati ya Wabunge wa CCM.

Alisema Kamati ilipochunguza kama kulikuwa na uendeshaji mbovu wa shughuli za Bunge chini ya Spika Sitta na kuwa chanzo cha malumbano hayo, Kamati hiyo ikiwajumuisha watalaamu wa zamani wa uspika (Msekwa-Spika Bunge la Tanzania na Abdulrahman Kinana – Spika Bunge la Afrika Mashariki), ilibaini kuwa Sitta alikuwa akiendesha Bunge kwa kuzingatia kanuni na sheria za Bunge bila kupotosha hata kidogo.

“Hata hivyo wao wenyewe (Wabunge wa CCM) walionesha wasiwasi kuhusu baadhi ya kanuni za Bunge kuwa inawezekana zikachangia malumbano hayo, lakini tuliwaambia kwa kutumia vikao vyao vya Bunge, wanaweza kuziangalia kanuni hizo kuona kama wanaweza kuzirekebisha kwa namna watakavyo bila kuingiliwa,” amesema.

Hata hivyo, alisema ishara iliyoonekana katika kikao cha Bunge kilichopita ambapo wabunge na Sitta walifunga rasmi mjadala wa Richmond ndani ya Bunge bila kushinikizwa, inaonesha kuwa Kamati hiyo imeanza kupata mafanikio makubwa ya kujenga umoja na mshikamano baina ya wanaCCM hao.

Alisema Kamati hiyo pia iliridhishwa na namna wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar walivyokuwa wakijadili masuala yanayowasilishwa katika Baraza hilo ili kujadiliwa.

CHANZO
Habari Leo
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
Msekwa hasemi ukweli; tofauti za makundi hayo mawili ni kubwa mno na hazihusu "kung'oana"! Ni tofauti za nani ni chanzo cha matatizo katika uendeshaji wa taifa hili. Nimezungumza na baadhi ya wajumbe waliokuwemo humo kwenye vikao na ukweli ni ule ule kama waraka wao ulivyotolewa, tofauti zao zinahusiana na kanuni na siyo masuala binafsi. Na katu hawawezi kupatana. Rudieni kusoma waraka wao!!!
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
94
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 94 0
- Msekwa an intellectual mzima inasikitisha sana anapohangaika na hizi taarabu, sio siri na inafahamika kwamba ana kinyongo na Six na anajaribu kila njia kulipa kisasi, habari za kamati zinatakiwa kuelezwa na Kinana ambaye hapa ni independent of any-kundi.

- Matatizo ya sasa ndani ya CCM ni more than kung'oana hata mtoto mdogo hawezi kudanganyika na hilo, kuna kundi linalodai haki za wananchi na la mafisadi, Msekwa na Mkewe wamo kundi hili la mafisadi, yaani kwa maneno mengine hapa kesi ya nyani umempelekea ngedere! I mean Msekwa katibu mtendaji mkuu wa kwanza wa CCM under Mwalimu, leo anababaika kwa sababu tu ya hela ndogo sana za mafisadi!

- Katibu mtendaji wa kwanza wa CCM, leo anatishika na fisadi Lowassa na kijana mdogo fisadi Rostam! na bila aibu anasimama mbele ya public na kubabaisha maneno as if sisi wananchi wote ni watoto wadogo tusio na akili! Akiwa Spika wa bunge alikuwa pia kwenye pay roll ya Rostam through Vodacom, halafu leo eti wananchi tutegemeee achunguze tatizo la makundi ya CCM eti aje aseme kwamba ni kundi la mafisadi ndio chanzo cha matatizo, si watamng'oa cheo chao hicho walichompa cha lala salama! ili atafute za mwisho mwisho, kama kweli CCM wanatafuta chanzo cha tatizo ndani ya chama chao, dawa ilikuwa kuwapa wachunguzi ambao ni Independent, lakini sio viongozi wenye visasi kama huyu aliyeshindwa kwenda kwenye mazishi ya Marehemu Akukweti, kisa alitumika kumngoa u-spika, hiyo ripoti ya hiyo kamati wangekaa nayo tu huko huko maana ni waste of our National time hata kuwasikiliza!

Respect.


FMEs!
 
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
2,223
Likes
101
Points
145
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
2,223 101 145
Kambi za Lowassa, Sitta zadaiwa kuipasua CCM

HERI wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Huo ni usemi katika kitabu kitakatifu cha Biblia....


