Kambi za Lowassa, Sitta zadaiwa kuipasua CCM

Rostam achukua nafasi ya Lowassa

Mwandishi Wetu
Raia Mwema
Februari 17, 2010
bul2.gif
Sasa suluhu ni yeye na Spika Sitta


bul2.gif
Lengo ni 'kumfunika' Lowassa


MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz, ametajwa kuchukua nafasi ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, katika kuongoza kundi linalopingana na la Spika na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta, wote wakiwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) iliyoshindwa kumaliza uhasama wa makundi hayo wiki hii.
Habari za ndani ya kikao cha NEC kilichomalizika usiku wa manane kuamkia jana Jumanne, zinaeleza kwamba hata Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, alionyesha kumtaja Rostam kama kiongozi wa kundi linalohasimiana na Spika Sitta na wenzake. Hata hivyo, Rostam hakuwapo katika kikao hicho.
rostam_3.jpg


MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz

Kwa mujibu wa habari hizo, hata kamati ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi yenye wajumbe wengine wawili, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na Abdulrahman Kinana, iliyoundwa kubaini suluhu ya mpasuko miongoni mwa wabunge na kwa upande wa Zanzibar miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watokanao na CCM, ilionyesha kumtaja Rostam badala ya Lowassa kama kiongozi wa kundi hilo linalohusishwa na tuhuma za ufisadi.
"Sasa naona hata Mwenyekiti (Kikwete) na Kamati ya Mzee Mwinyi wanamkwepa Lowassa na kuzungumzia kusuluhisha kundi la Rostam na kundi la Sitta, hii inaasharia malengo mahususi ya kumuondoa Lowassa katika mjadala huo," anasema mjumbe mmoja wa NEC, ambaye anafahamika kutofungamana na kundi lolote kati ya hayo mawili.
Mjumbe huyo ameendelea kulieleza Raia Mwema kwamba mkakati huo unaweza kuwa na malengo ya kumbeba ama kummaliza Lowassa, lakini alionyesha kutoridhishwa kwake na jinsi Kikwete anavyoendesha vikao na kusema, "ameonyesha upungufu wa kiuongozi."

Ndani ya NEC kuliibuka mgawanyiko wa waziwazi baadhi wakitaka Lowassa na wenzake wawajibishwe kwa kukichafua chama huku wengine wakitaka asafishwe na kwamba "kama ni suala la ufisadi CCM kama chama kitawajibika na si mtu mmoja."

Mmoja wa waliozungumzia suala hilo la Lowassa ni Mbunge wa Ukonga na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga ambaye alipendekeza kwamba Lowassa asafishwe.
Lakini habari zinasema baada ya Mahanga kutoa hoja hiyo, alijibiwa na Msekwa kwamba hakukuwa na haja ya kusafishana kwa vile kwa mujibu wa Kamati yao hakukuwa na upande uliokosa.

Taarifa zinasema kwamba Mahanga aliambiwa kwamba Lowassa, kama alivyokuwa Mwinyi aliyejiuzulu katika miaka ya 1970 kwa mauaji ya Shinyanga akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, aliwajibika kisiasa na kwa ajili hiyo hakuna kikao kinachoweza kumsafisha, bali alisafishwa na umma.

Ni katika hatua hiyo, ambapo Mwenyekiti Kikwete alipoingilia akisema kwamba mazungumzo ya Kamati ya Mwinyi na pande hizo mbili yalishindwa kuzaa matunda yaliyotarajiwa na ndiyo maana panahitajika muda zaidi kwa kamati.

Taarifa zinasema pia kwamba mjumbe mwingine alidai matatizo ya CCM yametokana na mitandao ya ndani ya vyama hivyo na kwa kwamba inatakiwa ifutwe ili kuleta amani ndani.

"Hoja hiyo ya wanamtandao ilichangiwa na wengi huku kigogo mmoja akisema makundi yanayopingana sasa yalikuwa ni ya ambao wote walikuwa kwenye mtandao. Akasema kinachoonekana sasa ni mfano wa yale yanayotokea katika uwanja wa mpira pale wachezaji wanapopigana ngwala na kukwatuana," anasema mjumbe mmoja.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwa siku mbili kikitanguliwa na kikao cha kamati ya maadili na kamati kuu, Msekwa alisoma taarifa fupi na kuomba kuongezewa muda na baadhi ya wajumbe kuchangia mjadala.

Hata hivyo, mwenendo wa mjadala wa NEC umedaiwa kutoridhisha baadhi ya wajumbe na hususan waliomo katika makundi hasimu wakiamini kuwa kamati imehofia kutekeleza wajibu wake na hasa kuwaadhibu waliobanika dhahiri kukiuka misingi ya kuanzishwa kwa chama hicho.