Huu ni unafki mkubwa kabisaaaa ati kambi ya Lowassa na Sitta, ivi mwatakaja kujifanya hamjui what was the main issue au mlikuwa mwatuzuga hapa? kwahiyo tuwaeleweje kuwa Richmond was Fake issue eeehh

....Msekwa amesema,kutokana na malumbano hayo, kila kundi liliingiwa na hofu kuhusu kundi lingine kuendesha mikakati ya chini chini ya kuwaondoa wenzao madarakani.


Ivi msekwa wewe wataka kutuambia hawa wabunge walipo chaguliwa walikuwa hawajui kuwa ukiingia kwa mjengoni "BUNGENI" ni kuchapa kazi sasa iyo hali ya wao kutiliana mashaka imetokea wapi? ni dhahili hao wabunge ni wachafu wote kwanini upande fulani uwe worried kwa kundi jingine if wanajuwa wako sure na walichokitenda kupitisha miswaaada mibovu ya richmond na hao waliowashutumu wenzao na wakijitutumua kuwa walikuwa na record zote yanini wawe na wasi wasi wa kuharibiwa kwa majimbo yaooo? hapo na hoji na kutiliashaka kipengere hiki, si mliapa kuwa watawatumikia wananchi wao walio wapigia kura sasa iweje uhofu kuwa jimbo lako watakumwaga kama unatetea maslahi ya nchi?

......“Kimsingi hali sasa ni shwari, lakini bado ipo kazi ambayo imebakia na tumeiomba NEC ituongeze muda ili tuifanye, nayo ni ya kukutanisha makundi hayo na vinara wao (Sitta na Lowassa) ili wote watoe madukuduku yao mbele ya wenzao na kuhitimisha uhasama. Kazi hii tutaifanya karibuni na tutaleta taarifa katika kikao cha NEC mwezi ujao,” alisema Msekwa.


Shwari kivipi na kama iko shwari kwanini minong'ono bado ipo? Je wananchi wamerithika na huko Mkataba fake wa Richmond kufungwa kiholela holela?? au ndio kujistiri viongozi wetu. Na kama ni kweli shwari ya nini kuwepo na vikao vya usuruhishooo kwa kundi na kundi jingine??

Nadhani ni Muda wenu sasa umewadia mtupishe kwa hayo madaraka sasa naona upeo wenu unaanza kufikia kikomo sasa sioni busara zenu zaidi ya kustiriana tuuuuu na unafki kukithiri kila kona ya uongozi wenu wa CCM na fitna kibao na kukiharibu chama kwakukipaka uchafu wenu. Hampendi kukubali mabadiliko kabisa na uwajibikaji na mwatuletea blaa blaaa zenu hapa

......Alisema Kamati ilipochunguza kama kulikuwa na uendeshaji mbovu wa shughuli za Bunge chini ya Spika Sitta na kuwa chanzo cha malumbano hayo, Kamati hiyo ikiwajumuisha watalaamu wa zamani wa uspika (Msekwa-Spika Bunge la Tanzania na Abdulrahman Kinana – Spika Bunge la Afrika Mashariki), ilibaini kuwa Sitta alikuwa akiendesha Bunge kwa kuzingatia kanuni na sheria za Bunge bila kupotosha hata kidogo.


Ivi bunge lilitakiwa liongozwe vipi kwa favor ya CCM au wananchii? kwahiyo hiii ni dhahili Pius Msekwa kipindi ulichokuwepo Bungeni ulikuwa unai favor serikali na CCM na uozo mwingine wote na ndio nyie wapinga maendeleo na mlioturudisha nyuma sana kwa kujistili na maovu yenu na mpaka sasa mwaendelea kufanya hivyo unafki mkubwa huo.

Hampendi kanuni zifuatiliwe hata kidogo nyie ni kupenda kupindisha katiba kila kukicha, Hii hali ikifika kikomo mtafungwa nyie viongozi msio kubali mabadiliko na upepo uendavyo.


 
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
2,223
Likes
101
Points
145
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
2,223 101 145
Kweli nasema kwa machungu,

Msekwa mie sija ona ulicho wasaaadia watu wako wa ukerewe kwa muda wote uliopo madarakani kwa CCM na kuijua siasa ipasavyo lakini ulishindwa kunyanyua wilya ya Ukerewe mpaka kesho kunaendelea kusinyaa tu, Hako karami na kaumeme mliko kaweka hapo mjini NANSIO wewe na Getrude Mongera mtasema mlishughurikia? wala ng'oo hiyo ilikuwa kwa sera muda mrefu tuu ni mlishindwa kufuatilia tizama huko Mwanga(usangi,Shinghatini,Vyagha, etc) umeme ulivyosambaaa mpaka mlimani juuu amabako huwezi tegemea na huko mwanga wana nini ambacho wanazarisha hakuna ni wanakijiji wanajilimia kile walicho nacho na wanweza lipia umeme lakini ukerewe nikisiwa kikubwa sana na kina mambo mengi lakini hakuna maendeleo mpaka kesho, mihogo ndio imemalizwa na wadudu hakuna chakula sasa hatupati udaga i mean unga wa mhogo na ndiko kulikuwa na Chuo Kikubwa cha CCM watu walikuwa wanakwenda jifunza siasa pale Mrutunguru sasa na chuo kimekuwa secondary na je inawasaidia hao wakazi wa mrutunguru na vijiji vilivyuko karibu kama Mkasika,Kazirankanda, Njia ya kwenda Bugorola?

Kuna misitu ya Mbao huko Rubya hata umeme haujafika.
 
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
31
Points
135
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 31 135
Fisadi ataweza vipi kuuchukia ufisadi?
 
F

FM

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2009
Messages
202
Likes
1
Points
0
F

FM

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2009
202 1 0
Niliipenda hii kutoka kwenye waraka wa wapiganaji wa ccm, kwamba hawtakubali kupatanishwa na mafisadi, na kwamba juhudi zozote za kuwapatanisha ni sawa na kukubali kuwafukuza kwenye chama (haya sio maneno halisi yaliyotumika). OK juhudi zinaendelea, Kamati ya usuluhishi nimeongezewa muda ikamilishe kazi yake ya upatanishi kati kambi ya mafisadi na wapiganaji. Chonde chonde mnaojiita wapiganaji, wakati wa kujitenga na ccm na kuendeleza mapambano ya kweli maslahi ya taifa ni sasa. TANZANZIA BILA CCM INAWEZEKANA.
 
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
1,098
Likes
12
Points
135
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
1,098 12 135
The game is going on..SITA vs LOWASSA..yaonekana ngoma inazidi kuwa nzito na ninatabiri kundi la lowassa sasa litajipambambanuaa zaidii kuwaonyesha akina Six kuwa CCM bila UFISADI haina UHAI wa kutawalaa Tanzania.
 
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Messages
7,495
Likes
104
Points
160
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2008
7,495 104 160
CCM si ipasuke basi? Viongozi wanachukiana hivi halafu tutarajie kusonga mbele kama TAIFA?
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Si vizuri sana kujisifu lakini mimi huwa mdadisi sana kabla ya kulikubali jambo kuna tamko moja lilitoka likisema ni la wapiganaji content yake ilinipa shida kuikubali kama iliandaliwa na wale tumekuwa tukiwasikia ndani ya CCM lakini katika matukio ya hivi karibuni yaliyotokea kwenye NEC yamezidi kuziweka karibu zaidi dots zangu ambazo bado naziunganisha imenilazimu niusome upya hebu soma mwenyewe baadhi ya matamko yao kabla ya vikao vya NEC
-----------------
Kwamba, hakuna uwezekano wowote wa mapatano, mshikamano, umoja, au kwa namna
yoyote ile usuluhishi kati ya pande mbili zinazopingana ndani ya chama hususan kwenye
masuala yanayohusiana na ufisadi. Tunaamini njia pekee ya kurejesha nidhamu na umoja wa
kweli ni kuondolewa mara moja kwa chembe zote zenye kuharibu jina la chama na ambao wamelidhulumu taifa letu utajiri wake.
1. Viongozi wafuatao wasimamishwe mara moja katika uongozi wa chama kwa mujibu

wa Ibara ya 8.2.4 ya Kanuni za Maadili ya Chama na kwa vile tayari wameshachafuka

kutokana na uzito wa tuhuma mbalimbali (wengine hadi za kihalifu) hawastahili kuwa

viongozi katika nafasi yoyote ndani ya Chama. Tunataka viongozi hawa waamue
wenyewe kuachia nafasi zao au Chama kiwawajibishe mara moja. Kundi hili
limekipaka chama matope.