"Humo ndani wamejaa ‘wasanii' wengi tu…kama ripoti ya Richmond imezimwa kienyeji tu bungeni ambako kuna watu makini zaidi kuliko humo kwenye NEC, unatarajia humo kuwe na jambo kubwa?" alidokeza mjumbe mmoja kutoka kanda ya ziwa, usiku baada ya kikao kuhitimishwa katika mazungumzo yake na Raia Mwema.

Licha ya kupitishwa kwa uamuzi huo baadhi ya wajumbe wenye ushawishi mkubwa katika kikao hicho na CCM kwa ujumla wameonyesha kutoridhishwa na upotevu wa muda usio wa lazima katika kutatua masuala yanayokihusu chama hicho na taifa kwa ujumla.
"Tatizo kubwa na ambalo kwa kweli ni suala la kukatisha tamaa ni kamati ya Mwinyi kutumia muda mrefu kuhitimisha mapendekezo yao kuhusu baadhi ya viongozi wa chama. Inafahamika na baadhi ya wabunge wamewasilisha ushahidi wao kuwatuhumu baadhi ya viongozi…

"Kuna ushahidi wa wazi wa ukiukwaji wa misingi ya chama lakini kamati badala ya kushughulikia tatizo kwa kutoa adhabu inataka upatanishi. Kila mmoja akikiuka misingi ya chama akifokewa au kukemewa na wanachama wenzake sasa itabidi baadaye wapatanishwe sidhani kama huu ni ufumbuzi.

"Misingi ya chama lazima iheshimiwe na kwa anayekiuka ni lazima aadhibiwe kwa kupewa onyo au vinginevyo. Ni kama vile hatujui chama hiki kimeanzishwa ili kusimamia nini," alisema mjumbe mwingine wa NEC ambaye alishiriki katika kikao hicho kutoka mikoa ya Kaskazini.

Taarifa zaidi kutoka ndani ya kikao zinaeleza kuwa hali ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa kamati hiyo teule ilikuwa dhahiri miongoni mwa wajumbe lakini kama ilivyo kawaida kwa chama hicho hatimaye maombi ya kuongezwa muda yaliridhiwa.

Hali inatajwa na baadhi ya wabunge waliozungumza na Raia Mwema kwa simu na ambao si wajumbe wa NEC wakisema wanasubiri taarifa rasmi za kikao hicho ili kutoa maoni na hata misimamo yao kwa kuwa chimbuko la kuundwa kwa kamati hiyo teule ni wabunge.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari saa nane usiku wa kuamkia Jumanne, Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alizungumzia maombi ya kamati ya Mwinyi kuongezwa muda akisema; "NEC imeona makundi hasimu waendelee kunyweshwa dawa ya Mzee Mwinyi hadi wapone."

Hata hivyo, Chiligati hakuwa tayari kufafanua kati ya makundi hayo mawili hasimu lipi hasa linalostahili kunyweshwa dawa hiyo ili wapone kile ‘wanachougua.'

Kamati ya Mwinyi iliundwa katika kikao kilichopita cha NEC mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuandaliwa kwa jaribio la kumnyang'anya kadi ya uanachama wa CCM Sitta kwa tuhuma za kuruhusu vuguvugu la kashfa ya Richmond kushika kasi bungeni na hatimaye kusababisha Lowassa na waliokuwa mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha kujiuzulu.

Kamati hiyo teule katika utendaji wake ilikutana na wabunge mjini Dodoma Novemba mwaka jana na kuzungumza nao. Katika mazungumzo hayo baadhi ya wabunge waliwasilisha ushahidi wa malalamiko yao dhidi ya wenzao na wengine kubaki wakitoleana maneno makali ya kashfa, na mengine yasiyo ya maslahi kwa Taifa bali maisha binafsi, yakiwamo masuala ya ndoa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ni rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na wajumbe wake wawili ni Pius Msekwa ambaye ni Katibu wa kamati na Abdulrahmani Kinana ambaye ni kada wa siku nyingi wa CCM.