Edward Lowassa MB
- nk

Viongozi wengine wa chama nao washughulikiwe kwa mujibu wa kanuni na taratibu za
chama bila ya kuwaonea haya, kuwavumilia, kuwabeba au kwa namna yoyote ile kuwatafutia
udhuru wa kwanini wasishughulikiwa.
2. Wahusika wakuu wa kashfa hizi zifuatazo washughulikiwe kichama na kiserikali

-Kashfa ya Loliondo – ambapo urithi wa watoto wetu uliuzwa na umeendelea kuuzwa kwa wageni.

-Kashfa ya IPTL - nk

Kashfa hizo zote zimetutia aibu kama Watanzania na zaidi pia kama wana CCM ambao

Chama chetu ndiyo kimeunda serikali inayotawala. Hatuwezi kamwe kukubali kwa namna
yoyote ile kuendelea kukaa na wahusika wa kashfa hizo kwa kisingizio au sababu
yoyote ile. Endapo Chama chetu kitaamua kuwavumilia na kuwasafisha wahusika wa
kashfa hizi mbalimbali kwa kisingizio cha kutafuta "umoja, mshikamano, na utulivu" basi watakuwa wamepiga kura ya kukimega chama,My take,
nimeanza kuamini kilichofanywa bungeni na wapiganaji kwenye sakata la Richmond si kushindwa ni retreat strategy hata vitani hiyo hufanyika wakati wa vita vya Iraki kuna wakati wamarekani walitumia mbinu hiyo kwa takriban kama siku tano tukajua wameshindwa basi hawa wanaojiita wapiganaji kama kweli wapo naona wako serious ni maoni yangu tu


 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Wameshaamua kupatana hivyo CCM haitapasuka. Kesho utawaona wakishikana mikono pamoja na kupata moja moto moja baridi katika meza moja.
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Wameshaamua kupatana hivyo CCM haitapasuka. Kesho utawaona wakishikana mikono pamoja na kupata moja moto moja baridi katika meza moja.
Mimi navyoona kumeguka will not happen today or tommorow it will take time but very soon well watashikana mikono wanywe bia pamoja hiyo si kwamba wamepatana kwenye mambo ya msingi hayo ni mambo ya ubinadamu zaidi ya maslahi ni kama kuosha uso mbele ya jamii kuondoa aibu

kama wanavyotumia magazeti kusema hakuna mpasuko hapo hapo wanasema tume imeongezewa muda wa nini sijui si kupoteza muda na pesa za walipakodi tu Msekwa anasema tatizo ni Richmond hapo hapo anaomba muda atafute source ya tatizo hajasema ule muda aliopewa aliufanyia nini na ameshindwa nini
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Wanachofanya sasa ni kuziba ili uchaguzi uwe mzuri ila wale waliokuwa wantumia ajenda ya ufisadi toka CCM ndio wataumia na utaona kuwa misamiati huu utaendelea mpka wa uchaguzi na makundi yao hivyo CCM wamechoka tayari kimawazo na hata wao wanajua hivyo
 
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,882
Likes
64
Points
135
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,882 64 135
- Msekwa an intellectual mzima inasikitisha sana anapohangaika na hizi taarabu, sio siri na inafahamika kwamba ana kinyongo na Six na anajaribu kila njia kulipa kisasi, habari za kamati zinatakiwa kuelezwa na Kinana ambaye hapa ni independent of any-kundi.

- Matatizo ya sasa ndani ya CCM ni more than kung'oana hata mtoto mdogo hawezi kudanganyika na hilo, kuna kundi linalodai haki za wananchi na la mafisadi, Msekwa na Mkewe wamo kundi hili la mafisadi, yaani kwa maneno mengine hapa kesi ya nyani umempelekea ngedere! I mean Msekwa katibu mtendaji mkuu wa kwanza wa CCM under Mwalimu, leo anababaika kwa sababu tu ya hela ndogo sana za mafisadi!

- Katibu mtendaji wa kwanza wa CCM, leo anatishika na fisadi Lowassa na kijana mdogo fisadi Rostam! na bila aibu anasimama mbele ya public na kubabaisha maneno as if sisi wananchi wote ni watoto wadogo tusio na akili! Akiwa Spika wa bunge alikuwa pia kwenye pay roll ya Rostam through Vodacom, halafu leo eti wananchi tutegemeee achunguze tatizo la makundi ya CCM eti aje aseme kwamba ni kundi la mafisadi ndio chanzo cha matatizo, si watamng'oa cheo chao hicho walichompa cha lala salama! ili atafute za mwisho mwisho, kama kweli CCM wanatafuta chanzo cha tatizo ndani ya chama chao, dawa ilikuwa kuwapa wachunguzi ambao ni Independent, lakini sio viongozi wenye visasi kama huyu aliyeshindwa kwenda kwenye mazishi ya Marehemu Akukweti, kisa alitumika kumngoa u-spika, hiyo ripoti ya hiyo kamati wangekaa nayo tu huko huko maana ni waste of our National time hata kuwasikiliza!

Respect.

FMEs!
Mkuu FMEs kama vile nilikuwa nakuona unavyoandika jinsi unavyotetemeka kwa hasira. I think it is stupid kumpa Msekwa nafasi aliyonayo, pamoja na yeye kuwa intelectual, inaonekana ni intelectual aliyebatizwa kuilinda CCM, kwa jema na hata kwa baya, ana abuse itelect ability yake kwa kutupumbaza na kutufanya wajinga.

I wonder anapata wapi courage ya kusema "kupatanisha makundi mawili", badala ya kusema kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria watu wa kundi, ambao inaeleweka kwa kila mtu, ikiwa pamoja na yeye kuwa ni mafisadi.

Nadhani tunaona jinsi mwalimu alivyokuwa kifanya kazi na wanafiki. Kati ya wajumbe watatu wa kamati ya Mwinyi nilitegemea busara zitatoka kwa Msekwa na Mzee Mwinyi, na Kinana awe kama katibu wao tu, lakini kinyume chake in Kinana naona dalili ya kutaka kurudisha respect of rules and laws, desire to resotore dignity na desire to put things straight.

Inagwa Mzee Mwinyi ni kama anabembeleza pande zote mbili, Msekwa is clearly in war with wapambanaji. Am glad imesemwa wazi kuwa Sitta alifuata kanuni zote za Bunge kwa usahihi, at least he does not have any excuse to raise the issue proffesional inadequacies in Six's speakership. To the contrary tunaweza kuanza kuuliza kwa nini bunge lake lilikuwa mhuri.
 
M

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Messages
7,377
Likes
1,526
Points
280
M

MkamaP

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2007
7,377 1,526 280
Lowasa na Sitta ni kama Raila na Kolonzo Musyoka wa kenya.Ama Raila na Kibaki .

Mwanzo kabisa Raila alimuunga mkono Kibaki kwa makubaliano ya kupewa uwaziri mkuu na kubadirisha katiba kuwa kama ya UK, yani Rais awepowepo tu wakati waziri mkuu awe na nguvu na kibaki alipofika Ikulu akampiga chini Raila na katiba yake.Raila akaacha uwaziri wa ujenzi akaenda kuungana na Musyoka ktk uchaguzi ulifuata kwa makubaliano yaleyale kwamba Musyoka agombee urais harafu yeye waziri mkuu.

Ulipofika uchaguzi Raila kaona anakundi kubwa akabadirika akautaka Urais wakatengana na Musyoka dakika za majeruhi. Uchaguzi ukafika Raila kashinda Musyoka kwa kumkomoa Raila kamwambia Kibaki iba kura mie nitakuwa upande wako lakini unipe umakamu wa Rais.Mchezo ukawa hivyo na ngoma ikalala.

Sitta ,Lowasa na RA na Kikwete hawa watu walikuwa ktk kambi moja na hata sakata la Richmond lilipoanza sitta alilikingia kifua. Sasa walichokorofishana baadae sijui yawezekana kabisa Sitta alinyimwa mugao eiza wa Richmond ama nafasi fulani.