Mara kwa mara, Katibu wa Kamati hiyo Mzee Msekwa alipata kuwaeleza waandishi wa habari kuwa kazi ya kamati hiyo si kufanya ukachero na kwamba isingeweza kuhoji mbunge mmoja mmoja bali ingewaita wote kwa pamoja na kuzungumza nao ili kupata maoni yao katika kikao cha pamoja.
Hata hivyo, kamati hiyo ilifanya hivyo lakini pia ilifikia uamuzi wa kuhoji baadhi ya wabunge mmoja mmoja. Ilibainika kuwa baadhi ya wabunge walijitokeza kutaka kukutana na kamati hiyo faragha na wengine wakiwasilisha ushahidi wa mazungumzo yao.
Kamati hiyo pia ilikutana na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kisiwani Zanzibar na kuwahoji wawakilishi hao kuhusu matamshi yao yaliyohusu suala la mafuta.
Suala hilo lilisababisha watoe kauli kali ambazo hazikufurahisha baadhi ya viongozi wa Serikali ya Muungano.
Mjumbe mwingine aliyezungumza na Raia Mwema kutoka Zanzibar kuhusu kikao hicho alielezea kuibuka kwa wito wa kutaka mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM atoke Pemba, ili kuiwezesha CCM kupata ushindi dhidi ya vyama vingine vya Upinzani hususan Chama cha Wananchi (CUF).
"Ilijitokeza, haikuwa kama ajenda lakini ni suala lililojitokeza kwamba ni wakati muafaka CCM kuwa na mgombea urais kutoka Pemba, jambo ambalo halikuwahi kufanyika miaka yote tangu Mapinduzi ya Zanzibar," alisema mjumbe huyo.
CCM Zanzibar inatarajiwa kuteua mgombea wake wa urais baada ya Rais wa sasa, Amani Abeid Karume kuhitimisha muhula wake wa pili wa uongozi. Karume aliingia madarakani kwa kupishwa na Dk. Salmin Amour ambaye naye aliongoza Visiwa hivyo kwa mihula miwili.
NEC katika kikao chake hiki imetangaza siku ya kuchukua fomu za urais wa Zanzibar kuwa ni Julai Mosi, mwaka huu, siku ambayo pia Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anapaswa kuchukua fomu pia. Wote watatakiwa kurejesha fomu hizo Julai 8, mwaka huu.
 
Mzee Msekwa anawabembeleza akina Rost tamu huenda anataka wamsaidie kumlipia fedha alizokopa ubalozini ufaransa eti kumtibia mwanake aliyeko uingereza ilihali huyo mtoto ni afisa balozi,sasa huyu mzee na njaa yake atakuwa na ubavu gani kwa RA kwanza RA alikuwa bosi wake pale Vodacom,pamoja na kupiga kelele kuwa mheshimiwa hele ya uspika inakutosha achana na Vodacom mzee wa watu akawa amenogewa na njuruku ajabu alipokosa uspika na uenyekiti Vodacom ukaota mbaya,kwa mzee wa tabia hii ninakosa imani ya kumwachia abwabwaje kuhusu mustakabali wa nchi ambayo mafisadi ndio wamekuwa vinara,ndugu zanguni TZ sasa imekuwa kama kisiwa cha Sicily kule Italy ambacho kiliongozwa na Mafia na si serikali na hapa ndipo tulipofika kila kitu ni the don na clan zake akina Mamvi na wapiga filimbi akina Mahanga,Serukamba,Nchimbi nk nk wa kadha
 
..CCM nzima imejaa wezi, wachumia tumbo, na wababaishaji.

..Mzee Mwinyi ni fisadi tu, na hatujasahau uchafu aliofanya alipokuwa madarakani.

..wakati wa utawala wake wafadhili walitususia kwasababu kwa kuendekeza rushwa serikali ilikuwa haikusanyi kodi. hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema wazi kwamba serikali inanuka rushwa.

..moja ya vituko vya kifisadi vya Mzee Mwinyi ni kumtoa kifungoni rubani aliyekamatwa airport DSM akitorosha madini na vito.

..Mzee Mwinyi tena anahusika katika kashfa ya mbuga ya Loliondo, na mshirika wake mkubwa ktk kashfa hiyo alikuwa ni Lt.Col.Abdulrahman Kinana.

..Kinana amekuwa campaign manager wa CCM tangu tuingie ktk mfumo wa vyama vingi. huyu anajua vyanzo na kuhusika na fedha zote chafu ambazo zimekuwa zikitumika ktk kampeni za CCM.

..hakuna kitakachotokea ndani ya CCM kwasababu ndani ya chama hicho hakuna mwenye MORAL AUTHORITY ya kuyashughulikia matatizo waliyonayo.

Good points Joka

Kumbuka vilevile fagio la chuma alilokabidhiwa pale magogoni aliliuza kwa mafisadi ati ndiye asuluhishe. Wanakula pesa za walipa kodi hawana lolote. Jakaya mwenyewe kwa nini aligombea kazi ambayo haiwezi?
 
mimi nashangaa sana jinsi kesi za ngiri zinapoamuliwa na nguruwe halafu sisi tunashangaa.... CCM yote ina ilani moja na dira moja tu!!!

so if you are in then you are in for everything, bahati mbaya sana ndio chama tawala
 
Back
Top Bottom