Sasa leo sielewi inakua je? sitta nimpinga ufisadi??
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
81,961
Likes
121,266
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
81,961 121,266 280
Kama kweli hawa wangekuwa wanazijua dini kwanini wasiache kuifisadi nchi na kuweka maslahi ya nchi mbele badala ya matumbo yao ili kumuogopa Mungu wao!? :confused:

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*


2/17/2010Biblia, Quran yatumika kuokoa mpasuko CCM

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania bara) Pius Msekwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu mustakabali wa chama hicho mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC)Habel Chidawali, Dodoma
MwananchiMAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa amesema mkutano wa Halmashauri Kuu wa chama hicho (Nec) ulilazimika kutumia mistari ya Biblia na Quran kuyapatanisha makundi yaliyoibuka baada ya sakata la Richmond kuibuliwa, hivyo kutishia uhai wa chama.

CCM iliingia kwenye mtafaruku uliotengeneza makundi mawili makubwa mwaka 2008 baada ya sakata la Richmond kutinga bungeni na kisha kuwakumba baadhi ya makada wa juu wa chama hicho, waliotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo ya kifisadi iliyotokana na zabuni tata ya uzalishaji umeme wa dharura iliyoipa ushindi kampuni hiyo(Richmond).

Baadhi ya makada wa chama ngazi za juu katika chama na serikali, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili walioitumikia Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa mchakato wa zabuni hiyo, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi walilazimika kujizulu kutokana na kudaiwa kuhusika katika sakata hilo, huku maofisa wengine wa umma wakitakiwa kuchukuliwa hatua na serikali.

Kutokana na hali hiyo kukaibuka makundi yaliyojulikana kuwa ya mafisadi na ya wapiganaji ambayo yote yanawapambe wengi. Makundi hayo yalijionyesha wazi kuwa hayapikiki chungu kimoja, hivyo kukiweka chama njia panda, huku baadhi wakibashiri kwamba, sasa CCM inaelekea kupasuka.

Akizungunza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Msekwa alieleza mambo ambayo kamati ya rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, iliyoundwa na Nec mwaka jana kuchunguza chanzo cha makundi hayo na jinsi Nec ilivyomaliza mpasuko huo.

Msekwa ambaye ni miongoni mwa wajumbe watatu katika kamati hiyo, alisema kupatikana kwa amani katika mgogoro huo, kulitokana na wapatanishi kutumia vitabu vya Biblia Takatifu na Quran Tukufu.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo iliyoundwa na Nec ni Abdulrahman Kinana na mwenyekiti, rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

"Mzee Mwinyi alitumia zaidi Quran na mimi nilitumia Biblia. Nilitumia neno la Mungu kutoka Injili ya Mathayo Mtakatifu kifungu kinachosema: "Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu" na Mzee Mwinyi alitumia maneno yanayosema: "Ikiwa kuna makundi mawili yanagombana basi ni heri yasuluhishwe na ikiwa moja litakataa basi waandamwe," alifahamisha Msekwa.

Mbali na kutoa siri hiyo, Msekwa alimmwagia sifa Spika wa Bunge Samuel Sitta kwa kile alichoeleza kuwa amefanikiwa kumaliza sakata la Richmond kwa busara kubwa.

Akielezea sababu ya uhasama wa wabunge wa CCM, Msekwa alisema yalitokana na sakata lililoibuliwa mwanzoni mwa mwaka 2007 na kusababisha mtikisiko mkubwa ndani ya serikali ya awamu ya nne.

Alisema baada ya sakata hilo kulipuka kulitokea mgawanyiko mkubwa katika chama uliozaa makundi mawili. Alitaja vinara wa makundi hayo kuwa ni mbunge wa Monduli Edward Lowassa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

Kwa mujibu wa Msekwa makundi hayo kila moja lilikuwa likituhumu kundi jingine kuwa lina nia ya kuwang'oa wenzao madarakani, jambo hilo lilileta mtafaruku mkubwa.

"Tumewaita vinara wa makundi hayo na kukaa nao meza moja. Lakini hatukuwa na nia ya kutaka kuwatoa kafara kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, bali tulitaka amani idumu jambo linaloonyesha kuwa tumefaulu," alisema Msekwa na kuongeza:

"Pamoja na kukaa nao kwa muda wa saa nne katika moja ya kumbi za pale bungeni, kila mmoja alikuwa na kero zake jambo tulilogundua kuwa kila mtu alikuwa akifagilia kitumbua chake kisiingie mchanga".

Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama ni kumtonesha kidonda jana Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Msekwa alimfagilia spika Sitta kwa kumaliza sakata la Richmond na kisha kuonya kuwa watakaoliendeleza watachukuliwa hatua.

Alisema kauli ya Sitta wakati wa kumaliza suala la Richmond, ilionyesha jinsi spika alivyo makini na kwamba, alimemaliza hasira zake zote na alikuwa na nia ya kuijenga nchi na kuimarisha chama.

"Yule Spika sisi tunaamini kuwa alimaliza hasira zake kabisa na kwa kweli ni mtu wa kupongezwa kwani alimaliza sakata la Richmond na kutoa onyo kwa wale wanaotaka kuendeleza.

Hilo ni jambo ambalo kiongozi makini anatakiwa kulifanya, pale inaonyesha kuwa amefungua ukurasa mpya kabisa."

Siku mbili kabla ya mkutano wa 18 wa Bunge kufunga hoja ya Richmond, lilijadiliwa kufungwa na kisha Spika Sitta alimwonya Rostam kuacha kuendeleza malumbano na badala yake akubali yaishe.

Hata hivyo mbunge huyo alikuja juu na kusema kuwa Sitta hakuwatendea haki Watanzania kwa namna alivyomaliza suala hilo, kwani bado kuna mambo mengi yangeweza kuwekwa wazi endapo ingeundwa kamati maalumu ya majaji kuchunguza suala hilo.

Wakati huohuo, CCM imepitisha kwa kauli moja kuwa siku ya Desemba 31 kila mwaka kwa Watanzania kuadhimisha Siku ya Kawawa kwa ajili ya kumkumbuka mkongwe huyo wa siasa nchini. Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari, wamewataka Watanzania kutumia jina la Kawawa katika maeneo muhumu ikiwemo viwanja vya ndege kwa ajili ya kumuenzi na wakasema wanaandaa utaratibu kumpa nishani ya juu ya heshima kutokana na uongozi wake uliotukuka.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Mimi navyoona kumeguka will not happen today or tommorow it will take time but very soon well watashikana mikono wanywe bia pamoja hiyo si kwamba wamepatana kwenye mambo ya msingi hayo ni mambo ya ubinadamu zaidi ya maslahi ni kama kuosha uso mbele ya jamii kuondoa aibu

kama wanavyotumia magazeti kusema hakuna mpasuko hapo hapo wanasema tume imeongezewa muda wa nini sijui si kupoteza muda na pesa za walipakodi tu Msekwa anasema tatizo ni Richmond hapo hapo anaomba muda atafute source ya tatizo hajasema ule muda aliopewa aliufanyia nini na ameshindwa nini
Mimi nadhani wanazuga tu kwani nimwaka wa uchaguzi huu..kamati ya Mwinyi kuongezewa muda ni kupoteza muda na kutuzuga tu hakuna lolote jipya watakalolifanya..Wameshindwa kwa kipindi chote walichopewa awali ndio wataweza sasa,wakati wengine wameshasafishwa tayari na kuwa weupe kama theluji??
 
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Msekwa anatakiwa alipe deni kwanza la matibabu ya mwanaye miaka 6 iliyopita huko nchini Ufaransa!
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,613
Likes
9,212
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,613 9,212 280
..CCM nzima imejaa wezi, wachumia tumbo, na wababaishaji.

..Mzee Mwinyi ni fisadi tu, na hatujasahau uchafu aliofanya alipokuwa madarakani.

..wakati wa utawala wake wafadhili walitususia kwasababu kwa kuendekeza rushwa serikali ilikuwa haikusanyi kodi. hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema wazi kwamba serikali inanuka rushwa.

..moja ya vituko vya kifisadi vya Mzee Mwinyi ni kumtoa kifungoni rubani aliyekamatwa airport DSM akitorosha madini na vito.

..Mzee Mwinyi tena anahusika katika kashfa ya mbuga ya Loliondo, na mshirika wake mkubwa ktk kashfa hiyo alikuwa ni Lt.Col.Abdulrahman Kinana.

..Kinana amekuwa campaign manager wa CCM tangu tuingie ktk mfumo wa vyama vingi. huyu anajua vyanzo na kuhusika na fedha zote chafu ambazo zimekuwa zikitumika ktk kampeni za CCM.

..hakuna kitakachotokea ndani ya CCM kwasababu ndani ya chama hicho hakuna mwenye MORAL AUTHORITY ya kuyashughulikia matatizo waliyonayo.
 

Forum statistics

Threads 1,250,048
Members 481,189
Posts 29,719,096